Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 43

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA  
 
“Nashukuru kwa kuendelea kumlinda mwanangu, ila ninakuomba huko Tanzania munapo kwenda uhakikishe kwamba anakuwa salama”
“Nashukuru baba, ila nina imani kwamba unaelewa ni jambo gani ambalo linaendelea?”
“Ndio kuna kijana amenifwata kama masaa manne yaliyo pita na amenieleza kwa kila kila kile kinacho endelea kwa sasa”
“Sawa baba, nashukuru kwa kulifahamu, ila ninacho kuomba kuanzia hivi sasa jilinde, nahitaji uingie ikulu. Ukiingia ikuli tutakuwa tayari kurudi nchini Ujerumani”
“Sawa nitahakikisha kwamba ninaichukua nchi na maadui zangu wote watakwenda kulipa kwa hili jambo ambalo wamelifanya.”
“Sawa sawa”
“Ila kuna kitu kimoja ninaomba unisaidie baba mke”
“Kitu gani hicho mwanangu?”

ENDELEA       
“Nakuomba unahakikishie kwamba utashinda uchaguzi mkuu”
Nikasikia mihemo ya kushusha pumzi ya baba Camila, huku ukimya wa sekunde kadhaa ukiwa umetawala.
“Nitashinda japo kuna changamoto nyingi sana mwanangu”
“Ninakuombea baba yangu”
“Sawa, niwatakie safari njema na mukifika nchini Tanzania ninaomba muweze kunifahamisha”
“Sawa baba”
Nikamrudishia Camila simu na akaendelea kuzungumza na baba yake. Safari hii ikatugarimu siku moja ambayo ni zaidi ya msaa ishirini na nne. Tukafika nchini Tanzania majira ya saa sita mchana, kwa bahati nzuri tukamkuta mwenyeji wetu akitusubiria eneo ambayo ndege imetua. 
 
“Karibuni sana Tanzania”
Dada huyu ambaye anaitwa Jojo kama vile tulivyo soma maelezo yake, alizungumza huku akionekana kuwa na furaha kubwa sana.
“Tunashukuru”
Tukapeana mikono kisha tukaanza kuelekea kwenye maegesho ya magari. Baadhi ya watu walijitahidi kunikazia macho nikiamini kwamba watakuwa wanajiuliza maswali mengi sana ya kunifananisha mimi na Ethan wanaye muona kwenye vyombo vya habari au kwenye mitandao ya kijamii. Tukaingia kwenye gari ya Chervolet Captival Extrem na kuondoka katika uwanja huu wa ndege.
 
Kumbukumbu zangu kuhusiana na safari yangu ya kwanza kundoka nchini Tanzania, ikaanza kurejea kichwani mwangu taratibu. Nikaanza kutazama majengo ya karibu na huu uwanja wa ndege ambao kwa namna moja ama nyingine yameongezeka, kwani kipindi nilipo kuwa ninaondoka nchini Tanzania hayakuwa kama hivi.
“Mbona unashangaa sana Ethan?”
Jojo Dany aliniuliza huku akinitazama.
“Ninakumbuka mambo mengi sana”
 
“Mambo gani hayo?”
“Siku nilipo kuwa ninaondoka nchini Tanzania, hapakuwa na majengo kama haya”
“Ohoo, ni kweli, nchi imezidi kubadilika hususani hapa jijini Dar es Salaam”
“Ila nilicho kipende kwenye nchi hii ni joto jamani.”
Camila alizungumza na kutufanya tushangae kidogo.
“Joto”
“Ndio. Ujerumani hali ya baridi kwa kipindi chote cha mwaka, inakera kwa kweli. Tumekuwa ni watu wa kuva amakoti tu”
“Haahaa, basi huko tunapo elekea kuna baridi kiasi”
“Ila si kama ya Ujerumani?”
“Hapana huko ni ya kawaida sana, nina imani mutauipenda”
“Sawa”
 
