AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 180 na 181 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA      
 
“Endeleni kusonga mbelee”
Raisi Sound akili zake wala sijui zipo vipi, kwani alicho kizungumza sikielewi kabisa, nikamtazama Ester sikumpa ishara yoyote.
“Siwaui marubani wako, sasa wewe ndio utawaua kwani mashambulizi sasa hivi yatakuja kwako hapo Washington D.C ulipo, jiandae muheshimiwa raisi”
Viongozi  wote wakaanza minong’ono wengi wakionekana kugopa sana kwa kile kitakacho kwenda kutokea hapo baada ya muda mchache. Ester na wezake ambao kwa sasa ndio wana uwezo wa kuziongoza ndege hizo wakafanya kile nilicho kizungumza, na ndege hizo zikageuzwa badala ya kueleke Pakistani zikaanza kueleke Marekani kwenye mji wa Washington D.C na zikifika hapo nilazima zifanye mashambulizi za kulichangua jengo hilo la serikali alipo raisi Sound na viongozi wengine wote na inchi itakosa kiongozi wa kisiasa kwani nilazima wafe.
   
ENDELEA   
“Kimya”   
Raisi Sound alizungumza na kuwafanya viongozi walio anzisha mijadala kunyamaza mara moja. Raisi akaka kimya huku akinitazama mimi, kichwani mwake anaonekana kwamba ana mawazo mengi sana.
“Meli zao za kivita zipo ngapi zilizo ondoka?”
Nilizungumza huku nikimtazama Ester, jambo lililo zidi kuzua taharudi kwa viongozi hawa wa Marekani, kwa ishara ya vidole Ester akanionyesha ni meli nne.
“Kila ndege itapiga meli moja”
Ester akatingisha kichwa akimaanisha kwamba emenilewa nilicho kizungumza.
“Nimebadilisha mawazo yangu, meli zako zitakwenda kushambuliwa na kuteketea, je mimi na wewe nani ni raisi wa Marekani?”
Viongozi wote wakamgeuki raisi huyu aliye chukua madaraka kwani yeye ndio muhusika anaye paswa kujibu swala ambalo nimemuuliza.
“Mimi ndio raisi wa Marekani”
“Basi amuru  meli zako  zishambulie hizo ndege ambazo zitafika eneo hilo baada ya dakika……”
Nikamgeukia Ester, akaniambia kwa sauti ya chini sana ambayo haisikiki.
“Dakika kumi na tisa kuanzia hivi sasa, kwa hiyo ukihitaji vita hii iishe, kubali kuniomba msamaha kuhusiana na makosa aliyo yafanya raisi aliye pita, kisha usahau kwamba kuna mtu anaitwa Dany”
“Siwezi kumsujudi gaidi tena muafrika, nitahakikisha kwamba ninakuangusha”
“Sawa subiri kitakacho tokea”
Nilizungumza huku nikijilaza taratibu katika kiti hichi cha kuzunguka, nikawatazama marubani hawa wanao jitahidi kadri ya uwezo wao kuongoza ndege zao ila wanashindwa kabisa kwani hata mimi mwenyewe sifahamu Ester na wezake wamefanyaa kitu gani hadi kuwadhibiti hizi ndege. Viongozi hawa wakaanza kujadiliana kuna ni jinsi gani wanaweza kumshawishi raisi aweze kufwata kile nilinicho muambia.
“Dakika tano zimebaki”
Nilizungumza na kuwafanya viongozi baadhi kunitazama, huku wengi wao wakiwa wamejawa na wasiwasi mwingi sana.
“Dakika mbili zimebaki muheshimiwa raisi”
Viongozi wakaonekana kuchoka kwani raisi wa sasa hashauriki.
