Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 12

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA  

‘Ethan”
Niliisikia sauti ya Ethan mwenzangu, ikiniita nyuma yangu ambaye uhalisia wake ni jini.
“Shitii umenistua sana”
‘Nisikilize sina muda mwingi sana. Kesho usiende hiyo safari kwa maana mukifika nchini Uingereza mmoja wenu kati ya baba yako au wewe atapigwa risasi na kufa hivyo musiendeee”
Maneno ya Ethan yakanistua sana moyo wangu, hakuhitaji hata nimuulize swali, akapotea mbele ya upeo wa macho yangu na kunifanya niwe katika wakati mgumu sana ulio iyeyusha furaya yangu mithili ya barafu katika jua kali.

ENDELEA
“Ethan kwa nini tusiende”
“Nimekuambia kwamba sina muda mwingi, hakikisha kwamba safari hii haifanikiwi sawa”
Ethan mara baada ya kuzungumza hivyo akapotea mbele ya uwepo wangu wa macho. Wasiwasi mwingi ukazidi kunitawala, hamu ya kwenda Uingeraza yote ikaniishia. Nikajikuta nikikaa chini na machozi yakianza kunimwagika.
‘Ethan niambie basi kama ulicho nieleza ni uongo’
Nilizungumza huku machozi yakinimwagika usoni mwangu.  Nikiwa katikati ya hali ya huzuni, mlango ukagongwa na nikasikia sauti ya Mery akiniita.
“Ethan umesha maliza?”
“Ndio dada ninakuja”
Nilizungumza huku nikianza kujifuta machozi yangu usoni. Nikaendelea kujifuta hadi nikamaliza. Nikanyanyuka kwa haraka na kufungua mlango. Mery akanitazama usoni mwangu huku macho yake akionekana kama mtu mwenye mashaka juu yangu.
 
“Ulikuwa una lia?”
Mery aliniuliza huku akiwa amenikazia macho.
“Hapana nilikuwa nina omba dada, kwa maana ni batati kubwa niliyo ipata”
“Ninaweza kuingia?”
“Ndio”
Mery akaingia na kukaa kitandani kwangu nami nikaka kitandani kwangu huku nikimtazama.
“Ethan ni mambo mangapi ulisha wahi kudanganya?”
Swali la Mery likanistua kidogo
“Kivipi dada?”
“Mimi ni daktari na ninauwezo mkubwa sana wa kumgundua mtu akifanya jambo hilo nikiwa nina mtazama tu machoni mwake. Natambua kwamba haukuwa una Sali, niambie ukweli ni kitu gani ambacho kimekukosesha furaha na amani?”
 
Nikajifikiria kwa muda huku nikiwaza nimueleze ukweli juu ya hili nililo ambiwa na Ethan, ila kusema kweli bado ninapata kigugumizi.
“Au Camila amekukataza kwenda huko?”
“Ndio dada”
“Ohoo usijali, nitazungumza na mama yake amshawishi ili akubali muende”
“Amesema kwamba tukienda huko anahisi kuna jambo baya litatokea”
“Hahaa…ana wivu tu, hakuna kitu kibaya ambacho kitakwenda kuwapata wewe na baba sawa. Kikubwa ni wewe ujiandae kwa safari kesho na hakikisha kwamba ukifika una muwakilisha baba vizuri, sawa Ethan”
Maneno ya Mery yakazidi kuniny’ong’onyeza japo nimejaribu kupindisha ukweli, ila anaonekana haelekei kabisa katika pointi yanug ya msingi ambayo nimeimaanisha.
“Sawa dada”
 
