AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 174 na 175 )


MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA 
  
Msichana huyu akamkabidhi Livna simu, akatazama kitu kinacho onyeshwa, nikamuona sura yake ikijaa makunyanzi baadhi yatokanayo na hasira, taratibu nikamsogela na kutazamaa anacho kitazama, nikaona wasichana wawili wakiwa wamefungwa gundi maalumu midomoni mwao huku wakiwa katika ulinzi mkali wa kikosi cha F.B.I kutoka nchini Marekani.
“K2 amewauza walinzi wangu nilio muachia kwa Wamarekanai, wakifa basi na yeye amekufaa poamoja na hao Wamarekani”
Livna alizungumza kwa msisitizo huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake akionekana kujawa na hasira kali dhini ya hili jambo lililo tokea kwa wasichana wake ambao hata mmoja akifarikia basi ni kosa kubwa sana kwa yule aliye msababishia mauti msichana huyo kwani naye ni lazima atakufa
   
ENDELEA
Video hii ikaendelea kuonyesha jinsi wasichana hawa jinsi wanavyo patiwa mateso. Livna akamkabidi msichana huyu simu na kuanza kutoka humu ndani huku akiwa katika kwendo wa haraka. Nami nikaanza kumfwata kwa nyuma huku tukiwa tumeongozana na msichana huyu.
“Hiyo video imetumwa saa ngapi?”
“Tumeweza kuipata kwa siri katika mtandao wa FBI na hivi sasa, wezetu wanahojiwa ili kuweza kutoa siri”
Msicha huyu alinijibu huku tukipandisha ngazi kwa mwendo wa haraka kama anao kwenda nao Livna aliye jawa na hasira.
 
“Wapo wapi?”   
“Hatujafahamu ni sehemu gani husika ambayo wanafanyiwa mahojiano ila tutafahamu katika muda mfupi kwani wengine wanendelea kutafuta ni sehemu gani mahojiano hayo yanafanywa. Livna akaufungua moja ya mlango na sote tukaingi, kwa haraka akaa kwenye kiti cha kuzunguka. Akanyanyua mkonga wa simu na kuanza kuminya minya namba. Sote tukakaa kimya huku tukimtazama usoni mwake.
“Wasichana wangu wamakamatwa vipi na FBI?”
Livna alizungumza kwa sauti ya ukali iliyo jaa mikwaruzo ya mtu anaye elekea katika hali ya kulia. Nikaitazama simu hii ya mezani, nikaminya moja ya batani ili kuweza kusikia ni kitu gani atakacho jibiwa.
“Wewe na wezako imejulikana mumejumuika katika kumteka raisi Donald Bush sasa unahisi hapo mimi nitafanya nini?”
“Kwa nini usinijulishe na kama kutekwa je kuna ushahidi, kwa maana nyinyi munamuhisi Dany kwamba ndio muhusika wa kumteka raisi si ndio”
 
“Mkuu”
Msicha huyu alizungumza na kutufanya tumtazame, akamkabidhi simu Livna, akaitazama nikaona machozi jinsi yanavyo mwagika usoni mwake, taratibu nikaichukua simu hii, sikuamini macho yangu kuona wasichana hawa jinsi wanavyo nyongwa kikatili sana jambo lililo anza kunikasirisha na kunihuzunisha kwani muhusika wa tukio hilo ni mimi na ninapelekea wasichana wadogo sana hawa kufariki dunia.
“Wasichana wangu wamenyongwa K2 yote ni kwa ajili yako. Sasa ninakuambia hapa huna chako na endapo utadhubutu kunyanyua mkono wako juu yangu. Unanijua, nitakuchangua wewe na familia yako na uwaambie hao Wamarekani wako wajiandae wamegusa pabaya”
Livna alizungumza huku midomo ikimtetemeka kwa hasira kali iliyo mtawala.
 
“Hahaaaa, Livna leo hii wewe ndio wa kunipiga mikwara mimi, umenisahau eheeee?”
“K2 hii ni vita kati yetu umeianzisha na wewe ndio muhusika katika hili sasa vifo vya hao mabinti, vitalipwa na damu yako tena na mwanao wa kumzaaa”
“Thubutuuuuu ole wako umgusee, nitakuja kukusambaratisha katika hiyo meli yako na kukuaa wewe na hivyo vimende vyako na mutakuwa chakula vya papa baharini”
“Ninakusubiri na angalia kitakacho tokea sasa kwako”
Kwa nguvu Livna akauweka mkonga wa simu kwenye meza huku akihema kwa hasira akajifuta machozi yanayo tiririka usoni mwake. 
 
