Sponsored Post: Kwanini Wanawaume Wenye Pesa Za Kichawi Huwa Wanatumia Pesa Nyingi Sana Kuwahonga Wanawake Zao?
DOKTA MUNGWA KABILI : 0744 000 473.
Je Mwanaume Mwenye Pesa Za Kichawi Anaweza Kutumia Uchawi Huo Huo Kumroga Mwanamke Kimapenzi ?
Kama Jibu Ni Ndio Kwanini Basi Wanawaume Wenye Pesa Za Kichawi Huwa Wanatumia Pesa Nyingi Sana Kuwahonga Wanawake Zao ?, Kwanini Wasitumie Tu Uchawi Wa Mapenzi Ili Kujiepusha Na Gharama Za Kutumia Pesa Nyingi Kwa Kitu Ambacho Uchawi Unaweza Kufanya.?Hili ni swali nililo ulizwa na kijana mmoja ambae amejitambulisha kama msomaji mzuri wa makala zangu.
YAFUATAYO NDIO MAJIBU YANGU :
Kwanza kabla ya yote unatakiwa ujue mwanaume huyo ambae unasema ana pesa za kichawi amezipata kwa kutumia tambiko la aina gani.
Na hii ni kwa sababu matambiko ya biashara na mali yamegawanyika katika aina kuu mbili.
Aina ya kwanza ni matambiko yanayo julikana kama MATAMBIKO BARIDI na aina ya pili ni matambiko yanayo julikana kama MATAMBIKO YA MOTO.
Linapokuja suala la matumizi ya pesa kwa wanawake, ni vigumu sana kwa mtu asie na jicho la tatu kutofautisha baina ya mwanaume anae tumia matambiko baridi katika biashara zake na mwanaume anae tumia matambiko ya moto katika biashara zake kwa sababu wote huwa wanatoa pesa nyingi sana kwa wanawake.
TOFAUTI NI HII HAPA CHINI
MWANAUME ANAE FANYA BIASHARA ZAKE KWA KUTUMIA MATAMBIKO BARIDI.
Mwanaume ambae anafanya biashara zake kwa kutumia matambiko baridi hutoa pesa nyingi kwa mwanamke kwa lengo la kuitumia nyota ya mwanamke huyo katika biashara na shughuli zake zote za kumuingizia riziki na kipato.
Ni hivi katika ulimwengu usio onekana, ukitaka kuchukua nyota ya mtu kwa njia rahisi kabisa, ni kumfanya mtu huyo akutegemee wewe kwa kila kitu hususani katika masuala yote yanayo husu pesa na rizki kwa ujumla.
Ukifanikiwa kumfanya mtu yoyote Yule akutegemee wewe kwa kila kitu, kuanzia kula chakula, kuvaa, na mambo yote muhimu katika maisha hasa hasa yale yanayo husu rizki basi unakuwa umeichukua nyota yake na matokeo yake milango yake yote ya kuingiza rizki inahamia kwako.
Riziki yake inakuwa inapitia kwako. Mlango wake wa kuingizia riziki unahamia kwako. Mtu huyo anakuwa hawezi kupata pesa yoyote ile bila pesa hiyo kupitia kwenye mikono yako.
Ili mtu huyo apate rizki yoyote ni lazima rizki hiyo ipitie kwanza kwako.
Kwa hiyo mwanaume huyu anapokuwa anakupa wewe mwanamke pesa nyingi maana yake ni kwamba anakupa pesa zako mwenyewe.
Kama nilivyo dokeza hapo juu kwamba njia hii ni njia ya halali kabisa kwa sababu wote mnafaidika .
Anaeitumia nyota yako anafaidika na wewe ambae nyota yako inatumika unafaidika pia.
Kwa lugha nyepesi mwanaume huyo anakuwa anasafiria nyota yako.
Ndio maana sharti kuu la kutumia njia hii ni lazima umtunze vizuri mtu ambae anakutegemea wewe kwa kila kitu.
