Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 06

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588 
ILIPOISHIA   

Nikamuona Camila akiingia kwa kasi uwanjani, breki ya kwanza akanirukia na kunikumbatia kwa nguvu huku akiliwa kwa furaha. Mechi tu ya kirafiki imeonekana kama mechi ya mashindano makubwa ya kugombania kombe.
“Nakupenda Ethan, nakupenda sana Ethan”
Camila alizungumza huku akiendela kunikumbatia kwa nguvu na machozi yakizidi kumiminika usoni mwake, nikajikuta nikishindwa hata kuzungumza kwani hara rafiki zake bonge walio nipiga leo bafuni, wote wakanifwata na kunikumbatia, kasoro Bonge tu yeye mwenyewe ndio amebaki nje ya uwanja huku akiwa amenuna sana na dhairi anaonyesha kwamba bado ana kinyongo na mimi.

ENDELEA
Mwalimu wangu wa darasa akanipongeza sana huku akionekana kuto kuamini kile kilicho tokea uwanjani. Tukarudi mabwenini huku nikipongezwa na kila mwanafunzi mwenzangu. Kusema kweli tangu nije kwenye hii shule, leo ndio ambayo nimetokea kupendwa na kila mwanafunzi.  Hata bafuni wachezaji wezangu hawakusita kunipongeza kwa uwezo wangu mkubwa sana nilio weza kuuonyesha katikati mchezo wa mapira na ukitegemea sisi wote bado ni watoto wadogo.
‘Unafuraha sasa?’
Niliisikia sauti ya rafiki yangu akiniongelesha.
‘Yaa nina furaha ulikuwa wapi wakati wote?’
‘Kuna mambo nilikwenda kuyafwatilia na leo nitakupeleka kwetu ukapaone’
‘Kwenu?’
‘Ndio, ili uwe mtu maarufu ni lazima ukapaone kwetu’
‘Si usiku tutakwenda?’
‘Ndio’
‘Sawa’
 
Nikaendelea kujifuta maji mwilini mwangu, kisha nikavaa nguo za kushindia usiku, kutoka na baridi kila mwanafunzi akavalia koti lake. Wachezaji wezangu hawakuhitaji kuniacha kila nilipo kwenda, basi wao wapo nyuma yangu. Tukapanga foleni katka bwala la chakula, sifa zikazidi kuniandama hadi kwa wadada wakubwa wa madarasa mengine. Kitendo hichi dhairi kikaanza kumkosesha amani Camila, akanifwata katikati ya wadada hawa wanao niuliza mambo mawili matatu huku nikiwa nimeshika sahani yanu ya chakula, akanichukua na tukatafuta meza yetu iliyo jitenga na tukaka.
“Tukae hapa wenyewe”
Camila alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.
“Mbona kama umekasiria ikiwa leo ndio siku ya furaha?”
“Sitaki kukuona na wale wadada”
“Kwa nini?”
“Sitaki tu”
“Mmmmm”
 
Mlinzi wa Camila akaleta chakula kisha wakasimama mbali kidogo na meza hii.
“Hawa walinzi wanakulinda muda wote?”
“Ndio, ila ninapo kwenda kulala huwa waniacha na wanakuja kuchukuliwa na asubuhi wanakuja tena”
“Wanachukuliwa na kina nani?”
“Hawa ni usalama wa taifa, hivyo lazima wakaripoti makao makuu”
“Ahaa”
“Ila leo Ethan umefanya jambo moja ambalo ni la kushangaza sana”
“Jambo gani?”
“Si kufunga magoli matatu na kusaidia timu kutoka nyuma magoli matano hadi kushinda. Nakuhakikishia ukiwa hivyo basi hadi unakuwa mkubwa basi vilabu vikubwa hapa Ujerumani vitawahi kukununua”
“Hahaaa kweli?”
“Kweli vile na ninapenda kukuambia jambo moja”
“Jambo gani?”
Camila akaka kimya kidogo huku akinitazama usoni mwangu.
 
“Zungumza”
“Ethan nina kupenda, nataka uwe mchumba wangu”
Moyo ukanistuka sana, kwani kwa umri wangu huu ni jambo zito sana kusikia kwamba nina pendwa na mtu anataka kuwa mchumba wangu, ikiwa hata maana ya mapenzi sifahamu.
“Ethan natambua kwamba una shangaa mimi kukuambia hivyo, ila huo ndio ukweli wa moyo wangu, nina kupenda sana, sipendi ninapo kuona na wasichana wengine nina jisikia wivu moyni mwangu”
“Ila Camila sisi bado ni watoto, tutawezaje kuhimili mikiki mikiki ya mapenzi yetu?”
“Si tutakua wakubwa, kwani kila siku tutabaki kuwa hivi. Lazima tuwe wakubwa na tukiwa wakubwa basi penzi letu litazidi kuwa kushamiri, tutafunga ndoa na kuzaa watoto wetu”
 