“Samahani ninaomba utupishe”
Nilimuambia msichana huyu, akamtazama Livna kwa sekunde kadhaa kwa ishara ya macho Livna akamruhusu kutoka ndani humu na nikabaki mimi na Livna.
“Dany wewe umeshindwa kumuua K2 mimi nilaizma nimuue sawa”
“Hilo halina tabu, mimi na wewe mpango wetu ni mmoja, nikumuua mimi, ukimuua wewe yote ni sawa”
“Nitarudi Tanzania leo kuhakiksha ninakata kichwa chake?”
“Hapana usirudi kwa sasa, umemsikia nahitaji kufanya shambulizi hapa kwenye hii meli, hawa wasichana watakufa na wewe ndio kiongozi wao. Hembu basi baki nao kuhakikisha kwamba unajiandaa kwa chochote kitakacho jitokeza hivi karibuni”
“Dany hivi unajua kwamba K2 amevuka mipaka, amavuka mipaka kabisa. Anajua thamani ya wale wasicha, wale watoto tangu wapo wadogo ninawalea leo hii wana miaka ishirini wanachinjwa hembu fikiria fikiria Dany?”
 
“Ni kweli, ila nina wazo”
“Wazo gani?”
“Video hii ninahitaji kuiachia hadharani”
“Baada ya hapo?”
“Tunaachia video ya mimi kumchinja raisi wao, nina imani kwamba italeta mgawanyiko duniani, zipo nchi zitakazo ungana na Marekani na zipo nchi zitakazo ungana nasi, kupitia wao basi dunia itakwenda kuvurugika”
“Dany”
“Naam”
“Hilo wazo ni zuri, ila utakwenda kuingiza dunia katika vita ya tatu ta Dunia”
“Acha ziingie, imeniaahidi kunifanya gaidi, tana gaidi mkubwa Duniani, hii ndio nafasi yangu ya pekee kuhakikisha kwamba nina andika historia kubwa dunia. Kama walivyo fanya kina Adolf Hitler na wengineo wengi”
Livna akakaa kwa muda huku akinitazama usoni mwangu, taratibu akanyanyuka kwenye kiti chake kisha akasimama mbele yangu.
“Twende tukaushangaze na kuibadilisha dunia sasa”
Livna baada ya kuzungumza meneno hayo akanibusu mdomoni mwanngu. Tukatoka chumbani humu na kuelekea upande wa pili wa meli. Tukaingia kwenye moja ya chumba, ndani ya chumba hichi nikakuta wasichana wakiwa bize na computer nyingi zilizopo humu ndani.
 
“Hichi ni chumba cha wawasiliano, hapa tuna mawasiliano ya kila serikali ya kila nchi zote duniani”
Livna alizungumza huku akiendelea kunionyesha jinsi wasichana hawa wakifanya kazi kwa juhudi zao zote.
“Njoo na kamera”
Livna alimuambia msichana mmoja kisha tukaingia kwenye chumba kimoja ambacho kina kitambaa kikubwa cha bluu kilicho funika karibia ukuta mzima wa upande wa kulia.
“Inabidi kujidhihirishia kwa dunia kwamba wewe ni gaidi”
Livna alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.
“Unahitaji kunirekodi?”
“Ndio, utaelezea juu ya tukio la FBI kunyonga wasichana hawa. Kisha utawaambia ni kitu gani na wewe ulicho kifanya.”
 
“Sura yangu nitahitaji kuifunika”
“Hakuna ananaye weza kuamini kama wewe ni gaidi ukifunika sura yako. Dany kwa sasa hakuna wakati wa huruma tena hakikisha kwamba kila kitu unakiweka hadharani”
Nikayafikiria maeno ya Livna kwa dakika takribani mbili, nikaona ni kweli hakuna haja ya mimi kuendelea kuificha sura yangu ikiwa ninatangazwa kila siku. Wasichana watatu wakaingia ndani ya chumba hichi wakiwa na kamera kubwa. Kila mmoja akaisimamisha kamera yake upande wake, nikasimama mbele ya tambaa hili la blue huku nikijiweka sawa nguo zangu za kijeshi nilizo zivaa.
 
“Dany si unajua nini cha kufanya?”
Livna alizungumza huku  akiwa amesimama nyuma ya mmoja wa wasichana hawa.
 “Ndio”
Kwa ishara ya vidole msichana mmoja akaanza kuesabu vidole vyake hadi ilipo fika tatu nikaanza kuzungumza.
“Hii ni kwa mara ya kwanza kujitokeza hadharani na watu wote Duniani munifahamu. Ninaitwa DANY. Leo mapema asubuhi kikosi cha FBI kimewanyonga wasichana waiso na hatia, walinzi wa raisi K2 aliye hitaji wasichana hao kunyongwa na kikosi chihi cha FBI kinacho pambana kila siku kuhakikisha kwamba kila siku wananikamata mimi”
Nikakaa kimya kwa muda kidogo huku nikiitazama kamera iliyopo mbele yangu.
 
