Mo Dewji aitakia kila la kheri Taifa Stars

Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Mo Dewji ametoa salamu za kheri kwa Timu yetu ya Taifa ya mpira wa miguu, Taifa Stars katika kuelekea mchezo wa kufuzu AFCON dhidi ya Lesotho.

Dewji amesema kuwa ushindi wa leo dhidi ya Lesotho utaleta furaha kubwa kwa Watanzania, kwani ni miaka 38 tangu timu ya taifa ifuzu michuano hiyo kwa mara ya kwanza.

“Nawatakiwa kila la kheri Taifa Stars katika mchezo wa leo dhidi ya Lesotho. Ushindi wa leo utarudisha furaha ya Watanzania ya kukosa kushiriki AFCON kwa miaka 38. Tunaamini mtafanya vizuri sababu nia tunayo na uwezo tunao. Mungu awe nanyi,“ameeleza Mo Dewji kupitia ukurasa wake wa Twitter.



from MPEKUZI

Comments