Kadri unavyo mtunza vizuri na kumpa mahitaji yake muhimu ndivyo mambo yako katika biashara na shughuli zako yatakavyo kuwa yanakunyookea.
Hii ni njia ya asili na ya halali kabisa, hata wewe unaesoma makala haya unaweza kuwa unasafiria nyota za watu wengine bila wewe mwenyewe kujua wala bila wao wenyewe kujua.
Kwa mfano kama una watu wanao kutegemea wewe kwa kila kitu kama vile mke, watoto, au wazazi na wewe unajitahidi kuwatunza na kuwapa mahitaji yao ya muhimu basi milango yao ya rizki inahmia kwako na rizki yako inakuwa kubwa na wala unakuwa hauwezi kuishiwa kabisa.
Ni rahisi kwa mwanaume ambae hana kabisa watu wanao mtegemea kuishiwa na kukosa hata hela ya kula lakini mwanaume mwenye wategemezi kama vile watoto. Ndio maana hata kwenye mabar na sehemu za starehe wanaume walio kwenye ndoa ndio wanao ongoza kwa kutoa ofa za pombe kuliko ambao hawana wategemezi.
Kama una nafasi unashauriwa usiishie kuwatunza watoto, mke na wazazi wako tu , jaribu kutafuta na watu wengine ambao unaamini wana mahitaji maalumu katika maisha lakini hawana watu wa kuwasaidia.
Kwa mfano watoto yatima. Unaweza kwenda kwenye kituo cha watoto yatima ukachukua mtoto mmoja au wawili kwa kadri Mwenyezi Mungu alivyo kujaalia na kwenda kuishi nao nyumbani kwako au kama nyumbani kwako hauna nafasi ya kuwaweka basi uwe unawapelekea mahitaji yao hapo hapo kituoni kwao.
Hii ni njia rahisi sana na ya uhakika ya kufungua na kuongeza milango ya rizki.
Ni njia mujarab sana na watu walio tumia njia hii wamepata mafanikio makubwa sana katika shughuli zao zinazo husisha vipato vyao.
MWANAUME ANAE FANYA BIASHARA ZAKE KWA KUTUMIA MATAMBIKO YA MOTO
Mwanaume huyu anakupa pesa nyingi sana wewe mwanamke kwa sababu pesa zake ni pesa za kichawi ambazo hazina thamani.Chenye thamani ni nyota yako.
Kwanza kabla ya kuanza kukupa pesa zake, anaanza kwanza kwa kuimiliki nyota yako kichawi.
Na anapata uhalali wa kiroho wa kumiliki nyota yako baada ya kutoa sadaka maalumu kwa ajili ya kumiliki nyota yako.
Mwanaume huyu anakuwa anaitumia nyota yako katika shughuli zake na anakuwa anapata pesa nyingi sana kupitia nyota yako.
Pesa anazo kupa wewe ni pesa za kichawi ambazo anakuwa amezipata kwa kufanya matambiko ya moto.
Ni pesa ambazo zina thamani tu katika ulimwengu wa rohoni lakini hazina thamani katika ulimwengu wa nyama.
Ili pesa hizo ziwe na thamani ni lazima atafute mtu mwenye pesa zenye thamani katika ulimwengu wa nyama kwa ajili ya kubadilishana nae.
Mtu huyo ni wewe kwa sababu nyota yako ina utajiri mkubwa.
Kwa hiyo anacho kifanya hapo anakuwa anakupa pesa zake za kichawi ambazo hazina thamani kwa kubadilishana na nyota yako ambayo thamani yake ni mara elfu zaidi ya pesa anazo kupa.
Hii haina tofauti na uchawi wa chuma ulete. Wachawi wanao chukua pesa za watu kwa chuma ulete huwa wanakuwaga na pesa za kichawi pia ambazo hazina thamani katika ulimwengu wa nyama.
Ili pesa ziwe na thamani ni lazima wazibadilishe na mtu mwenye pesa zenye thamani katika ulimwengu wa nyama.
Ndio maana mtu wa chuma ulete akikupa pesa yake ukamrudishia chenji. Hiyo chenji uliyo mrudishia ndio yenye thamani na sio ile aliyo kupa.
