Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 15

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA  
“Hata kama, ila nahitaji wale vijana nao niwafanye kitu kibaya”
“Kweli?”
“Ndio”
“Twende”
“Wapi?”
“Si sehemu walipo ukawafanyie kitu kibaya”
“Si unaona kabisa nina jeraha”
“Huniamini au?”
Nikamtazama Ethan kwa muda kidogo, kisha nikachomoa sindano inayo ingiza maji kwenye mishipa yangu. Nikashuka kitandani, Ethan akanikumbatia kwa kasi ya ajabu tukatoka katika eneo hili la hapo hospitalini na kuanza safari ya kwend aeneo walipo vijana ambao walinipiga na kunichoma kisu changu katika mbavu zangu.

ENDELEA
 Kwa uwezo wa Ethan, ndani ya muda mchache tukafika katika moja ya jumba bovubovu ambalo kidogo lipo nje ya mji.
 
“Hapa ndipo wanapo ishi?”
“Ndio”
Ethan alizungumza huku tukisimama nje ya mlango wa kuingilia. Taratibu Ethan akaanza kugonga mlango huu.
“Sasa kwa nini tunagonga”
“Unahisi tukiingia kwa staili tulio ijia unahisi watakutambuaje, kesho si watasema wewe ni jini, ikiwa jini ni mimi”
“Mmmh”
“Yaa, tena ninaingia ndani ya mwili wako”
Ethan akapotea kwenye uwepo wa macho yangu. Mwili mzima ukanisisimka na kujihisi ni mtu mwenye nguvu sana. Mlango ukafunguliwa, akasimama kijana ambaye kwa haraka niliweza kumtambua kwani yeye ndio aliye anza kunisemesha siku walipo nivamia.
 
“Hei wewe mtu mweusi umekuja kufanya nini hapa?”
Jamaa alizungumza kwa dharua. Nikamsukumia ndani, nikashangaa kumuona jamaa akipaishwa kimo cha mbuzi na akatua kwenye moja ya meza na kuiangukia hadi ikavunjika vunjika jambo ambalo liliwastua wezake wengine.
“Ni useng** gani huuu”   
Mwenzao mmoja alizungumza huku wakiacha kucheza game ya mpira kwenye tv iliyopo hapo sebleni na kunifwata. Woga na wasiwasi kama nilio kuwa nao kwa siku ya kwanza wote umeniondoka, maumivu kwenye jeraha langu sikuweza kuyahisi kabisa mwilini mwangu. Kuna kijana humu ndani akaokota kitu chake kuhakikisha kwamba ana nivamia.
 
Wakaanza kunishambulia ila kila walivyo jaribu niliweza kuwadhibiti kisawa sawa na kila niliye mpiga ngumi aliambulia ngumi au teke lililo wapelekea kuvunjika katika sehemu hiyo ambayo nitampiga. Ndani ya muda mfupi vijana wote nane nikafanikiwa kuwadhibiti na kila mmoja ana ugulia maumivu huku wengine wamepoteza fahamu.
“Unatakiwa kuwaua ili siri yako isitoke”
Niliisikia vizuri sauti ya Ethan  masikioni mwangu.
“Ethan kuua ni dhambi”
“Watakuua wewe siku, waue wote”
Ethan alizungumza kwa ukali, nikawatazama vijana hawa jinsi wanavyo pata shida ya maumivu. Roho ya kuwaua ikaanza kunijaa. Huruma ya kibinadamu ikafutika kabisa, nikaanza kuwavunja shingo mmoja baada ya mwengine. Zoezi la kuwaua halikumaliza dakika hata tano.
“Kazi nzuri”
 
Ethan alizungumza huku akitoka mwilini mwangu.
“Ngoja nifute ushahidi wote”
Ethan alizungumza huku akizikusanya maiti hizi na kuziweka eneo moja. Akanyoosha mkono wake wa kushoto, nikastuka sana mara baada ya kuona ukitoa moto mwingi ulio sababisha maiti za vijana hawa kuanza kuwaka. Tukatoka nje na Ethan kwa uwezo wake wa kijini akaendelea kuichoma nyumba hii na kuwaka moto mkubwa sana. Kama tulivyo kuja hapa ndivyo tulivyo rudi hospitalini na hakuna nesi aliye weza kugundua.  
 
