Saed Kubenea , Komu Waomba Radhi

Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao walikuwa wakituhumiwa kwa makosa ya kutaka kumzuru moja ya kada wa Chama hicho ambao ni Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea pamoja na Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu wameomba radhi baada ya kuhojiwa na kamati kuu ya Chama hicho.
 
Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu bara, John Mnyika wajumbe wa  kamati kuu ya chama hicho kiliwakuta  na hatia wabunge hao baada ya kukiri kuwa sauti zilizosambaa ni zao ambapo walitangaza kuwapa adhabu mbalimbali.

Akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na Athony Komu wameomba radhi kwa baadhi ya viongozi ambao wametajwa kwenye sauti iliyokuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii.

“Kwa niaba yangu binafsi wananchi wa ubungo na chama changu nichukue nafasi hii kusema yaliyotokea siku hiyo ilikuwa ni bahati mbaya sana, tunaomba radhi kwa chama chetu na wengine wote waliomuizwa na tukio hilo.”Amesema Kubenea

“Nataka niseme chama ni kikubwa kuliko sisi wote, tumeshawasilisha barua ya kuomba radhi kwa yaliyotokea na sasa tunaomba radhi kwa chama chenyewe na wapenzi wote wa chadema, na zaidi wale ambao walitajwa tunawaomba radhi, ninamuomba radhi sana mwenyekiti Mbowe, Meya Jakob Borniface wa Ubungo.” Amesema Komu

Katika kikao cha kamati kuu ya Chama hicho wabunge hao wamepewa adhabu nne ikiwemo kuvuliwa nafasi zao za uongozi ndani ya chama hicho, kuwa kwenye uangalizi kwa kipindi cha miezi 12, kuandika barua ya kuomba radhi kwa chama, pamoja na kupewa onyo kali.


from MPEKUZI

Comments