Serikali Yampa ONYO Kali Mtendaji Mkuu Mabasi ya Mwendo Kasi Dar

Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo, ametoa onyo kwa Mtendaji Mkuu wa wakala wa usafiri wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar es saalam Dart Mhandisi Ronald Lwakatare, kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake na kumtaka kujieleza ni kwanini ameshidwa kumsimamia mtoa huduma UDART.

Pia Mhe. Jafo amemwagiza Naibu Waziri wake Joseph Kakunda leo kufanya kikao kitakacho jumuisha mtendaji mkuu wa Dart pamoja na mtoa huduma UDART   ili kuweza kubaini matatizo makubwa ambayo yamekuwa yakichangia huduma hiyo kudorola kwa siku za hivi karibuni.

“Usafiri huu ulikuwa ni neema sana kwa wakazi wa Dar es salaam ambao wengine walikuwa wanatumia zaidi ya masaa matau kutoka Kimara kwenda Posta lakini leo hii kupitia usafiri huu wanatumia takribani dakika 40 hadi 45 hivyo hatuwezi kuacha huduma ziendele kudorola kwa kiasi hiki”amesema Jafo

Pamoja na kumwagiza naibu Waziri pia Jafo amemtaka katibu mkuu Tamisemi Mussa Iyombe, kufanya uchunguzi katika ofisi ya Dart ili kuweza kuona kama wapo watendaji ambao wanakwamisha huduma hiyo ili kuweza kuwaondoa na kutoa nafasi kwa wengine watakao fanya kwa ufanisi.

Waziri Jafo amesema kuwa onyo hilo kwa mtendaji mkuu wa DART linakuja kutoka na yeye kushindwa kumsimamia mtoa huduma wa mradi huo UDART ambaye ameshindwa  kufanya kazi zake kwa ufanisi.

Aidha amesema kutokana na kushindwa kusimamia kumekuwepo na malalamiko mengi kwa watendaji wa mradi huo wakiwemo madereva pamoja na wakatisha tiketi hali ambayo imesabaisha watu kukosa huduma.

Jafo pia amemwagiza Mtendaji mkuu huyo kuhakikisha mchakato wa kumpata mtoa huduma wa kudumu unafanyika haraka ili kuweza kufanya kazi katika ubora ulio tarajiwa na wananchi.

“Usafiri huu wa mabasi yaendayo kasi ulishalipatia heshima Jiji la Dar es Salaam  hadi kupata cheti cha kuwa na usafiri uliobora na watu kutoka mataifa mbalimbali wamekuwa wakija kujifunza kwetu juu ya mradi huu hivyo hatuwezi kuendelea kuwafumbia macho watendaji ambao hawatimizi majukumu yao”amesema Jafo.


from MPEKUZI

Comments