‘Ninaondoka ila hakikisha kwamba siri ya mauaji humuambii mtu wa aina yoyote hata Camila mwenyewe sawa’
“Sawa”
Ethan akaondoka katika eneo hili. Kupitia tv iliyomo humu ndani kwangu, nikaona taarifa juu ya kuungua kwa jumba moja lililopo nje ya mji huku ikisadikika kuna watu wemeungulia ndani ya nyumba hiyo. Taarifa hii kidogo ikanipa wasiwasi kwa maana watendaji wa tukio hilo ni mimi na Ethan.
 
    Asubuhi taratibu zikaendelea kama kawaida, madaktari wakanitembelea na kunichoma sindano za kukausha kidonda. Baada ya wiki moja nikaruhusiwa kutoka hospitalini hapa nikiwa na afya yangu nzuri kabisa. Nikakaa siku chache nyumbani kisha nikarudi shule kuendelea na masomo yangu ya darasa la pili. Kurudi kwangu shule imekuwa ni furaha kwa waalimu na wanafunzi wezangu. Maasomo yakazidi kusonga mbele huku ushiriki wangu kwenye michezo ukizidi kuinyanyua shule kwenye mashindano mbali mbali ndani na nje ya nchi ya Ujerumani. Ufauliji wangu katika masomo nao ukazidi kunifanya niwe kipenzi cha wanafunzi wengi sana, huku Camila kadri ya siku zinavyozidi kwenda ndivyo jinsi tulivyo jikuta tukizama kwenye penzi letu.
                                                                                                                 ***   
    Nikiwa na umri wa miaka kumi na mbili nikamaliza elimu ya msingi na nikachaguliwa kwenda shule ya vipaji maalumu huku Camila akichaguliwa kwenda katika shule nyingine ya jinsia moja ya kike ila ni karibu sana na shule yetu hii ya kiume. Nikiwa kidato cha pili, nikaletewa maombi mengine ya kujiunga na timu nne kubwa za mpira ambazo ni Liverpool, Real Madrid, Bacelona na Beyurn Munich.
“Ethan unaitwa”
 
Mwenzangu mmoja aliniita nikiwa bwenini nikipitia pitia baadhi ya mikataba niliyo tumiwa kwa njia ya barua pepe na mameneja wa timu hizo kwani kipaji changu cha mpira kimekuwa kikubwa kwa hali ya juu.
“Na nani?”
“Mkuu wa shule”
Nikarudisha mikataba hii ndani ya kabati langu, nikalifunga kisha nikaanza kuongozana na kijana huyu kuelekea kwa mkuu wa shule. Nikaingia ofisini kwake na kumkuta akiwa peke yake. Nikamsalimia na akaniomba niweze kukaa kwenye kiti kilichopo pembeni ya meza yake.
“Samahani kwa kukutoa kwenye mapumziko yako”
“Hakuna tabu mwalimu”
“Kuna taarifa imekuja hapa sio njema kidogo kwako na wala kwetu”
 
Nikajiweka vizuri kwenye kiti huku nikimtazama mwalimu mkuu usoni mwake.
“Nimepokea simu kutoka nyumbani kwenu na dada yako ndio alinipigia”
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda kasi huku nikimtazama mkuu wa shule.
“Unatakiwa kwenda nyumbani sasa hivi kwa maana hali ya mzee wako haipo vizuri sana. Tumekuandalia helicopter ya shule na itakuepeleka hadi nyumbani kwenu”
Nikashikwa na kigugumizi na nikashindwa hata kujua ni kitu gani ninaweza kukizungumza, kwani mzee Klopp ni zaidi ya baba kwangu, kwa maana amekuwa ni mpiganaji na ni mtu ambaye amenifunza mambo mengi sana hususani kwenye maisha ya mpira. Nikiwa katika hali ya bumbuwazi,  akaingia sekretari wa shule.
 
“Mkuu helicopter ipo tayari kwa kuondoka”
“Sawa, nenda na Ethan hakikisha kwamba humuachi peke yake hadi pale atakapo fika nyumbani kwao”
“Sawa mkuu”
Tukatoka ofisini humu na moja kwa moja tukaelekea katika kiwanja cha helicopter. Tukaingia ndani ya helicopter hii na taratibu tukaanza safari ya kuelekea nyumbani huku akili yangu ikijaribu kutengeneza picha ya hali ya nyumbani nitakavyo ikuta. Akili yangu moja inaniambia kwamba mzee Klopp amefariki huku akili yangu nyingine inaniambia kwamba mzee Klopp yupo hai.
 
