Sakata la Kawaha ....Rais Magufuli Kaagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, OCD, Mkuu wa Upelelezi, Mkuu wa Kituo Kyerwa Wasimamishwe Kazi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera Augustine Ollomi, Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Kyerwa Justine Joseph, Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kyerwa Everist Kivuyo na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kyerwa Robert Marwa.

Viongozi hao wa Polisi wanasimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za kuhusika katika magendo ya zao la kahawa katika Wilaya ya Kyerwa pamoja na tuhuma nyingine.

Aidha,Rais Magufuli amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mej. Jen Jacob Kingu na Inspekta Generali wa Polisi Simon Sirro kuhakikisha uchunguzi wa kina unafanyika na hatua stahiki zinachukuliwa endapo watabainika kuhusika katika magendo ya kahawa na makosa mengine kwa mujibu wa sheria.

Tuhuma dhidi ya viongozi wa polisi katika Wilaya ya Kyerwa zimebainika  wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa.


from MPEKUZI

Comments