Mwakembe Akerwa na uamuzi wa Shirikisho la Soka nchini TFF kumtimua kocha Emmanuel Amunike.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa rai yake kufuatia uamuzi wa Shirikisho la Soka nchini TFF kumtimua kocha Emmanuel Amunike.

Mwakyembe amesema kuwa kama TFF wameamua kufuata nyayo za Misri katika kumfuta kazi Amunike basi na wao wanapashwa wakamilishe mchakato kwa kujiuzulu nafasi zao.

"Sisi hatuna tatizo na maamuzi ya TFF endapo tu yatatupeleka mbele, lakini kama ni uamuzi wa kuwaiga Wamisri baada ya kutolewa AFCON, hayo ni makosa makubwa sana kwa sababu kama unaiga basi nao wakamilishe kwa kujiuzulu safu nzima ya uongozi", amesema Waziri Mwakyembe.

"Mimi ubabaishaji katika soka siwezi kukubaliana tena, kama nilivyosema juzi kwamba bora tuishie kucheza karata tu kama tunaona ndiyo sawa kuliko kuingia kwenye soka la ubabaishaji. Tunaingia kwenye ligi mpangilio hovyohovyo na wanaoharibu hakuna anayewajibika", ameongeza.

Pia amesema kuwa ametoa hadi 24 Julai kwa benchi la ufundi la Taifa Stars na Viongozi wa TFF kutoa ripoti yao ya michuano ya AFCON kwa ajili ya kujadiliwa.


from MPEKUZI

Comments