Nikazidi kushanga sana kumuona mtoto mdogo kama Camila akiwa na ujasiri wa kuzungumza mambo ambayo kwa umri wetu, endapo unazungumza tena ukiwa nchini Tanzania, basi ni lazima utachapswa sana na mzazi pale atakapo sikia kuhusiana na mazungumzo haya.
“Camila, huku kwenu unyanyasaji wa watu kama sisi ni mkubwa, nina ogopa?”
“Ethan hilo nitalichukulia uangalizi, hakuna mtu ambaye atakunyanyasa. Babu yangu ni raisi, babu yangu ana majeshi na ananipenda sana babu yangu, hivyo chochote ninacho mueleza ananisikiliza, na hakuna wa kukutisha sawa Ethan”
Camila alizungumza huku akivua gloves alizo vaa mikononi mwake kwa ajili ya kuzuia barini, akanishika mkono wangu wa kulia huku akinitazama usoni mwangu.
 
“Ethan nitakulinda kwa namna yoyote ile, nakupenda Ethan”
Camila alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake, hapa ndipo nikatambua kwamba jambo analo lizugumzia ana limaanisha kutoka moyoni mwake. Kutokana nina hitaji usalama wa maisha yangu ya hapa shuleni, sikuwa na budi zaidi ya kumkubalia. Camila akatabasamu, hapa ndipo nikazidi kuuona uzuri wake, japo ni mzungu ila amejaliwa uzuri na ujasiri mkubwa wa kuweza kuhitaji kumiliki chochote anacho kihitaji yeye.
Tukamaliza kupata chakula cha usiku na tukarudi mabwenini kwetu, huku wasichana wakielekea kwenye mabweni yao. Leo stori za wanafunzi wote ni kuhusian ana mimi pamoja na timu yangu, huku wengine wakijilaumu ni kwa nini kocha hakunianzisha mapema katika mechi iliyo pita.
 
“Umesha wahi kucheza mpira kabla ya leo?”
Mwanafunzi mwezangu aliniuliza.
“Hapana”
“Kweli?”
“Ndio haki ya Mungu, leo ndio siku ya kwanza kucheza mpira”
“Aisee unakwenda kuwa zaidi ya Messi na Christian Ronaldo”
Mwanafunzi huyo aliendelea kunimwagia sifa kedekede. Muda wa kulala ulipo fika, mlezi wa bweni letu akatuomba kila mwanafunzi aingie kwenye chumba chake na kulala. Mimi na rafiki zangu watatu tukaingia kwenye chumba chetu cha kulala, siku zote za nyuma sikuwa na maelewano nao mazuri, kutokanana rangi yangu ya mwili kwamba ni muafrika, ila leo hii wamekuwa ni watu ambao wana nisikiliza kwa kila kinacho kizungumza.
 
Tukaendelea kuzungumza mambo mbalimbali yanayo husiana na maisha ya hapa shuleni na familia zetu, baada ya mdua kidogo tukajikuta tukipitiwa na isingizi na watu wote tukalala usingizi fofofo.
‘Ethan’
Niliisikia sauti ya rafiki yangu ambaye hadi leo hajanitambulisha jina lake.
‘Naam’
‘Amka’
Rafiki yangu huyu alizungumza, taratibu nikanyanyuka kitandani, katika hali ambayo kwa binadamu wa kawaida hawezi kuifahamu, tukaanza kuondoka katika eneo hili huku kwa upande wangu nikiona ni jambo la kawaida sana.
‘Leo utaweza kuniona mimi na familia yangu’
‘Sawa, ila kwa kuna maswali nahitaji kukuuliza?’
‘Uliza?’
 
‘Hivi hamtishi nitakapo waangali?’
‘Hahaaa…hatutishi, kwa nini umefikiria kwamba tunatisha?’
‘Kwa maana kila siku ninaona kivuli chako na kama hivi tunavyo elea hewani, nina hisi uwepo wako tu ila sikuoni sura wala mwili wako’
‘Usijali utaniona tu’
‘Kweli?’
‘Ndio’
Tukafika baharini, maji yakaanza kuzunguka kama kimbunga kikubwa sana na kusababisha shimo kubwa sana, tukaanza kushuka kwenye shimo hili lenye maji, kila kitu kinacho tokea kusema kweli kina nishangaza. Tukafika katika mji mmoja mkubwa sana ambao watu wake ni tofati na binadamu.  Watu hawa wengi wao wanatembea hewani na si ardhini.
‘Maisha ya huko usije ukamuelea mtu wa aina yoyote na siku ambayo utazungumzia juu ya haya mambo basi maisha yako yatakuwa ni ya shida sana umenielewa Ethan?’
‘Ndio, naweza kuluuliza?’
‘Uliza?’
 