“Leo nitatoka kwenda mjini, nitakuletea nguo nzuri za kuvaa kesho sawa”
“Sawa dada”
Mery akatoka ndani humu huku akiwa ameishika simu yake mkononi. Nikajilaza kitandani huku nikijaribu kufikiria safari ya kesho ambayo tayari imesha anaza kuingia kikwazo. Nikajaribu kumuita Ethan kwa mara kadhaa ila hakuweza kuitika, wala kuzungumza nami katika ufahamu wangu wa akili. Usingizi taratibu ukanipitia kwani ukichanganya na uchovu wa mazoezi na kuamka asubuhi sana na mapema, sikuwa na sababu yoyote ya kuto kuacha kulala.
                                                                                                              **
Familia nzima ikatusindikiza hadi katika uwanja wa ndege huku tukiwa na wawakilishi wa wawili kutoka katika timu ya Liverpool. Kila mmoja wetu kusema kweli furaha imemjaa usoni mwake, kwani safari hii ni ya mafanikio na kila mtu ana amani kwamba ndio mwanzo wangu mzuri wa kuingia katika soka la kulipwa huku nikiwa na umri mdogo sana.
Tukaingia katika ndege binafsi iliyo tumwa kutoka nchini Uingereza. Tukaingia na kukaa katika siti nzuri ambazo zimewekwa katika eneo lililo tengenezwa kwa mfumo kama wa sebleni, kwani kuna Tv na friji ndogo. Nikiwa katikati ya furaha, gafla akatokae Ethan na kusimama pembeni yangu, nikawatazama watu wote wa humu ndani na sikuweza kumona hata mmoja wao aliye weza kustuka kutokana na uwepo wa Ethan katika eneo hili.
 
‘Mbona umekaidi maneno yangu?’
Ethan alizungumza kwa sauti nzito ambayo kwa kipindi cha awali alipo kuwa akizungumza nami ndio alikuwa akiitumia.
‘Etha…..’
‘Hivi hujui kwamba nina kulinda eheee, nikikuambia kwamba usifanye kitu kwa nini hunielewi au unajiona kwamba wewe una uwezo mkubwa kuliko mimi si ndio?’
Ethan aliendelea kufoka kwa hasira. Kusema kweli leo ndio nimeweza kumuona jini huyu akifoka kwa fujo na uzuri wake wote ukatoweka. Mwili mzima ukaanza kunitetemeka.
‘Ethan nilishindwa kumshawishi baba na tayari alisha fanya mawasiliano na hawa watu ndio maana leo hii tupo humu ndani ya ndege’
 
Ethan akamtazama mzee Klopp anaye cheka na kururahi huku simu yake akiwa ameiweka sikioni mwake.
‘Ethan rafiki yangu nakuomba ubadilishe mambo mabaya yatakayo tokea huko mbeleni, tafadhali ninakuomba sana.’
Ethan hakuzungumza chochote zaidi ya kuniangalia kwa mcho ya hasira. Akapotea kwenye uwepo wa macho yangu na kunifanya nizidi kuogopa, nikashusha pumzi nyingi sana huku nikimtazama mzee Klopp anaye zungumza na marafiki zake. Nikatamani kuzungumza jambo ila ndege tayari imesha anza kutembea. Ndege ikaanza kupaa angani huku nikishuhudia tukiiacha ardhi ya nchini Ujerumani taratibu.
“Ethan sasa mwanangu unakwenda kuwa nyota wa dunia”
Mzee Klopp alizungumza kwa furaha sana.
“Asante baba”
“Ukijituma ndio siri kubwa ya mafanikio sawa”
“Sawa baba”
 
Ndege ikazidi kuchana mawingu. Gafl ikaanzaa kuyumba na kutufanya watu wanne yulipo katika eneo hili kuanza kupatwa na wasiwasi. Kwa haraka muwakilishi mmoja akajifunga mkanda siti yake vizuri. Hali ikazidi kuwa mbaya mara baada ya ngede kugeuka, juu chini, chini juu, nikamshuhudia kiti cha mzee Klopp kikichomoka na akagongeza kichwa chake kwenye meza ya tv na kikapasuka. Mlango wa ndege hii ukachomoka na upepe mwingi sana ukaingia ndani, muwakilishi mmoja naye akachomolewa huku akipiga makelele mengi sana na akapotelea hewani. Huyu muwakilishi wa pili naye nikamshuhudia akiangukiwa na firi miguuni mwake na ikakatia vipande vipande, friji hili linalo onekana ni zito kama shelf ya kuhifadhia zitu vya siri, likaanza kumbingiria na kunipabiza kwenye mbavu zangu na kujikuta nikitoa ukeleke mmoja mkali sana wa maumivu.
                                                                                                                **
Nikastuka kutoka usingizi huku nikipiga kelele nyingi sana, nikaanza kujipapasa kwenye upande wangu katika mbavu ambapo friji imenibamiza ila nikajikuta nikiwa nipo salama salmin. Nikashusha pumzi nyingi sana huku macho yakiwa yamenitoka kisawa sawa.
“Ethan, Ethan”
Bibi Jane Klopp akaingia ndani humu huku akiniita jina langu, akaka pembeni ya kitanda changu huku akinitazama jinsi ninavyo mwagikwa na jasho jingi.
“Una nini?”
Bibi Jane Klopp aliniuliza huku akiwa amejawa na wasiwasi mwingi sana usoni mwake.
“Ni ndoto mbaya mama”
“Ohoo pole mwanangu”
Bibi Jane Klopp alizungumza huku akinikumbatia kwa nguvu.
“Ndoto yako ina husiana na nini?”
“Ajali mama, naogopa”
“Ajali ya nini?”
 
