Simba SC yatangaza kufanya kisomo juu ya mlezi na mwekezaji wa timu hiyo, Mo Dewji

Uongozi wa klabu ya Simba umetangaza kufanya kisomo hii leo siku ya Ijumaa huku lengo kuu ikiwa ni kumuomba Mwenyezi mungu aweze kuleta wepesi kwenye matatizo yaliyompata mlezi na mwekezaji wa timu hiyo, Mohamed Dewji aliyetekwa jana.
"Uongozi wa Klabu ya Simba unapenda kuwataarifu Wanachama, Wapenzi na Washabiki wake kuwa mchana wa leo baada ya Sala ya Ijumaa (Saa 8.00) kutakuwa na *KISOMO* katika Makao Makuu ya Klabu Mtaa wa Msimbazi.

"Lengo la *KISOMO* hiki ni kumuomba Mwenyezimungu aweze kuleta wepesi kwenye Matatizo yaliyompata Mlezi na Mwekezaji wetu Bw. Mohamed Dewji “MO”

"Tunapenda kuwakaribisha katika Kisomo hiki muhimu ili kumuomba Mungu aweze kumlinda na kumrejesha Mwenzetu salama. *Tunatanguliza Shukrani*"



from MPEKUZI

Comments