KUHUSU WANAUME WENYE PESA ZA KICHAWI KUWAROGA KIMAPENZI WANAWAKE.
Kwa kawaida mwanaume mwenye pesa haitaji kutumia uchawi kumroga mapenzi mwanamke.Uchawi wanao weza kuutumia wanaume hawa ni kumfunga mwanamke asiende kwa mtu mwingine kwa sababu za kinyota.
Hataki nyota ya mwanamke wake ichafuliwe kwa sababu tendo la kujamiiana ni moja kati ya mambo makuu yanayo chafua nyota za watu kwa kiasi kikubwa sana.
Kwa hivyo mwanaume huyu hatumii uchawi wa jamii ya limbwata katika kumroga mapenzi mwanamke isipikuwa atamfunga tu kichawi mwanamke huyo asiwe na mwanaume mwingine kwa sababu za kinyota.
Hata hivyo yapo mazingira yanayo walazimisha wanaume hawa kuwaroga mapenzi wanawake wanao wataka .Hasa hasa pale anapo gundua mwanamke Fulani ana nyota kali ya biashara, mali na utajiri.
Mwanaume anae fanya biashara zake kwa kutumia uchawi akigundua kuna mwanamke ana nyota kali ya biashara, mali na utajiri basi atafanya juu chini kumpata mwanamke huyo hata kama ni mke wa mtu.
Hata kama mwanamke huyo yupo kwenye ndoa na mumewe na wana watoto zaidi ya mmoja, mwanaume mwenye kutafuta pesa kichawi atafanya juu chini ampate mwanamke huyo.
Na hii ni moja kati ya sababu ya ndoa nyingi sana kuvunjika siku hizi licha ya kuwa wanandoa mmepata watoto na watoto wenyewe bado wadogo.
Kinacho tokea mwanaume huyu akigundua kuwa mwanamke Fulani ana nyota kubwa ataanza kwa kutumia njia zake zote za kawaida ili kumnasa kimapenzi mwanamke huyo kama vile kutoa pesa, zawadi kubwa kubwa na kadhalika.
Mwanamke huyu akiweka ngumu licha ya jamaa kutumia njia zake zote ikiwemo pesa kushindikana, basi ndipo mwanaume huyu huamua kutumia uchawi sasa.
Hii ni njia inayo fanywa hata na wachawi katika shughuli zao za kichawi.
Wachawi wakitaka kufanya misheni yao ya kichawi huwa wanaanza kwanza kwa kutumia njia za kawaida. Njia za kawaida zikishindwa ndipo sasa hutumia uchawi.
Kwa mfano A na B ni mke na mume wanao pendana sana na wanafanya shughuli zao na zinawaendea vizuri. Wachawi hawapendi kuwaona A na B wakiwa pamoja kwa upendo .
Watakacho kifanya wachawi hao ni kuanza kupeleka maneno ya umbea kwa A na B ili kuwagombanisha.
Maneno ya umbea yakigonga mwamba sasa ndio wachawi hao huamua KUPELEKA MAJESHI. Kupeleka majeshi maana yake ni kufanya uamuzi wa kutumia silaha za kichawi kukamilisha misheni yao na uamuzi huu ukishafikiwaga huwa haubatilishwi.
Vivyo hivyo mwanaume huyu anapokutana na mwanamke mwenye nyota ya mali huanza kumtongoza kwa kutumia njia za kawaida na njia za kawaida zikishindikana basi ndio hutumia uchawi.
Wakati mwingine mwanamke huyu kwa sababu anakua anampenda mume wake na ndoa yake na hataki kuwasumbua watoto wake anaweza kumkubalia mwanaume huyo kama mchepuko, lakini lengo la mwanaume huwa ni mwanamke huyo awe wake peke yake.
Kwa hiyo hata baada ya kuwa katika mahusiano na mwanamke huyo, mwanaume huyo ataendelea kumshawishi mwanamke huyo aachane na mume wake.