“Puuuuuuu”
Nilizungumza huku nikiitazama Tv ya namba tato ambayo inaonyesha video hizo jinsi zinavyo anza kufanya mashambulizi kwenye meli hizi kubwa za kivita na wanajeshi waliopo kwenye meli hizo wakajikuta wakishindwa kufanya chochote kwa moja ni ndege za nchi yao na mbili ni ndege ambazo zina uwezo mkubwa wa kivita na tatu shambulizi limetokea kwa kustukiza sana. Mashambulizi yakaendelea zaidi ya dakika kumi na kuziteketeza meli hizo zote za kivita.
“Wanajeshi wako wameteketea na wamekufa kutokana na ubishi wako. Ndege zako ninaziteketeza sasa”
Ester na wezake kazi yao ni kufanya kile nilicho waeleza, ndege moja baada ya nyingine ikalipuka na baada ya muda kidogo mabaki ya ndege hizo zikaangukia kwenye bahari.
“Tutaonana baadaye baada ya kuhakikisha kwamba mke wangu munamuachia”
Nikachukua rimoti na kuzima tv zote, nikawageukia watu walipo humu ofisini, kila mmoja yupo kimya akinisikiliza ni kitu gani ninacho kwenda kukizungumza.
“Vita sasa imeanza, ninacho kihitaji wote humu ni kuhakikisha kwamba kila mmoja anakuwa jasiri katika kila kitu kinacho jitokeza mbele yetu”
“Munaweza kukaa”
Livna alizungunza, Martin na wezake wakaanza kukaa kila mmoja kwenye kiti alichokuwa amekikalia.
“Kwa sasa mtu ambaye tunamgeukia ni K2, kifo cha Lucy siwezi kukiacha kipite bure, ninahitaji watu ambao watakwenda kumteka mtoto wa K2”
“Samahani Dany, labda mtoto wa K2 yupo wapi?”
“Ester unaweza kunitafutia huyo kijana”
“Si yule kibonge?”
Ester aliniuliaza huku akinitazama usoni mwake.
“Ndio”
Livna alimjibu, Ester akaanza kuifanya kazi hiyo.
“Kwa sasa mtoto wa K2 yupo nchini China ambapo ndipo anapo soma kwenye shule moja ya Kung Fu. Inaitwa Shing Ku Fu.”
Ester alizungumza huku akitutazama mimi na Livna.
“China nina watu ambao wanaweza kuifanya hiyo kazi”
“Hao watu wanahisiana na kikundi hichi?”
“Ndio wanahisiana na kikundi hichi”
“Basi ninaomba uwasiliane nao, ninahitaji kumuumiza K2 zaidi ya alivyo muumiza waziri mkuu”
Livna akawasiliana na watu hao  alio sema wanaweza kuifanya hiyo kazi, akawapatia maelekezo na watu hao wakaahidi kwamba wanaweza kuifanya hiyo kazi siku hii hii.
“Baada ya muda gani munaweza kuikamilisha”
Livna alizungumza huku akiwa ameiweka simu yake mezani na watu wote ndani ya hichi chumba tunayasikia mazungumzo ya Livna na msichana huyo.
“Baada ya lisaa moja mkuu nitakupigia ni wapi nipo na mtoto huyo”
“Sawa Sara, kuwa makini na hakikisha kwamba kila kitu kinakwenda sawa”
“Usijali mkuu unafahamu kwamba mimi sifeli kwenye kila kazi unayo nipatia”
“Nakuaminia ndio maana nikakukabidhi wewe”
“Basi usiwe na mashaka”
Livna akakata simu na kuirudisha mfukoni mwake.
“Mtoto wa K2 nina imani kwamba atakuwa amepatiwa ulinzi mmoja mkubwa sana”
Winy alizungumza kwa sauti ya upole huku akimtazama Livna.
“Yaaa, ila huyu ni professional killer, ana uwezo mkubwa japo nimempiga ila tupo vizuri sana”
“Hapa tusubirie matokeo”
“Ila inanibidi niende kumpokea, nje ya hii meli kwa mana yeye afahamu ni wapi ninapo jificha”
“Nitakwenda na wewe”
Martin alizungumza na kunitafanya nimtazame.