Bibi Jane Klopp alizungumza kwa wasiwasi mwingi sana huku akinitazama usoni mwangu. Nikashusha pumzi taratibu, kwa viganja vyake akaanza kunifuta jasho linalo nimwagika usoni mwangu.
“Baba yupo?”
“Ndio yupo ofisini kwake”
“Naomba nizungumze ndoto hii mbele yake”
“Sawa twende”
Bibi Jane Klopp akanisaidia kushuka kitandani, tukaelekea hadi ilipo ofisi ya mzee Klopp, tukamkuta yupo na wanaume wawili, kwa kuwatazama vizuri moyo wangu ukastuka sana, kwani ndio wanaume ambao nimewaona kweney ndoto niliyo iota muda mchache ulio pita.
“Ethan wasalimie wawakilishi kutoka katika timu ya Liverpool wamekuja na private jet yao ambayo kesho ndio tutaondoka nao”
 
Mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio mara baada ya mzee Klopp kuzungumza maneno hayo. Nikajitahidi sana kuiweka sura yangu ya furaha mbele ya watu hawa ila nikajikuta nikishindwa kabisa, kwani picha ya ajali tuliyo ipata ndotoni kila mara ina jirudia kichwani mwangu.
‘Ehee Mungu naomba unisaidie hili lisitokee’
Nilijitahidi kuzungumza kimoyo moyo huku nikiwatazama watu hawa. Nikawasalimia kwa heshima sana na wao wakaonekena kufurahishwa.
“Kijana wako ni mzuri sana, kwa hakika akiendelea kuwa hivi, timu itakuwa imepata mtu mzuri sana”
“Ni kweli, nimemkuza kwenye maadili mazuri ambayo nyinyi nyote mutaipenda tabia yake”
“Ethan mimi nina itwa John Mendez”
Muwakilishi mmoja alizungumza kwa furaha huku akinipa mkono.
 
“Nashukuru kukufahamu”
“Na mimi ninaitwa Lucas Leivis pia ni muwakilishi wa uongozi mzima wa timu ya Liverpool.”
“Nina shukuru sana kwa kuwafahamu”
“Tumeleta hund ya benk ya pand milioni kumi kwa ajili yako tu, hiyo itakuwa ni pesa yako ya kuanzia maisha utakapo kuwa jijini Liverpool kwa maana tumezungumza na mzee hapa na amakubali kwamba makazi yako yote kuanzia kesho yatahamia jijini Liverpool Uingereza.”
Macho yakazidi kunitoka hata bibi Jane Klopp akaonekana kustuka kidogo kwa kauli hiyo.
 
“Samahani munaweza kutupa nafasi nikazungumza na mume wangu?”
Bibi Jane Klopp alizungumza huku akimtazama mzee Klopp usoni mwake.
“Ohoo samani, jamani kwa furaha niliyo kuwa nayo nimejisahau kumtambulisha mke wangu. Anaitwa Jane Klopp”
“Tunashukuru kukufahamu maam”
“Nami pia nina washukuru kuwafahamu karibuni sana na mujisikie kama mupo nyumbani”
“Sawa sawa mama, kutokana tumesha maliza kuzungumza na mzee hapa, basi sisi acha twende, na hundi hii tunamkabidhi Ethan na hundi ya meneja wake ambaye ni mzee hapo tumesha mkabidhi hundi ya paundi milioni thelathin”
 
