RC Makonda Atimiza Ahadi Ya Kumpatia Mtaji Wa Milioni 5 Mama Mzazi Wa Marehemu Msanii Godzilla

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda  ametimiza ahadi aliyotoa ya kumpatia Mama Mzazi wa Marehemu Msanii Godzilla kiasi cha shilingi milioni 5 kama mtaji wa kufungua duka la kisasa la kuuza dawa za binadamu (pharmacy) itakayowezesha familia kujikwamua kiuchumi.

February 16 wakati wa maziko ya Msanii Godzilla,mama yake alisema Godzilla alikuwa na ndoto ya kumpatia  mtaji wa shilingi milioni 5 kwaajili ya kufungua Pharmacy itakayomsaidia kuendesha maisha na tayari alikuwa ameshamkabidhi milioni 4 lakini baada ya Marehemu Godzilla kuugua ghafla Mama huyo alisema alilazimika kutumia fedha hizo kumuuguza mwanae na kusababisha fedha kuisha. 

Baada ya kusikia hilo, RC Makonda alimfuta machozi mama huyo na kumuahidi kumkabidhi Fid Q pesa hiyo ili mama atimize ndoto yake kitu ambacho amekitekeleza jana


from MPEKUZI

Comments