Viongozi Wampigia Simu Nay Wa Mitego Kupongeza Kwa Wimbo wake wa ALISEMA

Staa wa muziki wa Bongofleva Nay wa Mitego leo amedai kuwa Viongozi wengi nchini wameonekana kumshangaza, baada ya kumpigia simu na kumpa pongezi nyingi kutokana na ngoma yake mpya ya “Alisema” aliyoiachia rasmi October 6,2018.

Nay Wa Mitego amesema amekuwa akipokea simu nyingi kutoka kwa viongozi tofauti tokea aachie ngoma hiyo, kitu ambacho kinamshangaza na kumpa maswali mengi, kuwa ni kitu gani wamekipenda kwenye ngoma yake ya ‘Alisema’ mpaka kumpa pongezi hizo.

“Napokea simu na msg nyingi za pongezi kutoka kwa viongozi tofauti tofauti wengine sijawai kuwaza hata kuzungumza nao au kuhisi kama wanasikilizaga hata nyimbo zangu. Watu wa kawaida pia kuhusu huu wimbo  ‘Alisema’ najiuliza nini kikubwa kipo kwenye hii ngoma?

“Maneno niliyoongea? Beat? Style niliyoimba? Chorus? kama ni verse ipi ya kwanza ya Pili? Au watu wamechoshwa na nyimbo za mapenzi kila siku.? Huu ni wimbo wa Taifa🇹🇿”Ameandika Nay wa Mitego

==>>Usikilize hapo chini


from MPEKUZI

Comments