Lugola Afunguka Baada ya Makamanda wa Polisi Aliowatumbua Kuonekana Wakiendelea na Kazi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola, amesema yeye alishatoa maagizo ya kuondolewa kwenye nafasi zao kwa Makamanda wa Polisi watatu katika Mikoa mitatu ya kipolisi Temeke, Ilala pamoja na Arusha na kilichobaki ni kutekelezwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

Kangi Lugola ameongea na kituo cha televishen cha EATV  baada ya mkanganyiko uliojitokeza kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonakana baadhi ya Makamanda wakiendelea kufanya kazi kwenye vyeo vyao.

"Sina taarifa kwamba agizo langu halijatekelezwa lakini kwa sababu nilimpa muda wa utekelezaji IGP kwa hiyo naamini litatekelezwa, saa nyingine watu hawajui kutengua mtu ni mamlaka na mimi ndiye nina mamlaka.

"Utekelezaji ndiyo unaendelea sidhani kama wamekaidi au IGP amekaidi kutekeleza agizo langu." amesema Kangi Lugola.

Juzi Kangi Lugola alitoa uamuzi huo wa kutengua uteuzi wa makamanda wa polisi wa mikoa mitatu akiwemo Salum Hamduni aliyekuwa Ilala, Emmanuel Lukula (Temeke) kwa kosa la kushindwa kusimamia mianya ya rushwa na utoaji wa dhamana kwa watuhumiwa.


from MPEKUZI

Comments