Serikali kuliweka kwenye kumbukumbu gari la Nyerere lililokarabatiwa na Veta

Serikali imesema italichukua na kulihifadhi kama kumbukumbu ya vitu alivyokuwa anatumia hayati baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere, gari alilokuwa akitembelea mwaka 1968 na kuundwa upya na Chuo cha Ufundi Stadi (Veta), mkoani Kilimanjaro.

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ally Mohamed Shein, amesema hayo jana katika sherehe za  kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru baada ya kutembelea banda la Veta na kujionea gari alilokuwa akitumia mwalimu wakati wa harakati zake za kutafuta uhuru ambapo pia aliwapongeza vijana hao kwa umahiri wa kutengeneza gari hilo.

“Vijana hao wameonyesha kwamba wamefuzu vizuri na wameonyesha uzalendo, Serikali inatambua mchango huo.

“Serikali itaongeza vyuo vya ufundi Tanzania Bara na Visiwani kwa lengo la kuhakikisha vijana wanapata fursa ya kujiunga na vyuo hivyo ili waweze kujiajiri,” alisema Dk. Shein.


from MPEKUZI

Comments