Meneja mawasiliano TFS afariki dunia akizungumza na waandishi wa habari

Meneja mawasiliano wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Glory Mziray kufariki dunia jana mchana Jumanne Februari 19, 2019.Glory amefikwa na umauti wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Hali yake ilibadilika ghafla muda mfupi baada ya kumaliza kusoma taarifa ya TFS kuhusu upandishaji hadhi wa misitu.

Inaelezwa kuwa meneja huyo alizungumza kwa uchangamfu na alipomaliza alionekana kama kuishiwa nguvu na kupoteza fahamu.

Alikimbizwa katika kituo cha Afya TMJ kilichopo Chang’ombe kwa ajili ya matibabu.

Baada ya kumfanyia uchunguzi madaktari wakaeleza kuwa Glory amefariki dunia kabla ya kufikishwa hospitalini hapo.
**********
Mtendaji Mkuu  wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) anasikitika kutangaza kifo cha mtumishi wake Glory Water Mziray aliyekuwa  Meneja Habari na Mawasiliano kilichotoke  Jumanne 19 Februari 2019 mchana mara baada ya kujisikia vibaya akiwa anatekeleza majukumu yake kwa kuongea na waandishi wa habari ofisini na kukimbizwa katika Hospitali ya TMJ Temeke ambapo madaktari walithibitisha kuwa amefariki dunia. Mipango ya Mazishi inafanywa.

Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake  lihimidiwe amen!

Imetolewa na
Utawala- TFS Makao Makuu


from MPEKUZI

Comments