Bunge la Ujerumani Lapiga Kura.....Laukataa Mradi wa Stiegler's Gorge Tanzania

Bunge la Ujerumani limepitisha muswada wa kuitaka serikali ya Ujerumani itafute njia mbadala ya mradi wa Tanzania wa kuzalisha nishati ya umeme katika Bonde la Stiegler kwenye Mto Rufiji, kusini mwa Tanzania ili kulinda turathi na asili.

Wabunge wa vyama vilivyomo katika serikali ya mseto ya Ujerumani; CDU/CSU, Kijani na AFD walishiriki katika kupiga kura hiyo lakini chama cha mrengo mkali wa kulia cha AfD, hakikushiriki. Azimio la vyama vya CDU,CSU na SPD pia linatokana na mapendekezo ya Kamati ya Serikali ya Ujerumani ya Ushirikiano wa Kiuchumi.

Azimio lililopitishwa bungeni na vyama hivyo vilivyomo katika serikali ya mseto ya Ujerumani linaitaka serikali kuu isaidie katika masuluhisho ya kukidhi mahitaji ya nishati ya Tanzania bila ya kuathiri mazingira. Katika azimio lao, vyama hivyo vimesema mradi huo mkubwa wa kuzalisha nishati ya umeme utavuruga mfumo wa mto mmojawapo mkubwa barani Afrika.

Tanzania inakusudia kujenga bwawa kubwa la kuzalisha nishati ya umeme kwa kutumia nguvu ya maji kutoka kwenye Mto Rufiji. Sehemu hiyo ni muhimu kwa shughuli za kilimo za wakazi wake. Ikiwa mradi huo utaendelea,  Bonde la Stiegler ambalo ni miongoni  mwa turathi za Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), litapoteza hadhi yake na huenda likasababisha athari kubwa katika raslimali zilizopo kwenye sehemu hiyo.

Katika ombi lao kwa serikali ya Ujerumani, wabunge wa vyama vya CDU, CSU na SPD wamesema sehemu hiyo ya mbuga ya wanyama ya Selous nchini Tanzania ni eneo kubwa na kongwe la hifadhi ya wanyamapori barani Afrika.

Wabunge hao wamesema mradi huo wa bwawa la nishati utahitaji sehemu kubwa itakayotokana na kukatwa kwa miti na hivyo kusababisha athari kubwa katika mazingira, tabianchi na katika uchumi.

Wabunge wa chama cha upinzani cha FDP wameshauri kujengwa kinu cha nishati kutokana na gesi kwa sababu Tanzania inayo gesi ya kutosha iliyogunduliwa hivi karibuni.   Chama hicho kilichopinga azimio hilo,  kimeitaka serikali ya Ujerumani ifanye mazungumzo na serikali ya Tanzania.

CREDIT: DW


from MPEKUZI

Comments