“Unajiweza Martin kwa maana ni hatari huko tunapo kwenda, dunia nzima inamtamani huyu jamaa na sisi tayari tumesha husishwa katika swala la kumsaidia, sasa je utaweza shuhuli?”
“Nitaweza niamini Livna”
“Sawa, Ester niandalie vijana wawili, baada ya lisaa wawe tayari”
“Sawa mkuu”
“Na wewe Martin ujiandae katika hili tunalo kwenda kulifanya. Logate hakikisha kwamba ulinzi unakiwa juu yetu kila tunapo kwenda muhakikishe kwamba munatulinda”
“Usijali mkuu”
“Dany wewe ndio ninakuacha hapa, nina imani ni mgeni ila una uwezo mkubwa wa uongozi, hakikisha kwamba ulinzi unakuwa imara”
“Usijali, mimi nitaendelea kudili na hawa wajinga”
“Sawa”
Livna akanyanyuka kwenye kiti hichi na kutoka humu chumbani huku akimuita Martin. Winy naye akaondoka humu ndani na nikabaki na Babyanka pamoja na Logate.
“Dany”
“Naam”
“Mtoto wa K2 unahitaji kumfanya kitu gani?”
Babyanka aliniuliza kwa sauti ya upole sana, nikamtazama usoni mwake kwa sekunde kadhaa huku nikiwa natafakari cha kumjibu.
“Nakuomba usimuue”
“Bayanka umekuwaje, mbona una roho ya huruma sana, au umekoka?”
“Hapana sio kuokoa, ninajia Dany hujapata mshauri mzuri mimi ndio mshauri wako kwa sasa”
“Unanishauri pumba muda mwengine, hivi hujawahi kuona picha za familia yangu ehee?”
“Nimesha wahi kuzioana”
“Sasa unacho kihitaji ni nini, unahitaji kumuacha K2 andelee kuishi kwa furaha na asipate machungu kama ninavyo upata mimi?”
“Najua una mamumivu makubwa moyoni mwako. Ila Dany leo umea watu wengi, ingia basi hata likizo ya kuua hawa watu”
“Nisipo waua wao, watania mimi. Kwanza nenda kamtazame Hawa anaendeleaje”
“Sawa”
Babyanka alizungumza huku akishasha pumzi nyingi sana. Akatoka chumbani humu na kuniacha mimi na Logate.
“Huyu dada ni mpole sana hadi sauti yake”
“Huyo alikuwa ni mlnzi mwenzangu”
“Mlinzi kivipi?”
“Tulikuwa tunamlinda raisi aliye pita nchini Tanzania kabla ya K2”
“Kumbe ulikuwa mfanyakazi muaminifu kwa raisi?”
“Ndio, ila alinibadilika na kuniwinda, wakaniuliza familia yangu na mwisho wa siku nikamuaa kubadilika mazima”
“Masikini wee, familia yako wanaitwa nani?”
Nikamtajia Logate jina la mama yangu, akalitafuta kwenye laptop yake, nikamuona akiziba mdomo wake kwa kile alicho kiona.
“Picha ndio hizi?”
Logate alizungumza huku akinigeuzia laptop yake, nikazitazama picha ya mama yangu akiwa amechinhwa kikatili sana, pambeni ya picha hiyo kuna mwanangu wa kike, pamoja na mdogo wangu. Kwa hasira na maumivu niliyo nayo moyoni mwangu, nikajikuta machozi yakinilenga lenga usoni mwangu.
“Ndio hao”
“Masikini jamani pole sana kaka Dany”
“Shukrani”
Livna akaingia humu ndani akiwa amebadilisha nguo, Logate akaigeuzia laptop yake upande wake. Livna naye akatazama picha zilizopo kwenye laptop ya Logate kisha akanitazama usoni mwangu.
