Raia wa Ethiopia Ahukumiwa Kifungo cha Maisha Jela na Mahakama ya Mafisadi Baaada ya Kunaswa na Madawa ya Kulevya

Mahakama Kuu Kitengo cha Uhujumu Uchumi ‘Mahakama ya Mafisadi’ imemuhukumu kifungo cha maisha jela raia wa Ethiopia, Ana Moises Chissano baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya Cocaine Kg 3.03.

Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Lilian Mashaka ambapo amesema mshtakiwa huyo amefungwa chini  ya kifungu cha sheria cha 15(1)(b) cha sheria namba 5 ya 2015 cha sheria ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya.

Mahakama imeamuru dawa hizo ziteketezwe.


from MPEKUZI

Comments