Ewura yaagizwa kupitia bei za dawa za kutibu maji

Waziri wa Maji, Prof.Makame Mbarawa ameagiza kwa  Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuhakikisha inafanya mapitio ya bei za dawa za kutibu maji na kuishauri serikali ili kuweka gharama nafuu.

 Prof.Mbarawa ametoa kauli hiyo leo wakati akizindua ripoti za utendaji wa mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira kwa mwaka wa fedha 2017/18 ambazo zinahudumia miji mikuu ya mikoa na miradi ya kitaifa kwa mwaka huo wa fedha.

Amesema kuwa bei za kutunzia maji kwa sasa gharama zake ni kubwa na kuwataka kuitumia Bohari ya Dawa nchini (MSD) kwakuwa wanaweza kuwa na gharama ndogo kuliko zinazotozwa na watu binafsi.

“Pitieni bei za watu binafsi na zile zinazotolewa na MSD ili mtushauri sisi serikali sehemu nzuri ya kununua ambayo inagharama nafuu, ua mamlaka za maji haziwezi kufurahia kwa kuwa wanamaslahi nako,”amesema.

Akizungumzia utendaji wa mamlaka za maji, Prof.Mbarawa amesema kuwa umekuwa ukisuasua kutokana na kutokuwa na elimu ya uendeshaji hivyo watumie muda wao kuwapa elimu na semina kwa viongozi wa taasisi.



from MPEKUZI

Comments