“Dany”
Livna alizungumza hukku akikaa pembeni ya kiti kilichopo pembeni yangu, taratibu akanisogelea na kunitazama uosni mwangu.
“Ninakuomba usikumbuke machungu haya, una safari ndefu kwenye maisha yako, ninakuomba uzidi kuwa jasiri”
“Niahidi kitu”
“Zungumza tu”
“Niahidi unarudi na mtoto wa K2 hapa”
“Usijali, hapa ninasubiria simu ya Sara, akinijulisha tu basi nitaondoka hapa na kwenda kumchukua”
“Unamuamini huyo Sara?”
“Sina mashaka naye kabisa, ni mtu ambaye amefanya kazi zangu nyingi kubwa sana”
“Sawa kuwa makini?”
“Usijali mutakuwa munatufwatilia kila tunacho kifanya kupitia hizi tv”
“Poa”
Ester akaingia akiwa na wasichana wawili warefu kiasi, sura zao zote zinafanana ikimaanisha kwamba ni mapacha.
“Hizi ni mashine zangu, ni pacha wapo vizuri kishenzi”
“Sawa”
“Wamefanana kusema kweli, kikubwa kuweni makini nanawahitaji muwee kufanya kitu kikubwa ambacho K2 hato kisahau kwenye maisha yake.”
“Ninatambua uchungu ambao upon aye, nitakuletea unacho kihitaji.”
Simu ya Livna akaita kisha akaitoa kwenye mfuko wa suruali yake.
“Sara”
“Nimefanikiwa mkuu, tuonane wapi?”
“Nipigie imo, nahitaji kumuona huyo mtoto”
“Poa”
Livna akakata simu baada ya muda simu yake ikaita tena, akapokea na kuiweka mbele yake. Nikaitazama video hiyo na nikamuona Sara huyo, ni binti mwenye asili ya kiafrika.
“Kibonge ninaye kwenye gari”
Sara alizungumza huku akionyesha video ya mtoto wa K2 ambaye nilisha wahi kumtibu kipindi nilipo pandikiza virusi vilivyo sababisha watu kuweza kupata mapunye miilini mwao nchini Tanzania.
“Nimemuona, hakikisha kwamba unachukua boti na kukutana kwenye kisiwa tunacho kutana kila siku”
“Sawa mkuu”
“Dany ninaianza safari”
“Unatumia usafiri gani?”
“Boti, ambayo hakuna satelaiti inayo weza kuinasa zaidi ya satelaiti yetu tu”
Martin akaingia huki naye akiwa amevaa nguo za jeshi.
“Martin mlinde Livna”
“Sisi tutamlinda yeye”
Msicha mmoja kati ya hawa mapach alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.
“Sawa”   
Kila mmoja akavaa kifaa maalumu cha mawasiliano, hadi mimi nikavaa ili niweze kuzungumza nao moja kwa moja pale pale wanapokuwa mbali nasi. Livna na watu wake wakaondoka humu ofisini na kutuacha na Ester pamoja na wezake, wakaziwasha Tv hizi na tukaanza kuwaona jinsi wanavyo ianza safari hii, ambayo itawachukua muda. Tukaendelea kuwafwatilia hadi wakafika katika kisiwa walicho panga kukutana, wakasimamisha boti hiyo pembeni, na wakashuka, kisiwa hichi sio kikubwa kwa maana tuna kiona kwa juu. Galfa kisiwa mlipuko mkubwa wa bomu ukatokea katika kisiwa hichi na kutufanya watu wote tuliopo humu ndani kustuka sana na nikajikuta nikisimama, sikuona mtu yoyote zaidi ya moto mwingi unao endelea kuteketeza eneo hili la hichi kisiwa.
“LIVNA LIVNA LIVNAAAAAAAAAAAA………………..”
