Uvumilivu Wamshinda Vanessa Mdee.....Aamua Kuwachana TraceMziki

Msanii wa Bongo fleva Vanessa Mdee ameonekana kukasirishwa na kile ambacho kinafanywa na kipindi cha Televisheni cha TraceMziki kucheza baadhi ya ngoma na kuacha nyingine huku ikitafsiriwa kuwa ni upendeleo unafanyika kwa baadhi ya wasanii.

Msanii huyo kupitia ukurasa wake wa Twitter amefunguka na kusema kwamba ” Wacha niseme tu, TraceMziki imekuwa station fulani ya upendeleo kwa wasanii kadhaa kwa muda mrefu sana.kuna ule upendeleo wa kuficha alafu kuna ile live bila chenga”



from MPEKUZI

Comments