Familia Yakaa Chini ya Ardhi kwa Miaka 9 Ikisubiri Mwisho wa Dunia

Familia moja iliyoishi katika chumba cha chini ya ardhi kwa miaka tisa "ikisubiri mwisho wa dunia" imepatikana na polisi nchini Uholanzi

Mwanamume wa miaka 58, na watoto wake sita walio na umri kati ya miaka 16 hadi 25 - walikuwa wakiishi katika shamba lao katika mkoa wa kaskazini wa Drenthe.

Walipatikana baada ya kijana wake mkubwa kuenda kununua pombe katika baa moja karibu na kijiji cha Ruinerwold, na kumfahamisha mhudumu wa baa hiyo kwamba anataka usaidizi,Kituo cha Televisheni cha RTV kiliripoti.

Waliomuona kijana huyo wanasema alionekana kana kwamba amechanganyikiwa.

Familia yake imekuwa ikiishi kwa kujitenga ikisubiri mwisho wadunia, RTV iliripoti.

"Aliagiza chupa tano za bia na kunywa zote. Baada ya hapo nilisema nae kidogo ndipo alipofichua kuwa ametoroka na kwamba anaomba usaidizi... tukapiga simu polisi," mmiliki wa baa hiyo Chris Westerbeek alikifahamisha kituo cha RTV.

Aliongeza kuwa: "Alikuwa na nywele ndefu, ndevu chafu,nguo zilizochakaa na alionekana kana kwamba amechanganyikiwa. Alisema hajawahi kwenda shule na kwamba hajawahi kunyolewa nywele kwa miaka tisa ."
 
"Alisema ana ndugu na dada zake ambao wanaishi katika shamba hilo. "

Maafisa walitembelea makaazi hayo ya vijijini ili kufanya upekuzi zaidi. Waligundua ngazi iliokuwa nyuma ya kabati katika sebule ya nyumba hiyo ambayo inaelekea chumba cha chini ya ardhi ambako familia hiyo ilikuwa ikiishi.

Polisi imethibitisha mjini Drenthe  kuwa mwanamume huyo wa miaka 58 amekamatwa na kuongeza anafanyiwa uchunguzi-baada ya kukataa kushirikiana nao. 

-BBC


from MPEKUZI

Comments