Operesheni nyakua nyakua yawanyakua madereva 57 wa pikipiki wasio tii sheria bila shuruti Kahama.

NA SALVATORY NTANDU
Madereva pikipiki maarufu kama bodaboda 57 wamekamatwa na Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama barabarani mkoani Shinyanga baada ya kubainika kukiuka sheria za usalama barabarani ikiwemo kupakia abiria zaidi ya mmoja na wengine kutokuwa na kofia ngumu.

Ukamataji huo imefanyika wilayani kahama na kuongozwa na Mkuu wa kitengo cha Usalama barabarani mkoa WA Shinyanga, Athony  Ngwandu na kusema kuwa Oparation Nyakua nyakua tayari imeshaanza kutekelezwa kwa mkoa mzima na kwa dereva yeyote atakayekiuka sheria za usalama barabarani atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Amesema Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa madereva bodaboda wazembe ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani huku baadhi ya madereva waliokamatwa katika operation hiyo wakiwaomba madereva wenzao wazingatie sheria  hizo.

Amefafanua kuwa miongoni mwa makosa ambayo wamekatwa waendesha bodaboda hao ni pamoja na kuzidisha abiria,kutokuwa na kofia ngumu,kutozingatia matumizi ya alama za barabarani kama vile taa na vivuko vya watembea kwa miguu.

Paschal mihayo, na Fundikira saidi ni miongoni mwamadereva waliokamatwa katika oparatisheni hiyo ya nyakua nyakua wamekiri kukiuka sheria za usalama barabarani na kuwataka madereva wenzao kuhakikisha wanatii sheria bila shuruti

Wameliomba Jeshi la polisi kuendelea kutoa elimu kwao ili kuhakikisha sheria hizo zinaheshimiwa ili kuzuia ajali ambazo zimekuwa zikitokea kwa kutozingatia sheria za usalama barabarani.


from MPEKUZI

Comments