Shule 10 bora matokeo ya kidato cha Sita 2019

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato sita mwaka 2019 na kutaja shule kumi bora  zilizofanya vizuri katika mtihani huo.

Akizungumza leo Alhamisi Julai 11, 2019 visiwani Zanzibar wakati akitangaza matokeo hayo katibu mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde amesema shule iliyoshika nafasi ya kwanza ni Kisimiri ya mkoani Arusha iliyokuwa na watahiniwa 60.

Msonde amesema Feza Boys ya jijini Dar es Salaam yenye watahiniwa 87 imeshika nafasi ya pili ikifuatiwa na Ahmes ya mkoani Pwani iliyokuwa na watahiniwa 112.


from MPEKUZI

Comments