“Hivyo sasa basi, kwa kitendo hicho cha FBI kuwanyonga wasicha wasio na hatia na kusikiliza amri ya raisi K2, nami nitakwenda kuliliza taifa hilo, kilio kinatacho gusa mamilioni ya watu duniani. Sikupenda kufanya hivyo ila mumenilazimisha kufanya hivyo na hichi ndio mutakwenda kukiona”
Baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo taratibu nikatoka eneo hili na kumfanya Livna kunipigia makofi.
“Yaani kama ulikuwa akilini mwangu, nilitamani useme hivyo na wewe umesema hivyo hivyo”
“Fupi tamu”
“Yaa. Ester hakikisha kwamba una edit hivyo vipande pamoja na video ipo humu kwenye simu yangu”
Livna alziungumza hukua kimkabidhi msichana huyu simu yake.
 
“Sawa mkuu”
“Itachukua muda gani?”
“Dakika kumi”
“Sawa hakikisheni munaitengeneza vizuri kisha unaileta humu ndani?”
“Sawa”
Wasichana hawa wakatoka huku kila mmoja akiwa na kamera yake.
“Una mpango gani na Wamarekani?”
Nilimuuliza Livna huku nikikaa kwenye moja ya kiti.
“Nilazima walipe kwa kile walicho kifanya”
“Hivi tuna nguvu ya kumpiga mmarekani, kwa maana video ambayo itakwenda kuruka baada ya muda mchache itashangaza na kuogopesha dunia?”
“Yaa acha ishangaze dunia, kikubwa ni kuhakikisha kwaamba kisasi tunakilipa kwa wote walio enenda kinyume nasi”
 
“Ohooo Mungu wangu, maisha haya ya kisasi yataisha lini sijui”
“Yataisha pale kila mzizi ulio pandwa na K2 tutakwenda kuukata”
Baada ya dakika kumi mlango wa chumba hichi ukafungiliwa, akaingia Ester akiwa ameshika laptop, akaiweka juu ya meza na kuanza kutuonyesha. Nilitarajia kuona nyuma lilipokuwa pazia kutakuwa na rangi ya hili pazia ila ni tofauti kabisa, kwani kuna muonekano wa kama ukuta ulio chakaa chakaa.
“Tumetengeneza madhari ya pangoni ili kuficha sehemu uliyopo”
“Vizuri”
Livna alijibu huku tukiendelea kutazama maelezo yangu ya mwanzo yanayo zungumzia FBI kuwanyonga wasichana hawa, video ya wasicha hawa kuanzia walivyo anza kuhojiwa hadi kunyongwa ikaanza kuonekana. Baada ya video hiyo kuishi maelezo yangu yakaendelea yakisisitizia kuiliza nchi ya Marekani kwa kile ninacho kwenda kukifanya. Video ya mimi ninavyo onekana nikimchinja raisi Donald Bush, ikaanza kuonekana.
 
“Hii video ni lazima iwalize watu”
Livna alizungumza hukua kijikaza kuangalia jinsi ninavyo kigawanyisha kichwa cha raisi Donald na kiwili wili cha mwili wake.
“Kwa staili hii hatuwezi kufika mbinguni?”
“Dany mbinguni si sehemu yako wala yangu, waachie wanaokesha makanisani na misikitini waingie mbinguni”
“Ester unaweza kuituma kwenye mtandao gani ambao utakuwa ni mwepesi kuweza kufikiwa na watu?”
 
“Twitter na Facebook”
“Unaweza kuirusha sasa hivi, na ninaomba mu hack kamera za maofisi ya ikulu ya  pamoja na Marekani, ninahitaji kuona reaction zao baada ya kuitazama hii video”
“Sawa mkuu”
Ester akatoka chumbani humu, nikarudia kuitazama video hii kwa mara yingine. Kusema kweli nilisha wahi kuona video kadhaa za magaidi wa kundi la Al-Quida, zikionyesha jinsi wanavyo waua mateka wanao wateka, ila kwa hii video yangu inakwenda kuvunja rekodi duniani, kwani nimemchinja raisi wa taifa kubwa ambalo linaogopwa karibia na dunia mzima.
“Ngoja niingie Twitter”
Livna alizungumza huku akianza kuminya minya batani za laptop hii, baada ya sekunde kadhaa ikafunguka.
“Mungu wangu!!”
Livna alizungumza huku akihamaki jambo lililo nistua sana.
“Nini?”
 