Niliita kwa sauti ya juu, sikuitikiwa zaidi ya kusikia kimlio kikali sana kilicho tuumiza masikio na kujikuta sote tukivua vifaa hivi vya mawasiliano masikioni mwetu huku mapigo ya moyo yakinienda mbio kwani sijui shambulizi limetokea wapi.
                                                                         
AISIIIII……….U KILL ME 181

 Ukimya ukatawala ndani ya chumba hichi huku kila mtu kiwa na wasiwasi mwingi sana.
“Hembu vuta karibu hiyo video”
Nilizungumza kwa haraka huku nikimtazama Ester usonii mwake. Kwa haraka akaanza kuisogeza karibu video ya kisiwa hichi kwani tulikuwa tuinaitazama kwa juu sana. Ikafika karibu, tukawaona wote wanne wakiwa wamelala chini, huku pacha mmoja akiwa amelala juu ya Livna. Nikajikuta nikiwa nimsehika mdomo wangu kwani hadi sasa hakuna anaye fahamu kama wapo hai japo tumewaona wamelala.
Tukaona boti mbili zikija kwa kasir karibu ya kisiwa hichi.
“Ni kina nani hao?”
“Sijafahamu mkuu”
Ester alizungumza huku akizivuta karibu sura za watu hawa. Sote tukawaona ni wazungu walio valia bukta na mashati waliyo yaacha wazi.
“Hawa ni wavuvi, ila pia niwatalii”
Ester alizungumza huku sote tukiwatazama jinsi wanavyo shuka kwenye boti zao, kisha kwa haraka wakakimbilia hadi sehemu walipo anguka Livna na wezake, wakaanza kuwageuza huku wakiwatazama.
“Wanawakagua kama wapo hai?”
“Hii ni hatari, Ester tuma vinaja wakawachukuee”
“Hatuto wawahi, kwa maana ni sehemu ya mbali sana kutoka hapa walipo, ngoja tuangalie mwisho wao utakuwa ni wapi?”
“Na mlipuko umetokea wapi?”
“Ni bomu la kutegewa ardhini, nahisi kuna mmoja wao atakuwa amelikanyaga pasipo kujua ndio likalipuka”
Wazungu hao wakawaingiza kwa haraka Livna kwenye boti yao na kuondoka kwa kasi katika eneo hilo.
“Hakikisheni kwamba hawawapotei hadi sehemu ya mwisho watakapo kwenda”
“Sawa kuna kisiwa kikubwa kama maili sita kutoka kisiwa hichi, ninaimani kwamba hapo ndipo wanapo kwenda”
“Ni lazima tukawachukue”
“Kama watafikia hapo basi ulinzi utakuwa ni wa uhakika kwa maana ni kisiwa wanacho ishi watalii pamoja na wenyeji”
“Wenyeji ni watu gani?”
“Ni Waafrika”
Tukaendelea kutazama boti zilizo wapakiza Livna na wezake jinsi zinavyo zidi kwenda kwa kasi, baada ya saa moja wakafanikwia kufika kweli kwenye kisiwa hicho kikubwa, wakawashusha Livna na wezake na kuwaingia kwenye magari na moja kwa moja wakawapeleka hadi kwenye hospitali iliyopo katika eneo hilo.
“Andaa vijana waweze kwenda”
“Sawa mkuu, ngoja nikawatangazie”
Ester akatoka chumbani humu na kuniacha na Logate.
“Logate tazama Sara yupo wapi, ninahitaji kwenda mimi mwenyewe kumchukua mtoto wa K2”
“Kwenda wewe mwenyewe?”
“Ndio, ninahitaji kwenda mimi mwenywe?”
“Hapana ni bora kuagiza watu waende kumchukua ila si wewe kwa maana ukiondoka wewe tunakosa kiongozi ikiwa kiongozi wetu mkubwa ndio kama hivyo yupo hospitalini”
“Kipindi sijafika nani alikuwa kiongozi?”
