Mke wa Kisena wa Udart naye Kafutiwa Mashitaka

Florencia Membe ambaye ni  mke wa  mkurugenzi wa mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (Udart), Robert Kisena amefutiwa mashtaka na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu.

Florencia ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Zenon Oil Gas Limited alikuwa akikabiliwa na makosa saba likiwamo la kuisababishia hasara ya Sh2.4bilioni kampuni ya Udart.

Mshtakiwa huyo amefutiwa kesi hiyo leo Jumatano Mei 15 chini ya kifungu 91(1) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai (CPA) sura ya 20 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Awali, wakili wa Serikali, Grory Mwenda aliieleza Mahakama hiyo kuwa, shauri hilo lilikwenda kwa ajili ya kutajwa lakini Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ameeleza hana nia ya kuendelea nalo.

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile alisema DPP ameliondoa shtaka hilo hivyo anamuachia huru mshtakiwa huyo kwa kutumia kifungu namba(91) cha CPA sura ya 20 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.


from MPEKUZI

Comments