Jojo akazidi kuendesha gari hili, tukafika kwenye moja ya motel ndogo na tukapata chakula cha mchana kisha tukaendelea na safari yetu. Hadi majira ya saa kumi na mbili jioni, tukaanza kukatiza kwenye msitu mmoja mkubwa ambao kidogo ukaanza kutupa mashaka.
“Musiogope, huku ni sehemu salama ambayo munaweza kuishi kwa amani  kwa kipindi chote”
“Mbona ni msituni sana dada Jojo?”
“Nyumba salama siku zote ni lazima ziwe katika maeneo kama haya. Hamuwezi kukaa mjini, kumbukeni kwamba hamumjui adui yenu atawavamia kwa namna gani”
 
Maneno ya dada Jojo kidogo yakatufariji na kupunguza wasiwasi mwingi tulio nao. Majira ya saa mbili usiku tukafika kwenye moja ya nyumba kubwa ambayo taa zake za nje hazina mwanga mkali sana. Jojo akaanza kushuka kwenye gari kisha nasi tukafwata huku nikiwa nimeshika Camila mkono. Tukamkuta mwanaume mmoja mrefu kiasi huku mwili wake ukiwa umejengeka kwa mazoezi.
“Karibuni sana”
Mwanaume huyu alizungumza huku akitusalimia kwa kunyoosha mkono wake wa kulia. Nikawa wa kwanza kuupokea mkono wake huo ambao hakika ni mgumu kiasi. Akasalimiana na Camila kisha tukakaribishwa ndani katika nyumba hii. Tukamkuta kijana mmoja akiwa ameketi sebleni huku uso wake ukiwa na majeraha kiasi.
 
“Karibuni sana. Huyu ni baba yangu anaitwa Dany. Huyu ni mdogo wangu anaitwa Randy”
“Tunashukuru kuwafahamu”
“Baba, Randy, hawa ni Ethan na Camila tutakuwa nao hapa kwa kipindi cha mwezi mmoja hivi”
“Karibuni sana. Ethan mimi ni mfwatiliaji wa mpira wako”
“Nashukuru sana Dany”
Tukakaribishwa mezani na tukapata chakila cha usiku huku kijana huyu mara kwa mara macho yake yananitazama jambo ambalo kidogo nikatamani kumuuliza ni kwa nini ananitazama sana ila nikashindwa kutoka na watu waliomo hapa sebleni.
 
“Ethan una mke mzuri sana, hakikisha kwamba una mlinda”
“Nashukuru sana”
“Ila kuna jambo moja nahitaji kuanzia kesho mujumuike nasi?”
“Jambo gani?”
“Nilazima muweze kujilinda wenyewe, musitegemee sana ulinzi wa watu ambao wamefundishwa vyuoni na mwisho munawapoteza bure”
Maneno ya Dany kidogo yakatufanya tutazamane na Camila usoni mwetu.
“Musiogope, ni mazoezi ya kawaida sana. Najua Camila baba yako atashinda kiti cha uraisi na wewe ulinzi utaongezewa, sasa inabidi ujipange vizuri”
 
“Sawa Dany nitashukuru”
Tukamaliza kupata chakula hichi cha usiku kisha Jojo akatupelekea kwenye chumba chetu ambacho tutalala kwa siku zote tutakazo kuwepo hapa.
“Vipi umeridhika kwa hayo mazoezi?”
Nilizugumza huku nikimtazama Camila usoni mwake.
“Mimi nipi tayari, kwa hizi ngija ngija tunazo kutana nazo hakika sina hata hamu kwa kweli. Laiti kama tungekuwa vizuri kwenye swala zima la kupamba, wala tusinge kuwepo hapa sasa hivi”
Camila lizungumza huku akinishika kiunoni mwangu, tukatazamana kwa sekunde kadhaa, kisha mkono wangu wa kulia nikaanza kuushusha hadi kwenye yake na nikaanza kuyaminya minya taratibu.
“Ethan mume wangu nimechoka”
Camila alizungumza huku akijitoa mikononi mwangu. Akaanza kuvua nguo zake,akaingai bafuni. Nikakichuguza chumba hichi kwa umakini, nilipo hakikisha kwamba kuna usalama wa kutosha, nami nikavua nguo na kuingia bafuni. Tukaoga kwa pamoja na kurudi kitandani na kulaa.
 
