Watu 26 wanashikiliwa, kutekwa kwa Mo Dewji

Watu 26 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam akiwemo, Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara kwaajili ya uchunguzi zaidi kutokana na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo’ ambaye pia ni mwekezaji wa klabu hiyo.

Taarifa za kutekwa kwa mfanyabiashara huyo anayekadiriwa kuwa na utajiri wa Sh3.5 trilioni zilianza kusambaa Alhamisi ya Oktoba 11, saa 1:00 asubuhi katika mitandao ya kijamii, kabla ya polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam kuthibitisha saa mbili asubuhi.

Akithibitisha kukamatwa kwa idadi ya watu hadi Jumapili Oktoba 14 ,Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa idadi imeongezeka na kufikia 26 na uchunguzi bado unaendelea.

"Mpaka sasa wanashikiliwa watu 26, na bado uchunguzi unaendelea endapo idadi ikiongezeka au kupungua tutawajuza", amesema Mambosasa.

Kuhusu idadi ya walioachiwa huru na majina yao, Mambosasa amekataa kutoa taarifa hiyo akidai inaweza kuathiri sehemu ya uchunguzi.


from MPEKUZI

Comments