Askari wanne wasimamishwa kazi kwa kuingiza simu na dawa za kulevya gerezani

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amemuagiza Kamishna Jenerali wa Magereze, Phaustine Kasike kuwasimamisha kazi Askari wanne wa Gereza la Ruanda jijini Mbeya kwa tuhuma za kushirikiana na wafungwa kuingiza simu na dawa za kulevya ndani ya Gereza.

Masauni alitoa agizo hilo jana alipokuwa anazungumza na wandishi wa Habari kwenye Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoani wa Mbeya ambapo alisema alibaini ukiukwaji huo wa sheria na maadili ya magereza alipofanya upekuzi kwa kushirikiana na baadhi ya maofisa wa Gereza hilo.

Alisema katika upekuzi huo waliwakuta wafungwa wakiwa na simu Tisa pamoja na dawa za kulevya aina ya bangi ambazo ziliingizwa gerezani kwa ushirikiano wa maaskari na wafungwa hao.

Aliwataja askari waliohusika kwenye tukio hilo ambao wanatakiwa kusimamishwa kuwa ni Inspecta Longino Mwemezi, WDR Ramadhan Mhagama na wengine Sajinitaji Alexander Mwijano na Benjamini Malango wote wenye cheo cha Sajintaji.


from MPEKUZI

Comments