‘Kwa nini watu hawa wanatembea hewani na ni wazuri sana kuliko hata binadamu?’
‘Huu ni ulimwengu wa majini, kuna majini wabaya na majini wa zuri. Sisi ni majini wazuri’
Wasiwasi ukaanza kunijaa kidogo.
‘Usijawe na wasiwasi wowote, hadi kufika huku ujue nimekuchagua na tunataka uwe muwakilishi wetu mzuri duniani’
‘Muwakilishi wa mambo gani?’
‘Kadri siku zinavyo zidi kwenda na unavyo zidi kukua ndivyo jinsi utakavyo weza kufahamu ni uwakilishi gani ambao sisi tunauhitaji kwako’
Tukaingia kwenye jumba moja kubwa ambalo katika kuona kwangu majengo dunia, jengo hili sijawahi kuliona. Rafiki yangu huyu akaonekana umbo lake. Nikabaki nikiwa nimejawa na mshangao kwa maana ni kijana mdogo kama mimi na ni mzuri sana ila ana sauti nzito sana. 
 
‘Mbona wewe ni mdogo!!!?’
‘Yaa ulihisi mimi ni mkubwa sana’
Alizungumza kwa sauti nyinine ambayo ni tofauti na sauti ambayo anazungu akiwa katika mwili usio onekana. Tukaanza kutembea kwenye kordo ya jumba hili, wasichana wazuri na wanaume wazuri kila ambao ana kutana nao wana muinamishia kichwa chini huku wengine wakimpigia na magoti chini kabisa.
“Kwa nini wana kuinamia?”
Nilimuuliza huku tukizidi kusonga mbele.
“Mimi ni mfalme wa huku chini, baba yangu alifariki miaka miachache iliyo pita”
“Ngoja kwanza una taka kuniambia kwamba nyinyi muna kufa?”
“Ndio tunakufa, ila kuishi kwetu sio kama wa binadamu, miaka kumi hamsini mia. Ila sisi tunaweza kuishia kuanzia miaka elfu kumi na ndio tunaweza kufa”
“Heee”
 
Tukaingia kwenye moja ya ukumbi, ambao wote umesakafiwa kuanzia kuta, nguo kwa kutumia dhahabu. Tukaendelea kutembea hadi kwenye kiti kikubwa cha dhahabu na akaka na wote waliomo ndani ya ukumbi huu wakainama chini na kumsujudia. Akapiga kofi moja wakayanyuka na kwa ishara akawaomba watokea ndani humu na tukabaki sisi wawili.
“Hawa ni kina nani?”
“Ni wafanyakazi wangu ambao ninaweza kuwatuma sehemu yoyote ulimwenguni na wakaniletea chochote nitakacho kihitaji”
“Chochote kile?”
“Yaaa njoo ukae”
Alizungumza huku akinionyesha kiti kilichopo pemeni ya kiti cheke, ambacho nacho kimetengenezwa kwa madini ya dhabu.
“Huku ni pazuri sana”
“Yaa ni pazuri, alafu umesahau kuniuliza jina langu”
“Ndio. Unaitwa nani?”
“Nina itwa Ethan kama wewe”
“Acha kunitania bwana?”
“Niamini mimi, nina itwa Ethan, ndio maana niliamua kuwa rafiki yako toka siku tu ulipo saidia wa wale wazee”
 
“Kwa hiyo ulikuwa una nifwatilia?”
“Ndio, siku hiyo nilikuwa ninapita kwenye matembezi yangu ya kila siku, nikakuona ukiwa upata tabu, nilitaka kuwadhuru wale walio kuwa wakikupa tabu, ila nikawaona hawana la maana, walipo kutupa basi nikawa pamoja na wewe”
“Ngoja kwanza, ni kina nani ambao walinitupa?”
“Kwa sasa Ethan sio muda sahihi wa wewe kuweza kuwafahamu watu hao, ila jambo la msingi ni kuhakikisha kwamba una pata kile unacho kihitaji kisha hayo mambo mengine kadri jinsi tunavyo zidi kwenda ndivyo jinsi utakavyo zidi kuyafahamu”
“Sawa nimekuelewa”
“Wewe ndio binadamu wa kwanza kuwa rafiki yangu.Ila ninakuomba usije ukanisaliti siku hata moja, ukinisaliti kila kitu kitamu kwako nitakibadilisha na kitakuwa kichungu na urafiki wangu mimi na wewe utakufa sawa”
 
Ethan mwenzangu alizungumza kwa ukali kidogo na msisitizo, nikatingisha kichwa nikimaanisha kwamba nimemuelewa anacho kizungumza.
“Unahitaji nguvu si ndio?”
“Ndio”
Kwa ishara Ethan akaniomba nisimame mbele yake, akaniamrisha nipige magoti mbele yake na nikapiga kweli magoti. Akaniweka mkono wake wa kulia kichwani mwangu, mwili wangu mzima nikahisi kuna nguvu fulani inaniingia, Ethana akaendelea kunipatia nguvu hadi mwili wangu ukaanza kutetemeka, na mwishowe nikajikuta nikianguka chini na kupoteza fahamu.

==>>ITAENDELEA KESHO


from MPEKUZI

Comments