Spika Ndugai awaombea likizo Mawaziri kwa Rais Magufuli

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndg. Job Ndugai, amewaombea likizo Mawaziri wa Tanzania kwa Rais John Pombe Magufuli.

Spika Ndugai, ametoa ombi hilo kwa Rais Magufuli, leo Januari 9 wakati akiwapongeza viongozi walioapishwa kutumikia nafasi mbalimbali wakiwepo Mawaziri na Makatibu Wakuu.

Mh. Ndugai amesema kwamba Mawaziri wa awamu ya tano wanachapa kazi sana kiasi ambacho hakijawahi kutokea, hivyo ameona bora awaombee likizo japo ya mwezi ili waweze kupumzika.

"Serikali ya awamu ya tano ina kasi ya kipekee sana. Wakati zoezi la kuapishwa linaendelea nikawa naangaliana na waheshimiwa mawaziri wanaonekana wamechoka sana nikajiuliza hivi wanalikizo. Mheshimiwa Rais nawaombea likizo japo ya mwezi kila mmoja mmoja. ", amesema Spika Ndugai.

Hata hivyo, Rais Magufuli amewataka Mawaziri pamoja na watendaji wengine wa Serikali wavumilie tu maana hata yeye hana likizo na hajawah chukua Likizo tangu achaguliwe kuwa Rais


from MPEKUZI

Comments