Livna akanigeuzia latpot hii.
“Ndani ya dakika sekunde hamsini, dieo imetazamwa na watu milioni kumi duniani, yaani ni amaizing”
Livna alizungumz ahuku akiwa amejawa na furaha kubwa kwenye uso wake.
“Dany twende tukaangalie reaction zao”
Livna akanyanyuka kwenye kiti na mimi nikajikuta nikinyanyuka, japo usoni nina tabasamu ila moyoni nina wasiwasi kidogo kwani hili jambo ni kubwa sana nililo lifanya. Tukakuta wasichana walipo humu ndani wakitazama video hii kwenye Tv kubwa inayo karibia kujaa ukuta mmoja humu ndani, huku wengi wao wakiwa na masikitiko ya kuona wezao wakiwa wananyongwa kikatili kwani hii ni taafira ambayo hawakuwa nayo. Livna akawacha wasichana hawa wamalize kuitazmaa video hii.
“Ninaombeni munisikilize”
Livna alizungumza na kuwafanya wasichana walio kaa kusimama na wote wakamgeukia yeye na kumtazama.
 
“Tupo katikati ya vita sasa, sikuhitaji kuwaeleza mapema kwani ingeathri utendaji wenu wa kazi. Catherini na Neema wamenyongwa leo asubuhi na kundi la FBI. Yule tuliye kuwa tunamlinda ndio ametugeuka na kututangazia kwamba sisi ni waasi. Ninacho wahitaji kuanzia hivi sasa ni kuhakikisha kwamba kila mmoja wetu, tuhakikishe kwamba tunajilinda na kufanya mashambulizi ya aina yoyote pale itakapo tulazimu kufanya hivyo. Ninaimani nyote mumenielewa”
“Ndio mkuu”
Wasicha wote walijibu kwa pamoja.
“Endeleeni na kazi”
Wasichana hawa kila mmoja akarudi kweye meza yake wote wakionekana kujawa na uchungu sana kwa kile walicho kiona.
“Ester umefanikiwa ku hack?”
“Ndio mkuu”
“Niwekee”
Tv hii kubwa ikaanza kuonyesha jinsi Wamrekani walivyo patwa na mstuko mkubwa, na viongozi wao wameanza mikakati ya kutafuta video hii imetokea wapi. Nchini Tannia napo, tukafanikiwa kupata video za ikulu, tukamuona K2 akishangaa sana kwa kile ambacho kimetokea.
 
“Ninaomba simu nimpigie K2”
Nilizungumza huku nikimtazama Livna usoni mwake.
“Unataka kumpigia sasa hivi?”
“Ndio”
Livna akatoa simu yake mfukoni, akatoa laini iliyopo na kuweka laini nyingine.
“Lini hii hakuna anaye weza kunasa mawasiliano yenu, unaweza kumpigia”
Livna akanikabidhi simu yake, nikaitazama namba ya K2, kisha nikaipiga na taartibu nikaiweka sikioni, nikamuona K2 akikabidhiwa simu na mlinzi wake, akaitazama kwa muda kisha akaipokea.
“K2 nina imani umekiona nilicho kifanya kwa Donald Bush, kama nimeweza kwake basi tambua kwako ni raisi sana kwani hapo sebleni ulipo kaa mmoja wa watu wako ana bomu mwilini mwake na sekunde yoyote kuanzia hivi sasa anakwenda kulipuka”
Nikamuona K2 akisimama simu akaiweka pembeni na kuanza kuwavua nguo watu wake mmoja baada ya mwengine jambo ambali kila mmoja aliyopo sebleni hapo alionekana kumshangaa raisi wao kwani wanamuona ni kama mwendawazimu aliye changanyikiwa.
 
AISIIIII……….U KILL ME 175
 
“Muheshimiwa raisi vipi?”       
Niliisikia sauti ya mmoja wa wamama ambaye ni mshauri wa karibu wa raisi.
“Kuna mtu anabomu, nani anataka kuniu?”
K2 alizungumza kwa ukali huku jasho likimwagika.
“Bomu muheshimiwa haliwezi kuingia ikulu kirahisi namna hii?”
“Munaona munaona alicho fanyiwa Donald, tayari amesha chinjwa na Dany na hapa ananipigia simu na kuanimbia mmoja wenu anabomu ni nani?”
 
