CUF Zanzibar kukagua ofisi zake Zilizobadilishwa Rangi

Makamu mwenyekiti wa CUF Zanzibar,  Abass Juma Muhunzi amesema chama hicho kitafanya ziara katika ofisi zake zote Zanzibar baada ya kumalizika kile alichokiita ‘vurugu’ alizodai kufanywa na wanachama wa chama cha ACT-Wazalendo.

Ametoa kauli hiyo jana Alhamisi Machi 21, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari kuzungumzia vitendo vya ofisi za CUF kubadilishwa kuwa na ACT, baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kujiunga na ACT.

Alisema licha ya kuwa na mpango wa kuyatembea matawi hayo ili kupanga mikakati kichama, lakini wakati huu hawawezi kufanya hivyo kutokana na wanachama wa ACT kupaka rangi za chama hicho ofisi za CUF.


from MPEKUZI

Comments