Manispaa ya Iringa yaongoza kwa ukusanyaji mapato

 Na Amiri kilagalila
MADIWANI  wa  halamshauri ya Manispaa ya  Iringa  mkoani  Iringa  wameipongeza  halmashauri  hiyo  kwa  kuendelea  kuongoza  kitaifa  katika ukusanyaji  wa mapato  kwa kundi la  Halmashauri za  Manispaa nchini .

Madiwani hao  walitoa  pongezi hizo jana  mara  baada ya  taarifa ya  mstahiki meya  wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe  kutoa taarifa  rasmi katika  kikao hicho kuhusu  Manispaa ya  Iringa  kuongoza  kwa  ukusanyaji wa mapato kwa  mwezi Januari .

Diwani  wa kata ya Mwangata Edward  Chengula  alisema  kuwa  ni hatua  ya  kujipongeza kwa  halmashauri  hiyo ya  Manispaa ya Iringa  kuendelea  kufanya  vizuri  katika  ukusanyaji wa mapato  na kuwa kinachoendelea ni uwajibikaji mzuri wa  watendaji wa halmashauri hiyo  chini ya mkurugenzi  wake Hamid Njovu pamoja  na  madiwani .

Alisema  pamoja na  kufanya  vizuri katika  ukusanyaji wa mapato , Manispaa ya  Iringa  ni  moja kati ya Halmashauri  ambazo zimefanya  vizuri katika  zoezi la  ujenzi wa vyumba vya madarasa na  kufanikiwa  kupeleka wanafunzi wote  waliofaulu  mtihani wa darasa la  saba  kujiunga na  sekondari .

" Ushirikiano  uliopo  ndio ambao  umepelekea  Halmashauri  yetu  kuendelea  kuwa  wamoja na  kuwatumikia  wananchi kwa  nguvu ya  umoja  bila kuwepo mivutano  ya kisiasa  hadi  sasa mfano kata  yangu ya Mwangata  najivunia  kuona  watoto  waliofaulu kujiunga na elimu ya  sekondari  wote  wanakwenda  shule  ila  pia  kuna  maendeleo makubwa  yanayofanywa katika kata ya Mwangata " alisema Chengula

Naibu  meya wa Manispaa ya  Iringa Joseph Lyata  alisema  kuwa  kuongoza kwa  Manispaa hiyo  katika  ukusanyaji  kodi ni ishara  nzuri  kuwa  wananchi  wa Manispaa ya  Iringa  wameitikia wito wa  serikali ya  awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt  John Magufuli ya  kila mmoja  kulipa  kodi kwa maendeleo ya  Taifa .

Naye Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa, Ritta Kabati (CCM) na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa, Suzana Mgonakulima (Chadema) wamesema kuwa mbali na kuipongeza manispaa yao kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato ila wanapongeza kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa ambavyo vimepelekea watoto wote kwenda shule . .


from MPEKUZI

Comments