‘Ethan upo wapi rafiki yangu’
Nilimuita Ethan kimoyo moyo pasipo hata sekretari wa shule kuweza kusikia kitu chochote. Ndani ya dakika kumi na tano tukafika katika jumba la mzee Klopp ambapo napo kuna uwanja wa helicopter, nikafunguliwa mlango na mmoja wa walinzi wa jumba hili la mzee Klopp, nikashuka na nikaanza kukimbia kuelekea ndani ya jumba hili.
Ukimya nilio ukuta sebleni ukanistua sana, kwa haraka nikapandisha ngazi kuelekea gorofani, nikakutana na madaktra wawili kwenye kordo wakizungumza na dada Mery. 
“Ethan”
Dada Mery aliniita huku kwa haraka akinifwata na kunikumbatia kwa nguvu huku akilia kwa sauti ya chini sana
“Baba yupo wapi?”
“Yupo chumbani”
 
Sikutaka hata kuulizia hali yake ipo vipi kwa haraka nikaingia ndani ya chumba cha mzee Klopp, nikamkuta akiwa amewekewa mashine za kupumulia huku pembeni yake akiwa amekaa bibi Jane Klopp. Bibi Jane Klopp taratibu akanyanyuka huku akinitazama usoni mwangu. Macho yake yamebadilika rangi na kuwa mekundu sana, anaonekana ni mtu ambaye alikuwa akilia kwa muda mrefu sana. Bibi Jane Klopp akanikumbatia kwa muda huku akilia. Mzee Klopp akanitazama kwa muda huku akihema kwa shida sana, kwa ishara ya mkono wake wa kulia akaniita. Nikamuachia bibi Jane Klopp na kumfwata mzee Klopp kitandani alipo lala.
“Eth…a….”
 
Mzee Klopp aliniita kwa shida sana, machozi yakaanza kunimwagika usoni mwangu.
“Ndio baba”
“M…ua…an..ngalie mama yak….o na dada yako”
“Mimi…..ni….nakufaa, ila hakikisha kwamba unatimiza ndoto zako sawa mwanangu?”
“Sawa baba”
“Makampuni yote yapo chini yako, wewe ndio mmiliki na nilisha weka kila kitu kwa mwana sheria hakikisha kwamba unayaongoza katika msingi na msimamo mzuri. Hakikisha kwamba huyumbishwi na umri wa mtu yoyote sawa”
Mzee Klopp alizunugmza kwa kujikaza sana
“Sawa baba”
 
Mzee Klopp akanitazama kwa muda kidogo, kisha akaniomba niweze kumkumbatia. Taratibu nikamuinamia na kumkumbatia. Kwa ishara mzee Klopp akamuita mke wake naye akamuomba amkumbatie, nikatoka nje na kumuita dada Mery akaingia chumbani humu tukawakuta bibi Jane Klopp na mume wake wakiwa wamekumbatiana huku wote wakiwa wanalia kwa uchungu sana. Dada Mery naye akajumuika mama yake katika kumkumbatia baba yake.
Mlio wa mashine ya kumsaidia kupumua, ikaanza kutoa mlio mithili ya alarm. Jambo lililo tufanya tushtuke sana na kuogopa kwa haraka wakaingia madaktari na wakamuomba bibi Jane Klopp na mwanaye wamuachie mzee huyo. Madaktari kwa kutumia mashine maalumu wakaanza kumstua kifuani mzee Klopp. Mashine hizo hazikuweza kufanya kazi kwani bado kijimstari cha rangi nyekundu kinaonekana kwenye mashine hiyo.
 
Madaktari wakajitahidi kulifanya zoezi hilo ndani ya dakika tano, kisha wakatugeukia huku wakiwa na sura za masikitiko sana. Daktari mmoja akatingisha kichwa akiashiria kwamba mzee Klopp hatupo naye tena duniani. Nikamshuhudia bibi Jane Klopp akianguka chini na kupoteza fahamu. Dada Mery akajitahidi kwa uwezo wake kuhakikisha kwamba hapati mstuko, ila bumbuwazi lililo mpata hakika limemfanya abaki amekaa pembeni ya mwili wa marehemu pasipo kufanya jambo lolote. 
 
