Halmashauri Zote Za Wilaya Mkoani Kagera Zabainika Kujihusisha Na Vitendo Vya Rushwa Kwa 38.8%

NA AVITUIS BENEDICTO KYARUZI, KAGERA
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoani Kagera imezitaja  Halmashauli zote za wilaya   Mkoani hapa kuongoza  kulalamikiwa katika vitendo vya Rushwa   kwa kupokea jumla ya malalamiko  87 sawa asilimia  38.8,  ikilinganishwa na sekta nyinginezo. 

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Kagera Bwana John K. E Joseph wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo kuanzia mwezi April hadi June mwaka huu kwa waandishi wa habari mkoani Hapa. 

Bwana John Joseph amesema licha ya juhudi kubwa zinazofanywa Taasisi hiyo lakini bado vitendo vya Rushwa vinazidi kuutafuna mkoa wa Kagera ambapo Mashtaka yaliyofunguliwa ni pamoja na  watuhumiwa 28 kufikishwa mahakamani katika kipindi cha miezi 3 ambapo 18 ni wajumbe wa mabaraza ya kata ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba. 

Amesema kuwa katika Mashtaka hayo mmoja ni mtu aliyejifanya mjasiliamali kumbe Tapeli, wengine ni wafanyabiashara na watumishi mbali mbali wa serikali huku mwezi April hadi juni mwaka huu taarifa 224 zilipokelewa majalada 35 yalifunguliwa kesi 9 zilifunguliwa mahakamani, kesi 50 zinaendelea mahakamani, kesi zilizoshinda mahakamani  ni 2 na kesi 2 zilizoshindwa mahakamani. 

Akitoa  mchanganuo huo wa malalamiko Mkuu huyo wa TAKUKURU Mkoani hapa amesema kuwa malalamiko  yaliyopokelewa kisekta katika Halmashauri za wilaya mkoani Kagera Halmashauli zote za wilaya  mkoani hapa zimeongoza  katika  kulalamikiwa kwa vitendo vya Rushwa   na kudai kuwa  jumla ya malalamiko  87 sawa asilimia  38.8,ambapo sekta ya Ardhi malalamiko 21 sawa na 9.4%, uvuvi 14 sawa na 6.7% Mahakama 13 sawa na 5.8% Polisi 11 sawa 4.9% Afya 9 sawa na 4.0% Taasisi za fedha 9 sawa na 4.0% Elimu 8 sawa na 3.6, Tanesco7 sawa na 3.1% T.R.A 5 sawa na  2.2% Ofisi ya mkuu wa mkoa 3 sawa na  1.3%, Huku sekta nyinginezo zikipokea malalamiko 22 sawa na 9.8%.   

amesema kuwa kwa kipindi cha miezi mitatuTakukuru imeweza kuchukua hatua  mbali mbali katika kukabiliana na vitendo vya Rushwa ambavyo vinafanywa na baadhi ya watu ambao kwa makusudi wanajaribu kujihusisha na vitendo hivyo kinyume na sheria za nchi. 

Katika mapambano dhidi ya vitendo hivyo Mkuu huyo ametoa wito kwa watumishi wa umma na watanzania wote kwa ujumla hasa waishio mkoani hapa kujiepushe na vitendo vya Rushwa vinginevyo watalipia matendo yao hayo kwa uchungu na kwa majonzi makubwa pale watakapofungwa jela.


from MPEKUZI

Comments