“Sawa asanteni baba zangu na Mungu awabariki”
Bibi Jane alizungumza kwa upole huku akiwatazama wawakilishi hawa.
“Tunashukuru mama yetu”
Wawakilisha hawa wakanyanyuka kwenye viti walivyo kuwa wamekalia, na wakaanza kutoka huku mzee Klopp akiwafwata kwa nyuma, huku kwa ishara akituomba tuweze kumsubiria anakuja. Tukaka kwenye viti walivyo kwua wamekali, bibi Jane Klopp akaichukua hundi niliyo pewa, akaisoma kwa muda kidogo kisha akaiweka mezani huku akiachia msunyo unao onyesha dhairi amekasirishwa na maamuzi ya mume wake. Baada ya muda kidogo mzee Klopp akaingia huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana usoni mwake.
 
“Mke wangu Ethan amezidi kuing’aza familia yetu na jina langu sasa linazidi kwenda kukua”
“Hembu njoo ukae hapa na uniambie kwa nini umeamua kufanya maamuzi yako wewe kama wewe, ikiwa mtoto ni wa kwetu wote na hakuna jambo kubwa ambalo unalifanya bila ya kuhitaji ushauri wangu?”
Bibi Jane Klopp alizunguzma huku sura yake akiwa ameikunja kwa kweli.
“Jamani mke wangu, hili swala si lipo wazi?”
“Lipo wazi kivipi, umenitarifu hata walipo kuja hawa vijana eheee?”
 
“Mke wangu, tuliza basi jazba”
“Klopp siku zote za maisha yetu sikuwahi kukupinga kwa maamuzi yako yoyote ambayo ulikuwa unayafanya kama baba na mume kwenye maisha yangu. Ila kwa hili la Ethan kwenda kuishi Uingereza hapana. Mtoto bado ni mdogo, miaka nane na kiasi chote hicho cha pesa unahisi Ethan ataweza kuhimili vishawishi vya Uingereza tena katika jiji la Liverpool ambalo limejaa wendawazimu na walevi?”
Bibi Jane Klopp alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake. Furaha ya mzee Klopp yote ikaondoka usoni mwake na kujikuka akikaa kwenye kiti chake taratibu.
“Kwa nini umeingiwa na tamaa ya pesa mume wangu na kuamua kuchukua pesa za watu pasipo kusika chochote kutoka kwetu, kama ungeona mimi sifai kwenye hayo maamuzi yako, umeshindwa hata kumuuliza Ethan, kweli eheeee?”
 
“Mke wangu kwa hilo nina kuomba uni samehe, nakiri nimefanya kosa na sipendi kukuona unalia mbele ya mtoto. Ethan nina kuomba uweze kwenda nje kidogo nizungumze na mama yako”
“Hapana hawezi kwenda nje ana jambo muhimu anahitaji kulizungumza kwetu sisi na nilikuja naye humu ili aweze kuzungumza kile alicho kiota”
Mzee Klopp akanitazama usoni mwangu, akagundua wasiwasi mwingi sana ambao ninao.
“Eti Ethan mwanangu una wasiwasi wa kitu gani ehee?”
Mzee Klopp alizungumza kwa sauti ya upole na unyeyekevu sana huku akinitazama usoni mwangu. Nikajaribu kufungua kinywa ila nikajikuta nikishikwa na kigugumizi kwa maana sifahamu hata nianzie wapi kusimulia ndoto niliyo iota kwani watu wawakilishi hawa nilio waona kwa macho yangu ya nyama ndio hawa hawa nilio waona kwenye ndoto yangu.
“Baba”
“Naam”
“Mama”
 
“Bee mwanangu”
“Munanipenda na kunisikiliza kwa kile nitakacho waomba”
“Ndio mwanangu, zungumza chochote tutakupatia”
Mzee Klopp alizungumza kwa shahuku huku akitengeneza tabasamu zuri usoni mwake, akisubiri ni nini ambacho waomba.
“Kwa…..usala…ma wangu na nyinyi. Baba sitaki kwenda nchini UINGEREZA tena na pesa za watu nakuomba uzirudishe”
Mzee Klopp macho yakamtoka, akasimama kwa hasira huku mikono yake miwili akiipiga mezani kwa nguvu hadi mimi na bibi Jane Klopp tukastuka, kwani anaonekana kukasirika waziwazi 

==>>ITAENDELEA KESHO


from MPEKUZI

Comments