    Saa kumi na mbili alafajiri mlango wetu ukagongwa, tukaisikia  sauti ya Jojo akituhamsisha tuamke na tuanze mazoezi. Nikawa wa kwanza kuamka kitandani na kuvaa boksa yangu. Nikatembea hadi mlangoni nikafungua na kumkuta dada Jojo akiwa ameshika nguo za mazoezi. Akanikabidhi nguo hizi kisha akaelekea kwenye chumba kingine na kugonga.
“Ohoo Mungu wangu”
Nilizungumza huku nikiwa ninapiga miyayo mingi sana. Nikajitupa kitandani ambapo Camila bado amelala. Kabla hata usingizi huu wa asubuhi haujanipitia, nikasikia mlango ukigongwa kwa nguvu na kutufanya wote tukurupuke kitadani.
“Muna dakika moja ya kutoka nje”
Tuliisikia sauti nzito ya Dany na kunifanya nianze kuzichambua hizi nguo za mazoezi.
 
“Jamani haya ni mateso sasa”
Camila alizungumza huku akipiga miyayo mingi  sana.
“Tungekataa jana haya wala yasinge tukuta”
“Kwani mimi nilijua mambo yenyewe yanaweza kuwa hivi jamani?”
“Ndio hivyo mke wangu, tukafanye tu. Tukiona mambo magumu leo, tunaomba tuache tu kwani lazima”
“Mmmmm kumbuka tupo ugenini na huku hayupo Ethan wala mtu ambaye atatusaidia hata tukiwa na shida”
“Haaah! Tutajua mbele ya safari bwana”
Nilizungumza huku nikianza kuvaa nguo taratibu, Camila naye akavaa nguo zake.
“Sasa tunakwenda kufanya mazoezi peku?”
“Sijui mimi”
Camila alinijibu huku akiw aamenuna kutokana na uchovu huu wa asubuhi. Tukatoka chumbani hapa na kuanza kutembea kwenye kordo hii ndefu. Tukashuka ngazi na kuwakuta Dany, Camila na Randy sebleni.
 
“Viatu jamani”
Nilizungumza huk nikiwatazama. Dany kwa ishara akatuonyesha kwa ishara miguu yake ambayo haina hata soksi, akafungua mlango wa sebleni na tukaanza kutoka.
“Tunakimbia hivi jamani?”
Niliuliza huku nikimuona Dany akianza kukimbia kwenye barabara hii ndefu tuliyo jia. Hakuna ambaye alinijibu zaidi ya watu wote kuanza kufwata nyuma. Camila naye hakunijibu zaidi ya kunitazama tu, tukaanza kukimbia kwenye mchanga huu ambao umejaa vijiwe jiwe vidogo ambavyo mara kwa mara mimi na Camila vilituchoma na ilitulazimu kutulia kidogo ili kutoa vijiwe hivyo.
 
“Oohoo jamani tutakufa”
Nililalama huku nikiandelea kuwafwata nyuma kwa kukimbia.
“Jikaze bwana mume wangu, je ungeenda jeshi ingekuwaje?”
“Bora ujue upo jeshi mke wangu kuliko huku”
“Acha hizo una kera bwana, kumbuka wewe ni mchazaji mzuri wa mpira”
“Kuna tofauti ya uchezaji na mazoezi haya”
“Sitaki bwana kusikia maneno yako”
Camila alizungumza kwa ukali huku akionekana dhairi kwamba ana jikaza. 
 