Juhudi za kumshawishi mwanamke huyo kwa njia ya kawaida zikishindikana basi ndipo mwanaume huyo huamua kutumia uchawi wa kuwatenganisha mwanamke huyo na mume wake na yeye mwanaume kumchukua mke na kwenda kuishi nae.
Mwanaume aliye kimbiwa na mkewe katika mazingira haya anaweza kujiona hana thamani na kwa kudhani labda ana kasoro kumbe kilicho tokea ni kitu kingine kabisa ambacho hata mke wake akijui.
Ushauri wangu ukiwa na mkeo hakikisha unamtunza na kumuhudumia kwa kila kitu bila kujali na yeye ana kazi au lah.
Wazee wetu walikuwaga na msemo wao mzuri sana ambao vijana wa siku hizi wanautumia vibaya. Wazee walikuwa na msemo usemao “ Mwanamke ni kama mtoto “ sasa bahati mbaya vijana wa siku hizi msemo huu wanauchukulia kumaanisha kwamba mwanamke ana akili kama za mtoto.
Watu wenye mtazamo huu wanakosea sana . Wazee waliposema wanawake ni kama watoto walimaanisha kitu kimoja tu, nacho ni MATUNZO.
Mtoto wako hatakiwi kuwaza atakula nini au atavaa nini, mtoto wako akiumwa atakacho kiwaza ni uchungu wa dawa au maumivu ya sindano na sio kwamba atapata dawa au la.
Vivyo hivyo mke wako au mwanamke wako hatakiwi kuwaza atakula nini au atavaa nini nakadhalika.
Wewe unatakiwa kuwaza kwa ajili yake na ni lazima uwaze kwa ajili yake kwa sababu usipo waza kwa ajili yake watatokea wanaume wengine ambao watawaza kwa ajili yake na kuchukua nafasi yako.
Asili ya wanawake ni kuishi kwenye utajiri kwa sababu nyota zao ni nyota za utajiri. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu alivyo waumba. Hakuwaumba wateseke.
Ndio maana HAWA alimkuta ADAMU akiwa tayari kwenye bustani ya Edeni ambayo ndani yake kulikuwa na kila kitu. Katika ulimwengu usio onekana EDEN maana yake ni utajiri.
Simaanishi kwamba kama wewe sio tajiri usioe au usiwe na mwanamke, hapana namaanisha unapokuwa na mwanamke au mke jitume fanya kazi kwa bidii na umtunze mkeo kwa kila kitu, ukifanya hivyo basi utachukua nyota yake na wewe pamoja na yeye mtapata mafanikio makubwa sana kwa sababu wanawake karibu wote wana nyota za mali na utajiri na wasio kuwa na nyota za mali na utajiri ni wale ambao nyota zao zimechafuliwa. Katika ulimwengu usio onekana, hapa ndipo unapokuja ule msemo “nyuma ya mafanikio ya kila mwanaume kuna mwanamke”.
Sura ya saba ya kitabu changu “ MAMBO TISA YANAYO UNDA NYOTA YA MWANADAMU: UHUSIANO KATI YA NYOTA YA MTU NA MAFANIKIO YAKE KATIKA MAISHA ina itwa “ NAFASI YA NYOTA YA MWANAMKE KATIKA MAFANIKIO YA MUME WAKE “.
Watu wengi walio pata bahati ya kusoma kitabu changu hicho wameniomba sura hiyo niitolee kitabu chake yenyewe na nina wa ahidi kuyafanyia kazi maombi yenu.
Nitakapo kamilisha kuandika kitabu hicho basi nitawatangazia ili mpate kujifunza zaidi.
Kwa ambao hawakubahatika kupata nakala za kitabu changu mnaweza walau kusoma maelezo kuhusu kitabu hicho kupitia : http://mungwakabhili.blogspot.com/2018/06/mambo-tisa-yanayo-unda-nyota-ya.html
MAKALA HAYA YAMESIMULIWA NA DOKTA MUNGWA KABILI. DOKTA MUNGWA KABILI ANAPATIKANA KUPITIA SIMU NAMBA : 0744 000 473.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment