Mke wa Mzee Yussuf aendelea vizuri....Ni Baada ya Kujeruhiwa na Majambazi Usiku

Hali ya mke wa Mzee Yussuf, Leyla Rashid, inaendelea vizuri baada ya kujeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwili na majambazi waliovamia nyumbani kwake, Chanika, jijini Dar es Salaam, juzi usiku.

Leyla amesema baada ya kupata majeraha hayo alikimbizwa hospitali na kupatiwa matibabu na sasa ameruhusiwa kurudi nyumbani na hali yake inaendelea vizuri.

“Nashukuru kwa sasa naendelea vizuri nimetoka hospitali nipo nyumbani kwangu Chanika, nimegundua vitu ambavyo nimeibiwa vinafika thamani ya shilingi 5,000,000, nashukuru ndugu na jamaa waliojitokeza wakati wa tukio,” amesema Leyla.


from MPEKUZI

Comments