Ajali ya Basi Yaua Watu 2 na Kujeruhi 21 Lushoto

Watu wawili wamefariki dunia na wengine 21 kujeruhiwa huku sita kati yao wakiwa na hali mbaya baada ya basi la Royal Classic waliokuwa wakisafiria, kuacha njia na kupinduka eneo la Kibaoni wilayani Lushoto jana Jumanne Desemba 11.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda waPolisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe, amesema basi hilo lilikua likisafiri kutoka Tanga kwenda wilayani Lushoto.

Kamanda Bukombe amebainisha chanzo cha ajali hiyo ni utelezi uliotokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika eneo hilo.

“Majeruhi sita kati ya 21 hali zao ni mbaya na wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Bombo kwa matibabu zaidi,” amesema.


from MPEKUZI

Comments