Halmashauri Ya Lindi Vijijini Kuwa Halmashauri Ya Mtama

Rais Magufuli ameagiza Halmashauri ya Lindi Vijijini kuitwa Halmashauri ya Mtama na Makao Mkuu ya Halmashauri hiyo yahamishiwe Mtama kutoka Mjini

Amesema, ndani ya siku 15, Viongozi wa Halmashauri hiyo watoke Mjini na kuhamia Mtama na hiyo ndio italeta maendeleo kwani kama ni giza ndio watashughulikia umeme haraka

“Najua kulikuwa na mabishano, wapo wanaotaka Makao Makuu yaende Subi, wapo waliotaka yaende Mchinga, wapo waliotaka yaende Rondo, kila mmoja anataka la kwake

“Kwa kuwa mimi ndio Rais, na mimi napasua katikati kwa kufuata haki, nimetoa maagizo, Manispaa ya Lindi itachukua eneo lake iliyokuwa nalo mpaka Mnazi Mmoja hadi Mingoyo na kuongezewa eneo la Mchinga.”-Rais Magufuli


from MPEKUZI

Comments