#Kimataifa: Urusi kuchukua hatua kukabiliana na tishio linalotokana na Marekani kujitoa kwenye mkataba wa makombora ya masafa ya kati

Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema nchi yake itatumia makombora ya aina kadhaa kukabiliana na tishio linalotokana na Marekani kujitoa kwenye mkataba wa makombora ya masafa ya kati.

Rais Putin amesema hayo kwenye mkutano na wajumbe kadhaa wa kudumu wa baraza la usalama la shirikisho la Urusi, huku akisema Marekani imejitoa katika mkataba huo kwa kisingizio cha kufikiria na kuvunja mkataba huo wa kimsingi katika sekta ya udhibiti wa silaha. 

Hatua hiyo imeifanya hali ya dunia kuwa na utata zaidi na kuleta hatari kubwa kwa pande mbalimbali. Amesema Marekani inawajibika na hali hiyo.

Rais huyo ameamuru wizara ya ulinzi, wizara ya mambo ya nje na idara ya ujasusi kufuatilia hatua za Marekani katika utafiti, utengenezaji na upangaji wa makombora ya masafa ya kati na mafupi, na Urusi  itachukua hatua sawa kujibu hatua za Marekani.


from MPEKUZI

Comments