DPP aiomba mahakama itupilie mbali rufaa ya Freeman Mbowe na Ester Matiko

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) ameomba Mahakama ya  Rufaa iamuru rufaa iliyofunguliwa Mahakama Kuu na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wakipinga kufutiwa dhamana itupiliwe mbali na kwamba rufaa hiyo ni batili.

Akiiwakilisha Jamhuri mbele ya jopo la majaji watatu, Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi amedai wajibu maombi waliwasilisha rufaa Mahakama Kuu mbele ya Jaji Sam Rumanyika bila kuambatanisha uamuzi wa Mahakama ya Kisutu na mwenendo wa kesi hiyo.

Nchimbi alidai rufaa yao ina sababu tatu ambapo sababu ya pili inayodai kwamba Jaji Rumanyika alikuwa  na upendeleo aliiondoa baada ya jopo kuhoji na kuonekana haijawahi kuwasilishwa Mahakama Kuu.

Jopo la majaji hao, Stellah Mugasha, DK. Gerald Ndika na Mwanaisha Kualiko.

Nchimbi anadai kwa kupokelewa kwa rufaa ya kina Mbowe Mahakama Kuu ikiwa hakijaambatanishwa na uamuzi na mwenendo wa kesi kama Sheria namba 362(1) inavyoelekeza kunaifanya rufaa hiyo kuwa batili na kuonekana haiko sahihi mahakamani.

Kwa upande wa Wakili Peter Kibatala alidai kuhusu lalamiko la kuwa hawakupewa muda wa kutosha wa kusikilizwa, rufaa iliyopo Mahakama Kuu haikusikilizwa na kwamba kilichosikilizwa ni mapingamizi pekee.

Hata hivyo, Jaji Mgasha kwa niaba ya jopo amesema watazingatia hoja zilizowasilishwa na pande zote mbili na kwamba watatoa uamuzi katika tarehe itakayopangwa.

Kibatala amedai sababu za rufaa hiyo hazina mashiko hivyo aliomba Mahakama ya Rufani kuitupilia mbali rufaa hiyo.

Mbowe na Matiko wamerejeshwa Segerea


from MPEKUZI

Comments