Waitara: Watumishi Wa Umma Msijiingize Kwenye Utumwa Wa Mikopo Ya Taasisi Zisizo Halali

Na Tiganya Vincent
Watumishi wa Umma wametakiwa kuacha kujiingiza katika mikopo inayowasababisha kuuza uhuru wao na kuwa watumwa kwa wakopeshaji wasio halali na ambao hawajasaliwa na Serikali.

Kauli hiyo imetolewa wilayani Nzega na Igunga na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR TAMISEMI) Mwita Waitara wakati wa vikao vya majumuisho na Watumishi wa Wilaya hizo.

Alisema baadhi ya wanawakopesha hawakusajiliwa na hawalipi kodi za Serikali na hivyo kuendesha biashara hiyo kinyume cha Sheria na taratibu za nchi.

Waitara alisema wakopeshaji hao wamekuwa wakikopesha kwa riba kubwa ambazo zimewafanya baadhi ya watumishi kuishi maisha magumu yaliyojaa utumwa ndani yake.

Alisema baadhi ya watumishi ambao ukopa wamekuwa wakikabidhi hata Kadi za kuchukua Fedha (ATM) kwa wakopeshaji na inapofika mwisho mwa Mwezi ndio upiga simu kwake ili waende kwenye ATM achukue fedha kwa ajili ya kulipa deni na kidogo za matumizi na baada ya hapo anarudisha kadi mdai wake.

Waitara alisema kitendo kinafanya taarifa za mshahara wa mtumishi kutokuwa siri kwake bali kuwa wazi hata kwa mkopeshaji jambo ambalo ni kuuza uhuru wake.

Aliwataka Watumishi wa umma kuishi kulinga na mishahara wanayolipwa na kujiepusha na tamaa ambazo zinaweza kuwasababisha kujiingiza katika matatizo.


from MPEKUZI

Comments