Katika Kuelekea Mtihani Wa Kuhitimu Elimu Ya Msingi, CWT Yawataka Waalimu Kuwa Waaminifu Na Watulivu.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Katika kuelekea mtihihani wa Kuhitimu Elimu ya Msingi,Walimu wa shule za Msingi Nchini, wameshauriwa kuwa Waaminifu na Watulivu katika kipindi hiki ambacho Wanafunzi wa Darasa la Saba wanatarijiwa kufanya Mitihani ya kuhitimu Elimu ya Shule ya Msingi.
 
Hayo yamebainishwa mapema leo na katibu wa Chama cha Walimu Nchini CWT, Bwn Deus Seif katika Mkutano na Waandishi wa Habari Jijini hapa ambapo amesema kipindi hiki, mara nyingi kumekuwa na changamoto mbalimbali ambazo hujitokeza, hivyo  vyema Walimu wakaweza kujiepusha nazo.
 
Ameongeza kuwa kutokana na Uaminifu kupungua kwa baadhi ya walimu,  imepelekea zoezi la usimamizi wa Mitihani wapewe Askari Mgambo hali ambayo ni tofauti na awali huku akiwashauri walimu hao kufanya jitihada za kurudisha imani iliyokuwepo awali.

Aidha Bwn Deusi amesema anaimani na Serikali juu ya Maandalizi ya Zoezi zima la usimamizi wa mitihani kwa Wanafunzi na Walimu, kwa kuhakikisha mazingira yanakuwa wezeshi na rahisi kwao kama ilivyokuwa kwa mwaka uliyotangulia.

Wanafunzi wa Darasa Saba kesho Jumaatano September, 11 wanatarajiwa kufanya mitihani wa kuhitimu shule ya msingi ambapo Bwn Deusi ametumia fursa hiyo kuwatakia Walimu na Wanafunzi maandalizi mema ya Mtihani huo.


from MPEKUZI

Comments