“Ester”
“Basi atachukua madaraka na mamlaka niliyo nayo, sawa”
Nilizungumza kwa msisitizo hadi Logate akatingisha kichwa akikubaliana na kile nilicho muagiza. Ester akaingia na kusimama mbele yangu.
“Tayari nimesha andaa vijana watano watakao kwenda kwenye hicho kisiwa na nimesha wapo maelezo ya kutosha, pia wasicha wote nimwafahamisha kwamba kiongozi wetu yupo kwenye hatari.”
“Vizuri na mimi niandalie boti ninahitaji kwenda kuonana na Sara, ninahitaji kumchukua mtoto wa K2 na kurudi naye hapa”
“Unataka kwenda kuonana na Sara!!!?”
“Ndio”
“Hapana Dany, hicho kitu siwezi kukiruhusu kabisa. Dunia nzima unatafutwa, satelaiti zaidi ya maelfu zinakutafuta wewe, unahisi kwamba inaweza kuwa ni rahisi wewe kupiga hatua hata ya kutoka usawa wa hii meli. Huwezi, tulia humu ndani hilo swala la kumpokea mtoto wa K2 nitawapa kazi watu wengine sawa”
Ester alizungumza kwa msisitizo huku akiwa amenyang’ata meno yake, ikiasihiria kwamba kile anacho kizungumza amekidhamiria kutoka moyoni mwake.
“Nitaendelea kuishi humu ndani hadi lini?”
“Ishu si kuishi humu ndani, hii ndio sehemu ya wewe kuwa salama, nimepokea jukumu la kuhakikisha kwamba unakuwa salama, basi ni lazima uwe salama siwezi kuenenda kinyume na kakuli ya mkuu wangu Livna, sawa”
Ester aliendelea kuzungumza kwa jazba huku akiwa amenisogelea karibu yangu akionekana kuto kuniogopa kabisa.
“Logate, mtafute Sara, kisha mtumie Carin hiyo picha ya wapi alipo Sara na mtumie namba za mawasiliano kwa maana nimesha muweka tayari kwa hilo”
“Nimesha mpata Sara anakaribia kufika kisiwani hivi sasa”
“Nitumie namba yake nimpigie imo”
“Sawa mkuu”
Logate akafanya alicho agizwa, Ester akatoa simu yake mfukoni baada ya meseji kuweza kuingia. Akampigia Sara, huku akivaa earphone sikioni mwake.
“Habari yako dada Sara”
“Ninaitwa Ester ni msaidizi wa Livna”
“Nashukuru kama unanifahamu, nina imani unampigia Livna na umeshindwa kupata mawasiliano naye?”
“Basi amepata tatizo katika hicho kisiwa kuna mabomu kadha ambayo yalitegwa kwa kipindi kirefu sana cha nyuma, mmoja ya watu alio ongozana na Livna ameweza kukanyaga bomu hilo na kulipuka, ninamuagiza kijana mwengine kuweza kuja kumchukua huyo kijana”
“Yeye kwa sasa amechukuliwa na wavuvi ambao ni watu salama, na yupo katika kisiwa cha Bama, na kwa sasa wapo hospitalini”
“Basi utakutana na vijana wengine huko”
“Shukrani”
Ester akakata simu yake aliyo ipiga kwa mfumo wa video, akanitazama usoni mwake.
“Pasipo kukuvunjia heshima, ninakuomba tuendelee kushirikiana kuhakikisha kwamba mkuu na wengine wanakuwa salama katika sehemu walipo”
Ester alizungumza kwa sauti ya upole, sikuwa na jambo la kuzungumza zaidi ya kukubaliana naye. Nikaka kwenye kiti nilichokuwa nimekalia huku nikiwa nia wasiwasi mwingi sana.
“Hakuna aliye kanyaga bomu”
Logate alizungumza huku akianza kurudisha vidoe ya muda mchache ulio pita.