“Msitu huu una wanyawa wote wakali, hakikisheni kwamba tunapo kimbia munakuwa karibu nasi, tunaingia msituni sasa”
Dany alizungumza huku akiwa amepunguza kasi ya kikimbia na kuwa sambamba nasi tunao jikongoja
“Wa….wany….a..nyama waka…li!!?”
Niliulliza kwa wasiwasi mwingi sana huku macho yakiwa yamenitoka.
“Tazama kule”
Dany alizungumza huku akinyoosha mkono  wake wa kulia, nikahisi kama roho inanitoka kwani kwenye moja ya mti kuna joka moja kubwa sana ambalo toka kuzaliwa kwangu leo hii ndio nimeweza kuliona. Woga ukanifanya niongeze mwendo wa kukimbia na kuwa sawa na Jojo huku Camila na Dany wakitufwata kwa nyuma na Randy yupo hatua chache pembeni yetu.
“Vipi unaogopa?”
“Sana”
“Usiogoepe, hakuna mnyama anaye weza kuwashambulia mukiwa nasi. Huwa tumewafundisha mbinu ya kutusikiliza na kutii kile ambacho tunakihitaji wakifwate.”
 
“Kivipi?”
“Ulisha wahi kumuona mbwa?”
“Ndio”
“Mbwa ukimfundisha baadhi ya vitu huwa ana kisikiliza kama ni bwana wake unaye muongoza, ni sawa sawa na hawa wanyama”
Mapigo ya moyo yakazidi kutuenda kasi sana mara baara ya kuonda kundi la Simba kama watano wakiwa wamelala mbele katika barabara tunayo ipita. Jojo akawafukuza Simba hawa kwa ishara na wakatupisha na kuendelea na mazoezi yetu.
Hadi tunamaliza mazoezi haya ya kukimbia, hakika kama sijafa leo kwa woga basi sinto kufa maisha yangu yote kwa woga, labda kifo changu kisababishwe na jambo jengine, kwani leo nimeona wanyama wakila aina na wengine wanatisha ila hapakuwa na mnyama hata mmoja ambaye ametudhuru.
 
“Hahahaa haki ya Mungu napenda sana kuishi huku”
Maneno ya Camila aliyo yazungumza huku akiwa amesimama pembeni yangu, yakanifanya nimgeukie huku nikiwa nimejawa na mshangao mkubwa sana.
“Nini?”
“Napenda kuishi huku, yaani Ujerumani hakuna wanyama kama hawa nilio waona leo”
“Hivi hujui kama wale wanyama wanaua, wakikung’ata eheee?”
“Najua, ila nitahakikisha kabla ya kuondoka nimesha jifunza jinsi ya kuishi  nao. Haki ya Mungu ninapenda wanayama mimi jamani ohoo”
Nikajikuta nikiondoka eneo alilo simama Camila na kumfanya acheke sana.
 
“Mbona mpenzi wako anakucheka sana”
Jojo aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.
“Ahaa ni mambo yake ya wanyama wanyama. Ananikera sana sipendi kabisa wanyama”
“Kwa nini uwapendi, ikiwa wao ndio walinzi wetu hapa msituni. Hakuna binadamu mwenye nia mbaya ambaye anaweza kukatiza hapa”
“Mmmm mimi sijaumbwa kwa kweli kuwapenda hao wanyama”
“Hahaa usijali kila jambo litakuwa sawa”
Tukaingia katika awamu ya pili ya mazoezi ya taikondo. Mazoezi haya hakika ni magumu kuliko hata kukimbia katika msitu wa eneo hili. Zaidi ya masaa mawili saa Jojo na Danya wakawa wanatufundisha mazoezi haya ambayo hakika hadi tunamaliza wote watatu viungo vyetu vimeorojeka kwa kuchoka na kuapa majera kadhaa yaliyo tokana na kukosa umakini.
 
“Camila”
Nilimuita Camila huku tukiwa ndani ya chumba chetu, kwa maumivu niliyo nayo nikajikuta hata nikishindwa kulala kitandani.
“Mmmmm”
“Mimi nahitaji kutoroka, siwezi kuendelea kukaa hapa”
“Mmmm…….”
“Ndio nahitaji kutoroka, maisha gani haya ya mateso naomba ujumuike nami mke wangu na tutoroke wote”
“Umewasahaua wale Simba na wanayama wengine humu msituni ehee?”

ITAENDELEA KESHO


from MPEKUZI

Comments