K2 aliendelea kuzungumza kwa kufoka sana, walinzi wake wote wakabaki kukaa kimya kwani hakuna mwenye bomu na nimemtisha ili mradi kuichanganya akili yake.
“Vueni nguo”
Watu wote walipo  sebleni macho yakawatoka.   
“Nimesema vueni nguo”
Raisi akizungumza tayari amesha zungumza, watu wote wakaanza kuvua nguo zao kwa haraka haraka kwani nina imani kwamba wanamuogopa sana K2. Wakabakiwa na nguo za ndani.
“Bado badoo mtu anawea kuweka bomu hata ndani ya chupi yake na boksa”
Nilizungumza kwa sauti nzito na kunzidi kumchanganya K2 ambaye sisi wawili ndio tunazungumza na kuyasikia mazungumzo yetu.
“Vueni chupiii zenuu”
“Ahaaa…..muheshimiwa”
Jamaa mmoja alizungumza huku akimtazama K2 usoni mwake, kwani anaona sasa hichi kinacho endelea hapa sebleni ni masihara.
 
“Unapinga amri yangu eheee?”
K2 alizungumza huku akimfwata jamaa huyo.
“Sio hivyo muheshimiwa raisi ila huu ni uzalilish…….”
Jamaa wala hakumaliza sentensi yake, K2 akaokota moja ya bastola iliyopo chini na kumtandika risasi ya kichwa.
“Kuna mwengine, eheee nasema kuna mwingine anaye hitaji kufaaaaaa?”
Swali la K2 likawafanya watu wote kuvua nguo zao za ndani na kubakiwa kama walivyo zaliwa. Nikamtazama Livna kwa jicho la kuiba nikamuona jinsi anavyo kaukia kwa kucheka chini chini, nikatabasamu kwani watu wengine hapa walio vuliwa ni wamama watu wazima kabisa ambao wamempita K2 umri.
“Bomu lipo kwenye hiyo suti yako uliyo ivaa”
“Dany acha kunifanya mimi mjinga, nimawavulisha nguo watu hakuna bomu”
“Moja, mbili, ta……”
Nikaanza kumuoa K2 akivua koti lake la suti akalitupia pembeni, akaivua suruali yake ya suti na kuitupia pembeni, akaanza kujipasa mwilini mwake. Akaona haitoshi akavua shati lake na kubakiwa na skin taiti pamoja sidiria.
 
“Haya sasa lipo wapi hilo bomu”
Livna akatingisha kichwa kukataa nisimuambie avue zaidi ya hapo tumjengee kidogo heshima yake.
“Vua skin yako hiyo ndio bomu ukichelwa ninakuchangua kiuno chako. Puuuuuuuuu”
K2 kwa haraka akavua skin taiti yake na kubakiwa na chipi
“Waooo hujabadilika sana "
“Dany huu ni uzalilishaji, lazima nikuuee”
“Niue kama ulivyo muua mtu wako huyo ambaye ana familia inamtegemea. Utakwenda kuiambia vipi jamii ya Wata.Je wewe bado unafaa kuwa raisi? Jibu unalo kichwani mwako asubuhi njema”
Nikakata simu huku nikiangua kicheko kikali sana, nikamuona jinsi K2 anavyo kaa kwenye sofa huku akiwa amechoka sana.
 
“Hii video si imerekodiwa?”
“Ndio”
“Nayo tuirushe hewani?”
“Dany”
“Yaaa mwisho wa ubaya ni kudhalika”
“Dany kuna wamama watu wazima pale, unataka waonekane hadahrani?”
“Ndio, acha wajutie ni kwa nini waliamua kuajiriwa katika utawala wa K2”
“Sawa bosi, umefanya kazi nzuri acha iruke. Ester fanya yako mdogo wangu”
“Sawa mkuu”
Ester wala hakumaliza hata dakika mbili video hii akairusha kwenye mitandao yote ya kijamii. Video hii ikaanza kupata ushabiki mkubwa kuliko hata video ya kwanza inayo onyesha mauji ya wasichana wa Livna pamoja na raisi Donald Bush.
“Ukitaka kupambana na adui wako hakikisha kwamba unamuua kisaikolijia”
 
“Kwa hili lazima K2 anywe sumu, hahaaa hapana sijapata ona raisi kuwavua nguo watu wake”
Watu  wa K2 wakavaa nguo zao huku wengi wakionekana kuwa na masikitiko makubwa sana kwa udhalilishaji huu walio pewa na bosi wao. K2 akabeba nguo zake na kutoka sebleni humo huku akwia na hasira kali sana.
“Nini kinafwata?”
“Hapa ni kuwaangaliwa Wamarekani wana mipango gani dhidi yako, ila kwa K2 sasa hivi hana ujanja kwani jeshi alilo kuwa analitegemea ni watu wasichana wangu na ndio hao amesha watoa sadaka na nina imani kwamba hakuna hata mmoja ambaye anatamani kumuona au kumshikia”
“Poa, ninahitaji kwenda kuiona timu yangu, si unajua tangu nimeamka sijaonana nao”
 