“Kuna mnyama huyu nguruwe pori, alikanyaga bomu na kulipuka na mlipuko huo  wa galfa ndio ulio pelekea mkuu na wezake kupoteza fahamu”
Logate alizungumza huku akituonyesha nguruwe aliye lipuliwa upande wa pili wa hichi kisiwa, japo sio mbali sana kutoka sehemu na walipokuwa Livna na wezake.
“Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa, mkuu kuwa salama”
Logate aliendelea kusisitiza na kidogo akafufua matumini na furaha kwa mbali ndani ua moyo wangu.
“Sara naye amebadilisha mawazo anaelekea walipo Livna nina imani kwamba yeye ndio atawai kufika kuliko kina Carini”
“Si wemesha anza safari?”
“Ndio wamesha anza”
“Watafika hapo baada ya muda gani?”
“Kama saa moja na nusu”
“Poa ninikuja”
Nilizungumza huku nikinyanyuka katika kiti nilicho kalia, nikatoka ndani humu na kuwaacha Ester na Logate wakinitazama. Moja kwa moja nikaelekea katika chumba alipo Babyanka na Hawa, nikawakuta wakizungumza huku wakicheka sana.
“Mbona unaingia bila kubisha hodi jamani ungetukuta tupo uchi ingekuwaje?”
Babyanka alizungumza kwa utani.
“Kwani kuna ubaya kuwakuta mupo uchi?”
“Mmmmm”
Hawa akaguna, nikaka pembeni yake huku nimshika shika tumbo lake.
“Mtoto tumtarajie lini?”
“Mmmm bado. Babyanka amenisimulia kwamba kuna ndege za Marekani umezilipua?”
“Ndio”
“Unajisikia raha kuua eheee?”
“Utasikia raha na wewe nikiuliwa eheeee?”
Nilizungumza kwa sauti ya ukali huku nikimtazama Hawa usoni mwake.
“Lengo langu si kukukasirisha baba yangu”
“Kwenye swala la uongozi sinto hitaji kuona mtu yoyote ananishauri kitu ambacho atahisi kwamba kipo kinyime nami sawa?””
“Sawa baba nisamehe kwa maana mimi mwenyewe ninasubiria kifo changu baada ya kujifungua huyu mtoto”
Hawa alizungumza kwa sauti ya upole, kwa jinsi walivyo nichefua kwa maneno yao nikatoka chumbani humu na kupanda juu  kabisa ya hii meli kubwa sana. Huku napo kuna wasichana wanao fanya mazozi, pia kuna kiwacha cha helicopter ambacho kinaweza kupoteka helicopter zaidi ya tano kwani ni kikubwa sana.
“Shikamoo”
Msichana mmoja alinisalimia nikamgeukia na kumtazama usoni mwake.
“Marahaba”
“Naomba nijipime na wewe”
“Ujipime?”
“Ndio mazoezi”
“Una umri gani?”
“Miaka ishirini na mbili”
“Tutapambana kesho sawa”
“Sawa kaka Dany”
“Nenda kaendelee na mazoezi”
Msichana huyu akaondoka na kuniacha nikimuangalia makalio yake yaliyo banwa vizuri na suruali iliyo mbana sana. Sikuhitaji kuendelea kumfwatilia msichana huyu kwani sihitaji kumjengea matamanio ya kimapenzi. Nikaitazama mikono yangu hii miwili, nikajikuta machozi yakinilenga lenga kwani ni mikono ambayo imejaa damu za watu wengi sana ambao wengine nimewaua wakiwa na hatia huku wengine nikiwa nimewaua wakiwa hawana hatia kabisa.
‘Mungu wangu ninakuomba unisamehe’
Nilizungumza huku machozi yakinilenga lenga kwani sidhani hata siku ikitokea nimefariki, ninaweza kuridhi ufalme wa mbinguni kama vile tunavyo amini katika imani zetu za kidini.
“Dany Dany”
Niliisikia sauti ya Logate akiniita, nikageuka nyuma yangu na kumtazama.
