#Kimataifa: Korea Kaskazini yaonya dhidi ya kupelekwa mifumo ya makombora Korea Kusini

Korea Kaskazini imesema leo kuwa jaribio lolote la Marekani la kupeleka mifumo ya makombora ya masafa ya kati nchini Korea Kusini litazusha zama mpya za vita baridi na kuzidisha mashindano ya kuunda silaha kwenye rasi ya Korea. 

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Mark Esper alisema mapema mwezi huu kuwa anaunga mkono kupelekea mifumo ya makombora ya masafa ya kati barani Asia, sikummoja baada ya Marekani kujitoa kutoka mkataba na Urusi wa kuzuia uundaji makombora ya nyuklia. 

Korea Kaskazini imesema mpango huo wa Marekani unalenga kutanua nguvu zake kwenye eneo la Kaskazini Mashariki ya Asia na siyo kutoa ulinzi kwa Korea Kusini dhidi ya kitisho kutoka mataifa hasimu.

Korea Kusini kwa upande wake imesema hakujafanyika mazungumzo yoyote ya kuweka mifumo ya makombora ya Marekani nchini humo na hadi sasa hakuna mipango ya kufanya hivyo.


from MPEKUZI

Comments