Mahakama Kuu Yaitupilia Mbal Kesi Ya Kupinga Kanuni za Maudhui ya Sheria Mpya Ya Mtandaoni

Mahakama Kuu kanda ya Mtwara leo imetupilia mbali kesi ya kutaka mapitio (Judicial Review) ya Kanuni za Maudhui ya Kimtandao iliyofunguliwa na MCT, LHRC na Muungano wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu(THRDC)

Katika kesi hiyo washtakiwa ni Waziri wa Habari, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mwanasheria Mkuu.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatano Januari 9, 2019 na Jaji Wilfread Ndyansobera.

Katika maamuzi yake Jaji Ndyansobera amesema kwamba maombi ya wapeleka maombi hayana uzito.

Amesema walalamikaji wameshindwa kuthibitisha  jinsi gani Kanuni hizo zitakavyo athiri haki za msingi za Walalamikaji katika masuala ya uhuru wa habari na mawasiliano ya mitandaoni.

Hivyo, amesema Mahakama imekubaliana na hoja za  Mawakili wa Serikali kuwa Kanuni za Maudhui Mtandaoni zimetungwa kwa mujibu wa sheria na kupelekea Mahakama hiyo kutupilia mbali shauri hilo.

Shauri hilo liliendeshwa na mawakili kutoka Ofisi Mpya ya Wakili Mkuu wa Serikali ambao ni Bibi Alesia Mbuya, Bw. Ladislaus Komanya, Bw. Sylvester Mwakitalu, Bw. Johanes Kalungura, Bw. Killey Mwitasi, Bw. Abubakar Mrisha na Bibi Neisha Shao ambapo upande wa walalamikaji waliwakilishwa na mawakili Fulgence Masawe, James Marenga na Jeremia Mtobyesa.

Kwa hukumu ya kesi hiyo iliyofunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara Septemba 4, 2018, sasa ni rasmi madai ya kwamba Kanuni hizo zinabana uhuru wa habari na kwamba zilitungwa kimakosa yaaanguka rasmi.

Kwa kawaida kanuni hizo zilipaswa kuanza kutumika rasmi Mei 5, 2018 lakini Mei 4, 2018 mwaka huu, Mahakama hiyo iliweka zuio la muda baada ya kuwasilishwa kwa shauri la kupinga.



from MPEKUZI

Comments