“Poa twende, pia tukapate kifungua kinywa”
Tukatoka katika chumba hichi huku baadhi ya wasichana wakionekana kunishangaa sana, si kunishangaa kwasababu nimefanya tukio la ukatili wa kumuu raisi Donald Bush au tukio la kumdhalilisha K2, ila wananishangaa kwa matamanio ya kimapenzi.
“Wasichana wangu wanapata shida sana tangu jana walivyo kuona wewe na Samweli”
“Watazoea tu”
“Itawachukua muda sana kuzoea jinsia ya kiume kuiona humu ndani kwa maana walisha zoea kujiona wao tu, kama ni wanaume wanawaona kwenye filamu, miziki ila kukutana nao hivi uso kwa uso ni ngumu, labda wale ambao ninawatoa kwenda kufanya kazi maalumu za viongozi baadhi huko duniani”
“Hivi umesema kwamba hawa wote ni bikra?”
“Yaaa wote ni bikra?”
“Mmmm unashuhuli sana ya kuwalinda?”
“Unahisi kwamba nina walinda, ila sheria ni kali na zinatekelewa kwa utashi wa hali ya juu”
 
Tukafika kwenye sehemu ambayo jana tulipata chakula, nikawakuta Babyanka na wezake wakiwa wamekaa wakijipatia chakula taratibu.
“Mumeamkaje jamani?”
Niliwasalimia huku nikivuta kiti kimoja na kukaa.
“Salama, tumeona mambo yako uliyo yafanya kwa K2”
Winy alizungumza huku akinionyesha kwa kutumia kidole kwenye tv kubwa iliyopo humu ndani.
“Yaaa sasa hapo wananchi wao wenyewe ndio wataamua kufanya maamuzi juu ya K2, nina imani vyama vya kisiasa na wanachama wao hawato kaa kimya kuona udhalilishaji kama huo ulio fanywa na raisi, isitoshe amefanya mauji ya mtu asiye na hatia kabisa”
“Ila hii inaweza kuleta machafuko kwenye nchi?”
Babyanka alizungumza huku akinitazama.
 
“Video ya kwanza muliiona?”
“Ipi hiyo?”
Martin aliuliza huku akinywa juisi taratibu.
“Kama hamjaiona basi malizeni kupata kifungua kinywa mambo mengine yataendelea baadaye”
“Si tuitazame sasa hivi?”
“Hamuto kula baadhi yenu hususani mama kijacho hapo?”
“Kama inatisha mwenzenu, niacheni kwanza nile nikalale, hapa ninajisikia uchovu kama nini”
Hawa alizungumza na kweli ukimtazama usoni mwake unaona ni jinsi gani alivyo chokeana kwa ujauzito alio nao.
“Haja bosi kitambi meneja”
Winy alizungumza na kutufanya sote kucheka. Nikawatazama hawa watu nilio kaa nao moyoni mwangu nikajikuta nikiwa nimejawa na furaha kubwa sana kwani ni watu walio amua kuachana na kila kitu wanacho kipenda na kuamua kuingia kwenye harakati hizi za hatari na kuwa pamoja nami, mtu ambaye siwapatii hata shilingi kumi.
 
“Kusema kweli ninawashukuru sana, kwa huu umoja wenu ambao mumeweza kuujenga kwa ajili yangu. Mumejitoa maisha yenu na kuamua kuhaharisha maisha yenu kwa ajili yangu, ninawapenda sana zaidi ya sana. Nyinyi ndio familia yangu, nitabeba majukumu ya kuwalinda katika maisha yangu yote hata ikitokea nimekufa, basi nitakufa kwa ajili ya timu hii”
Nilizungumza kwa hisia kali huku machozi ya furaha yakinilenga lenga usoni mwangu. Taratibu Livna akanyanyuka akiwa ameshika glasi yake mkononi mwake, kwa ishara ya mkono akatuomba tunyanyuke, kila mmoja akiwa na glasi yake mkononi.
“Chiazi kwa misha marefu ya Dany”
Livna alizungumza na sote tukaanza kugongesheana glasi zetu ikiwa ni ishara ya kunitakia maisha mema na marefu. Taratibu kila mtu akaka kwenye kiti chake.
 
