Uongozi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Wajibu Tuhuma za Msanii Ray Kigosi Kuibiwa Vitu Vyake

Uongozi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) umewataka abiria wanaodhani wamepoteza vitu vyao wakati wanasafiri kwa kutumia Uwanja huo watoe taarifa mapema ili waweze kusaidiwa kupata vitu vilivyopotea.

Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Paul Rwegasha amesema iwapo mtu atapata tatizo lolote ni vyema akawasiliana na uongozi badala ya kuandika kwenye mitandao ya kijamii kwani atakuwa anaichafua nchi.

Rwegasha amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada  Msanii Maarufu wa Filamu nchini, Vincent Kigosi ‘Ray’ kuandika kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram akieleza aliibiwa vifaa vyake akiwa anaelekea Dubai.

“Wiki iliyopita mliniibia raba pamoja na pafyumu ( mafuta ya manukato), sasa swali langu? Kwa nini uongozi hauwachukulii hatua kali hao wafanyakazi wenu wenye tabia ya udokozi wanaoharibu sifa ya uwanja wa ndege huu wa kimataifa?” Aliandika Ray Kigosi

Mmoja wa wachangiaji ambaye ni msanii mwenzake mwenye jina la @Gabozingamba aliandika ;“Wakati tunakwenda Kigali (Rwanda) nilikuambia wameniibia laptop (kompyuta mpakato) na manukato wamezuia ukaniambia tulia dogo ndiyo ukubwa. Basi na wewe utulie kaka ndiyo uzee huo kumradhi.”


from MPEKUZI

Comments