“Kuna kitu unatakiwa kukiona huku”
Logate alizungumza huku akiwa na wasiwasi mwingi, kwa haraka tukaanza kukimbia kuelekea katika chumba cha mawasiliano. Tukafanikiwa kufika kwa haraka, tukafungua mlango na kumkuta Ester akiwa amesimama mbele ya Tv huku akitazama mapambo kwenye kisiwa ambacho Livna na wezake wamepelekwa na watalii.
“Wamarekani wametuma jeshi na wanaendelea kushambulia katika hospitali”
“Wanapambana na nani?”
“Wanapambana na Sara, yupo peke yake na amefanikiwa kufika eneo hilo”
“Ulio  waagiza bado hawajafika?”
“Bado hawajafika, ila wamebakisha dakika kama kumi na tano kuweza kufika”
Tukamuona jinsi Sara anavyo endelea kushambuliana na wanajeshi wa Marekani walio fika katika hospitali hiyo. Kusema kweli Sara ana uwezo mkubwa wa kuttumia mwili wake katika kufanya mashambulizi ya silaha na hata mapigano ya kawaida.
“Unaweza kumpigia?”
“Hapana siwezi kumpigia na wala hawezi kupokea simu kwani simu yake alisha iangusha mbali na hapo hospitalini”
“Mtoto bado anaye?”
“Ndio anaye?”
Nikashusha pumzi nyingi huku nikimtazama dada wa watu jinsi anavyo pambana.
“Ohoo Mungu wangu”
Logate alizungumza mara baada sisi sote kuona malori mawili yalio jaa wanajeshi yakisimama nje ya hospitali hiyo. Wanajeshi wakaanza kushuka kwa kasi huku kila mmoja akiwa na silaha yake.
“Waelezee wezako ulio  watuma juu ya hili linalo endelea”
“Nmesha wasiliana nao na wanazidi kuongeza mwendo kasi boti yao kuweza kufika kisiwani hapo”
“Hatuwezi kufanya mashambulizi yoyote ya kuweza kuwazuia hawa wanajeshi kuingia ndani ya hii hospitali?”
“Hapana na tukisema tufanye mashambilizi ya juu, tujue tunaharibu eneo  zima na tutawapoteza watu wetu muhimu”
“Wamefika”
Logate alizungumza huku akituonyesha wasichana walio agizwa na Ester wakisimamisha boti yao kisiwani, wote wakashuka na kukimbilia kwenye moja ya gari lililopo barabarani, wakaondoka kwa kasi walipo fika eneo la tukio, wala hawakuuliza maswali, wakanaza kushambulia.
“Carin hakikisheni mkuu anakuwa salama”
Ester alizungumza huku akiwa ameishika vizuri earphone aliyo ivaa sikioni mwake.
“Muweke loudspeaker”
Ester akafanya hivyo, akaminya moja ya simu za mezani na tukaanza kusikia milio ya risasi jinsi inavyo endelea kurindima katika eneo hilo. Wanajeshi wa Marekani wakazidi kuongezeka jambo ambalo ni hatari sana kwa vijana Livna.
“Mkuu tumezidiwa tunaomba msaada, narudia tena tumezidiwa tunaomba msaada”
Tuliisikia sauti ya Carin alizungumza jambo lililo tufanya sote kutazamana, kwani hata tukituma wasichana wengine ili kuweza kufika eneo hilo watachukua muda mrefu njiani na wanaweza kukuta kila kitu kimekwisha, jambo ambalo ni hatari sana kwetu.
 
 ITAENDELEA
‘Haya Wamarekani wameamua kuhakikisha kwamba wanamkamata Livna na kumuokoa mtoto wa K2 hali inazidi kuwa tete kwa wale walipo eneo la tukio je nini kitakacho endelea? Usikose sehemu inayo fwata ya hadithi hii ya kusisimua kutoka kwa muandishi mahiri Eddazaria G.Msulwa”


from MPEKUZI

Comments