Alikiba atangaza kuachia nyimbo mbili siku ya funga mwaka na King Kiba

Msanii wa muziki wa kizazi Ally Salehe Kiba a.k.a Alikiba ameweka wazi kuwa December 19 mwaka huu ataachia nyimbo zake mbili.

Hiyo ni katika show yake kubwa ya kufunga mwaka, huku show yake na muimbaji maarufu Afrika,  Yvonne Chaka Chaka kutokea Afrika Kusini ikihairishwa hadi February 2019. 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

"Kuelekea kwenye show yangu kubwa ya mwaka 'Funga Mwaka Na King Kiba' December 19, 2018 pale Next Door Arena, nitaachia “HITS” zangu mbili kabla mwaka haujaisha pamoja na kuizindua rasmi kinywaji changu cha Mofaya Energy Drink.

"Sema kuna mabadiliko ya tarehe ya show yangu na Mama Yvonne Chaka Chaka pamoja na King Of Best Melodies, Christian Bella christian  kutoka December to February 2019, the month of Love ❤"

Kwa sasa Alikiba anafanya vizuri na wimbo unaokwenda kwa jina la Mwambie Sina alioshirikiana na kundi lake la Kings Music ambalo pia kwa sasa linafanya vizuri na wimbo uitwao, Toto.


from MPEKUZI

Comments