Majizo Ajitoa Muhanga Sakata la Matibabu ya Ruge Mutahaba

Mkurugenzi wa EFM na E-TV, Majizo ameunda kamati ambayo itaratibu namna ya kukusanya fedha za kusaidia mtibabu ya mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba ambaye yupo nchini Afrika Kusini kwa matibabu.

Akihojiwa leo Jumatano Februari 20, 2019 katika kipindi cha 360 kinachorushwa na kituo cha Clouds TV, Majizo amesema tayari kamati ya kufanikisha uchangishaji wa matibabu hayo imeundwa na imeanza kukutana jana.

Amesema Watanzania watarajie kamati hiyo itafanikisha walilokusudia na kuwaomba wasiache kuwapa ushirikiano pale watakapowafuata kueleza walichoamua kufanya katika kufanikisha matibabu hayo.

"Undugu, urafiki na ukaribu wetu hauwezi kufa kwa sababu ya kazi zetu kwani ukitaka kuwa mfanya biashara mzuri hutakiwi kuchukulia vitu personal kwenye kazi huwa tunafanya kazi, na ili ukae muda mrefu kwenye biashara hutakiwi kuchukulia vitu personal na ukichukulia personal lazima upotee”

“Kabla sijafungua redio nilimwambia Ruge nataka kufungua redio akaniambia kwa sababu unaweza vitu vingi fungua, nilitaka kumfanyia surprise na nilivyofungua nikamwambia tayari nimefungua. Alinipongeza kwa furaha karibu kwenye game.”

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa zake za kuumwa na kwa nafasi yangu nitaonyesha jinsi gani nimeguswa tutajitoa kwa namna yoyote kupitia vyombo vyangu vya habari au hata mimi personal, ili kuweza kusaidia hili kikubwa ni tuungane kwa pamoja”

‘Kamati ilikutana jana kwa bahati mbaya sikuwepo nilikuwa kwenye kamati zingine mipango haikuwa vibaya imekamilika, kamati yetu italeta mafanikio makubwa lengo letu ni kutaka Ruge arudi akiwa mzima, kikubwa ni ushirikiano pindi tukirudi kwenu wananchi’’

“Baada ya kupata taarifa za Ruge kuumwa, nilitamani miujiza ya haraka na nilikuwa najaribu kuweka karibu mawasiliano, na nilipata ushirikiano kutoka kwa watu wa hapa mjengoni na kunipa taarifa kuhusu hali yake”

“Kuna vitu vingi ambavyo tumepanga kuvifanya kwenye kamati yetu ya kihakikisha Ruge anarudi kwenye game na mwenyikiti wa kamati atakuja kuongea mengi ambayo tumeyapanga na mimi na vituo vyangu ( #TvE na #Efm) tutashiriki kwa pamoja” Amesema Majizo


from MPEKUZI

Comments