Waziri wa Madini, Doto Biteko Awasimamisha Kazi Watumishi Wawili

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameagiza kusimamishwa na kuchukuliwa hatua kwa watumishi wawili wa wizara yake kwa kutoa leseni ya uchimbaji madini ya Tanzanite kwa wageni kinyume cha Sheria ya Madini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Februari 18, 2019 jijini Dodoma, BIteko amesema watumishi hao  walitoa leseni hizo za uchimbaji wa madini hayo kwa raia wa Kenya kinyume cha Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na marekebisho yake ya mwaka 2017.

Amesema kifungu hicho kinakataza leseni ndogo za uchimbaji (PML) kutolewa kwa wageni.

Pia ameagiza kufutwa kwa leseni hizo tatu na maombi ya leseni tisa ambayo yako katika hatua mbalimbali.

 “Naagiza Tume ya Madini kufuta leseni na maombi hayo mara moja na wahusika wote walioshiriki katika utoaji leseni hizo wasimamishwe kazi na kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa kanuni za utumishi mara moja kuanzia leo,” amesema.


from MPEKUZI

Comments