Kilichoendelea Mahakamani Asubuhi ya Leo Katika Kesi ya Kupinga Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa

Shauri la kupinga muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa ambalo lilipangwa kusikilizwa na jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu leo Ijumaa saa tatu, limehamishiwa kwa Jaji mmoja.

Shauri hili lilipangwa kusikilizwa na jopo linaloundwa na Jaji Barke Sehel (kiongozi wa jopo), Benhajo Masoud na Salma Maghimbi, lakini usikilizwaji huo umekwama baada ya wajibu maombi (Serikali) kuwasilisha pingamizi la awali wakiitaka Mahakama hiyo ilitupilie mbali.

Kutokana na pingamizi hilo, Mahakama ilisitisha usikilizwaji wa shauri la msingi na badala yake ikaamua kuanza kusikiliza pingamizi na ikapanga pingamizi hilo lisikilizwe na jaji Masoud katika chemba kuanzia saa 4:00 asubuhifrom MPEKUZI

Comments