Kwa kusaidiana na madaktari hawa wawili tukasaidiana kumnyanyua bibi Jane Klopp na kumlaza kwenye moja ya sofa na akaanza kumpatia huduma ya kwanza. Hali ambayo inayo endelea ndani humu hakika imenifanya nami niwe nimekaa njia panda, hakika sijui nianzie wapi, kwani kila linalo endelea ninahisi ni kama muujiza ambao natamani siku zirudi nyuma ila ninashindwa.
“Ethan”
Daktari mmoja aliniita kwa ishara tukatoka nje ya chumba hichi.
“Mzee ameondoka duniani, wewe kama mwanaume hivi sasa tunakutegemea kuweza kutoa kauli ya familia kama mwanaume. Dada yako ndio kama vile unavyo muona alivyo. Mama naye ndio kama vile, tunakusikiliza”
Maneno ya daktari huyu yakanifanya nimkodolee tu macho na kushindwa hata kumjibu jambo la aina yoyote.
“Ethan”
“Naam”
“Umenielewa kitu ninacho hitaji kukizungumza”
“Ndio nimekuelewa”
“Jiandae katika hilo na tunahitaji mwili wa mzee kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kabla haujaanza kuharibika”
 
“Ngoja kwanza kwani mzee alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa gani?”
“Saratani ya damu ndio ilikuwa inamsumbua”
“Kwa nini sikuweza kuambiwa hadi leo amefariki ndio ninaambiwa hili jambo?”
“Mzee mwenyewe alihitaji usiambiwe”
“Kwa nini?”
 
“Kwanza ni kutokana na umri wako, pili ni kutokana na masomo.”
Nikafumba macho yangu taratibu kisha nikayafumbua.
“Hakikisheni kwamba habari ya kufa kwa baba haivuji hadi pale nitakapo wambia sawa”
“Sawa Ethan”
Nikarudi ndani ya chumba hichi na kumshika mkono dada Mery na kutoka naye ndani humu. Tukaingia chumbani kwangu, Mery akanikumbatia kwa nguvu na kuanza kulia kwa uchungu sana, nikaanza jukumu la kubembeleza taratibu.
 
“Ethan kweli baba amekufa”
“Yaa amekufa, ila nakuomba ujikaze sasa”
“Eheee”
“Nahitaji ujikaze nitazame nitazame”
Nilizungumza huku nikimshika dada Mery mashavuni mwake. Tukatazamana kwa sekunde kadhaa.
“Sisi ndio tulio baki sasa, tujikaze na tushirikiane katika hili, ukiniacha mimi mwenyewe katika hili nitashindwa sawa dada yangu”
“Ehee”
“Sasa sikia kitu kimoja, nahitaji niweze kupata kitabu cha orodha ya mameneja wote wa kampuni za mzee na wale wanasheria wake wawili. Si unafahamu kitabu kilipo?”
“Ndio”
 
“Twende ukanipatie”
Tukatoka katika chumba changu na kuelekea katika ofisi ya mzee Klopp. Dada Mery akafungua moja ya kabati, tukaona shelf ya chumba akaingiza namba za siri ambazo niliweza kuziona. Akafungua mlango na akatoa kitabu hicho chenye majina na namba za simu za watu wote ambao ni wasimamizi wa makampuni ya mzee Klopp ambayo ni zaidi ya kumi na mbili. Nikaanza kazi ya kumpigia kila mmoja na kumuomba aweze kufika katika nyumba ya mzee Klopp haraka iwezekanavyo kwani kuna kikao cha dharura. Ndani ya lisaa moja mameneja kumi na mbili pamoja na wanasheria wawili wakafika nyumbani humu, huku kila mmoja akishangazwa na wito wangu, kwani haukuwa ni wito wa kubembeleza zaidi ya kuwa wito wa kuamrisha.
 
“Kijana mdogo inakuwaje unatuita kwa kutuamrisha?”
Mzee mmojaa alizungumza kwa kufoka huku wakiwa wamekaa sebleni hapa.
“Mzee kabla sijamaliza kuzungumza nilicho waitia kuanzia hivi sasa huna kazi”
Maneno yangu yakawafanya watu wote kustuka sana, hata dada Mery mwenyewe akaonekana kustushwa kwani maamuzi yangu hakuna hata mmoja aliye yataarajia kwamba nitayatoa hivyo.

==>>ITAENDELEA KESHO


from MPEKUZI

Comments