“Dany ninazidi kukuahidi kwamba nitakufa kwa ajili yako. Kwenye shida raha mateso tutakuwa pamoja mkuu wangu”
Martin alizungumza kwa msisitizo huku akinitazama usoni mwangu.
“Ninakushukuru Martin”
“Dany wewe mwenyewe umeona, nimetekeza jumba langu la kifahari kwa ajili yako, ni fika kwamba ninaheshimu mchango na uwepo wako kwenye maisha yangu. Nitasimama nawe bega kwa bega hadi kufa kwangu”
“Asante Winy”
“NSS, itakuwa inaukumbuka mchango wangu kwa asilimia nyingi sana. Niliipenda, ila Dany nimekupenda zaidi, nitasimama nawe, kwenye mvua, jua, masika au katika hali yoyote nitahakikisha pumzi yangu kama wataitoa basi wataitoa nikiwa ninakutetea wewe, Dany nipo kwa ajili yako”
“Asante sana Babyanka”
 
Nilizungumza huku machozi yakinimwagika kwenye mashavu yangu.
“Nipo tayari kufa……….. Kufa baada ya kukuzalia mtoto wako. Nilikusaliti kwa ajili ya ufinyu wa akili yangu Dany, ikiwa nina tambua ni jinsi gani ulivyo yahatarisha maisha yako kwa ajili ya nchi ambayo hata si chimbuko lako. Nilitakiwa bega kwa bega na viongozi wa Kimarekani kuhakikisha kwamba wanakupatia huduma sahihi kule ulipo kwenda kukamilisha kazi ya kuwaondoa Boko haramu kwenye ramani ya dunia. Nilifeli Dany,  nilishindwa kuzuia hisia zangu kwa raisi Donald Bush. Najutia kwa usaliti huo Dany. Nakuomba nikikuzalia tu mtoto, ninakuomba uniiue hata kwa kunikaba koo langu. Sinto hitaji kumuona mtoto wetu. Niue tu Dany”
Hawa alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake kwa wingi sana. Taratibu Hawa akasogeza kiti chake nyuma kisha akasimama pembeni ya kitu hicho, taratibu akapiga magoti huku akiendelea kulia sana. Nikanyanyuka kwenye kiti nilicho kalia na nikamsogelea taartibu. Nikamnyanyua Hawa na kumkumbatia.
 
“Ninaiani kwamba umejifunza kitu, sinto kuua. Wewe ndio mama wa mwanangu, mtoto atahitaji malezi bora kutoka kwako. Mimi baba yake sina maisha marefu hapa duniani, ninakuomba umlee kwenye mazingira mazuri, maadili mema. Kama ikitokea nimekufa ninakuomba usimueleze historia yangu kwani si ya kuigwa, ni historia mbaya na sihitaji kizazi changu kije kuishi kama kizazi cha magaidi, ninahitaji kizazi changu kiishi kama kizazi chema, chenyekufwata sheria za nchi na kufwata mafundisho ya Mungu sawa, Hawa?”
Hawa wala hakuweza kunijibu chochote zaidi ya kuangua kilio kikubwa sana. Nikaendelea kumbembeleza hadi akatulia. Nikarudi kwenye kiti na kukaa.
“Naombeni nikapumzike”
Hawa alizungumza huku akinitazama usoni mwangu. Nikamkubalia, taratibu akanyanyuka kwenye kiti chake, Babyanka naye akanyanyuka na kuanza kumshika mkono Hawa, kumpeleka ndani.
“Ukiachilia familia kubwa hii niliyo achiwa na waanzalishi, ila hii ni familia yangu nzuri kusema kweli ninawapenda na jisikieni mupo nyumbani kwani sisi sote ni wamoja katika vita hii”
“Shukrani Livna”
“Mwenye shida yoyote jamani, muwe huru, nipo kwa ajili yenu sawa jamani?”
Tumekuelewa dada”
Martin alijibu huku akitabasamu.
 
“Mwenzako Dany hadi leo ana pete yake ya ndoa, wewe pete yako umetupia wapi Martin?”
“Nikuulize na wewe yako ulitupia wapi?”
“Hahaaa tuachane na hayo, yamesha pita”
Babyanka akarudi na kukaa kwenye kiti chake.
“Ndugu zangu, hivi sasa dunia ipo kwenye hati hati ya kuingia katika vitaya tatu ya Dunia”
“Vita ya tatu ya dunia!!?”
Babyanka alizungumza huku macho yakiwa yamemtoka sana.
“Ndio. Dunia nzima kwa hivi sasa itakwenda kugawanyika katika makundi mawili, wao watakao waunga mkono Wamarekani kwa kuwanyonga vijana wawili wa Livna pamoja na kuuwawa kwa raisi wao. Pia wapo watakao tuunga mkono sisi kwa kumuua raisi wao ambaye alipeleka nchi mrama kwa ajili ya matakwa yake, hususani matakwa yake ya kimwili.”
”Ila mkuu hapo naona vita kuu ya tatu ya dunia haina haja, kwa maana kuna watoto wapya wanazaliwa. Sasa vita hiyo itakwenda kuhatarisha maisha ya kizazi kijacho”
 
“Hilo ni kweli Martin, ila muda mwengine si kila anaye ingia kwenye vita au anaye ingia kwneye uwasi wa jambo fulani si kama anapenda. Kuna watu nyuma yake ambao wanamchochoea na kumpeleka kuwa kama hivyo. Mfano mzuri ni mimi, sikuwaza hata siku moja kwamba nitakuja kujulikana duniani kama Gaidi, ila leo hii ninaitwa Gaidi, ukifwatilia kwa umakini historia ya maisa yangu utakuja kuamini kwamba mimi sina makosa makubwa kama wale wanao nisaka kwa udi na uvumba, usiku kucha wao ni kuniwazia mimi”
Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimtazama Martin usoni mwake.
“Sawa Dany, sasa hiyo vita wewe utakwenda kuiongoza vipi ikiwa upo mafichoni?”
“Mimi nitasimama kwa niaba yake, hata Osama Bin Laden alipigana na Mmarekani. Si yeye aliye beba silaha na kupambana na Mmarekani, ila watu wake walikwenda kwa niaba yake.”
 
Livna naye alizungumza kwa msisitizo na kunifanya nizidi kujiamini katika maamuzi haya.
“Hii meli ni nchi tosha, ina kila aina ya vifaa vya kijeshi ambavyo tunaweza kuishambulia nchi yoyote, na kwa muda wowote, na sehemu hii tulipo hukuna satelaiti hata mmoja duniani inayo weza kutuona hapa tulipo ila sisi ndio tuna uwezo wa kuweza kuiona nchi yoyote ambayo tunahitaji kuishambulia au tupo kwenye mpango nayo.”
Mlango ukafunguliwa akaingia Ester akiwa ameshika laptop moja kwa moja akamfwata Livna na kumuwekea mbele yake na kuanza kumnong’oneza na kutufanya sote tukae kimya huku tukiwatazama.  Livna akaitama laptop hii kwa sekunde kadhaa kisha akanyanyuka huku akiwa ameibeba, akaniomba nimfwate. Nikaanza kumfwata kwa nyuma, tukatoka katika chumba hichi na kusimama kwenye moja ya kordo. Akanikabidhi laptop hii, kisha Ester akanikabidhi earphone nikavaa msikioni.
“Mkuu wa jeshi la Marekani anahitaji kuzungumza nawe”
Livna alizungumza huku akiminya moja ya batani katika laptop hii, nikamuona mzee mmoja mwenye nguo zilizo jaa vyeo vingi.
“Habari yako Dany”
“Salama”
“Tunakupatia masaa ishirini na nne kujisalimisha kwenye jeshi lolote la Marekani, popote pale duniani kwa……”
“Hivi mzee una akili nzima, kujisalimisha kwangu sahau kwenye akili yako”
 
Ilinibidi kumkatisha mazungumzo mzee huyu kwani kitu anacho kizungumza ni upumbavu  mtupu.
“Sawa kama huto jisalimisha”
Wanajeshi wawili wakasimama nyuma ya mzee huyu huku wakiwa wamemshikilia mtu aliye valishwa kigunia cheusi kichwani mwake. Wanajeshi hawa wakamvua mtu huyo, moyo ukanistuka, mapigo ya moyo yakaanza kwenda kasi huku jasho jingi likinimwagika usoni mwangu, kwani mtu waliye mkamata ni Yemi msicha ambaye hadi leo ninaishi na upendo wake moyoni mwangu na pete yake ya ndo bado ipo kidoleni mwangu, mzee huyu akasogea pembeni taratibu na hapo ndipo nikaona tumbo la Yemi ambalo limevimba kidogo, ikiashiria kwamba ni mwanamke mjamzito.
“Huyu ni mke wako wa ndoa, ni mjamzito sasa. Chagua kati ya mke na mtoto au kujisalimisha mbele ya jeshi la Kimarekani”
Sikujibu kitu chochote zaidi ya kutetemeka mwili mzima, maumivu ya moyo ninayo yasikia kusema kweli hayana mfano, kwani nilimuacha Yemi aende akaishia maisha yake salama salimin kwani ninatambua maisha yangu ni maisha ya hatari sana kwa kila ninaye ingia naye kwenye mahusiano ya kimapenzi.
 
ITAENDELEA
‘Haya Wamarekani wamemkamata mke wa ndoa wa Dany. Wanamtumia Yemi ambaye ni mjamzito sasa, wanahitaji ajisalimishe mikononi mwao je Dany atajisalimisha? Usikose sehemu inayo fwata ya hadi hii ya kusisimua kutoka kwa muandishi mahiri Eddazaria G.Msulwa”


from MPEKUZI

Comments