Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 05

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   

‘Wewe…..wewe…..’
Nilijitahidi kumuita ila hakuitika. Nikamaliza kula na nikaacha chombo changu hapa hapa juu ya meza kama utaratibu wa kawaida, kwani kuna wafanyakazia maalumu hushuhulika katika swala la kuosha vyombo, nikarudi bwenini, nikavua nguo zangu, nikajifunga taulo na kueleka katika bafu ambalo tunatumia wanafunzi wa darasa la kwanza kwenye bweni hili. Nikavua taulo langu na kulitundika kwenye msumari, nikajifunga taulo langu kisha taratibu nikaanza kuoga, nikiwa nimejipaka mapovu mwili mzima, akaingia bonge na kundi lake na wakaanza kunicheka huku wakizunguka jambo lililo sababisha nijawe na woga mwingi sana.

ENDELEA
“Wewe sokwe unajifanya hodari kupendwa na wasichana wetu si ndio?”
Bonge alizungumza huku akinisukuma sukuma, kwa woga nilio nao nikajikuta nikishindwa kufanya jambo lolote zaidi ya kushika sabuni yangu walio nikuta nayo.
“Mshikeni”
Bonge aliwaamuru wezake, ambao kwa haraka wakanishika mikono yangu, jambo lililo nifanya nianze kulia hata kabla sijapigwa.
 
“Hehehee, linalia jinga hili”
Bonge alizungumza hukua kicheka na kuwafanya wezake wote walio nishika kuanza kucheka kwa dharau, bonge akaanza kunipiga vibao vya mashavuni huku akiendelea kunicheke. Nikajitahidi kwa nguvu zangu ili mrdi nijitetea kwa vijana hawa ila sikuweza kufanya chochote zaidi ya kuendelea kupigwa vibao vya unyanyasaji na bonge huyu. Akanipokonya sabuni yangu na kuanza kunipakaza nayo kichwani kwa nguvu hadi nikaanza kunishi maumivu.
“Nataka hii rangi yako nyeusi itokea mwilini mwako”
 
Bonge alizungumza huku akiendelea kunisugua sabuni hii mwilini mwangu huku akihamia mgongoni mwangu. Kusema kweli machozi ya hasiri yalizidi kunimwagika. Baaada ya bonge kunifanyia vitendo hivi vya unyanyasaji, akaniamshirisha wezake kuniachia na nikaanguka chini huku nikilia kwa uchungu sana. Wakaongeza nguvu ya bomba hili la maji kisha wakatoka bafuni humu huku wakicheka sana. Taratibu nikanyanyuka huku moyoni mwangu nikijiapiaza kulipiza kisasi kwa bonge na wezake. Nikajitahidi kuoga huku nikiendelea kububujikwa na mchozi, nikamaliza na kurudi chumbani kwangu. Nikabadilisha nguo na kuvaa nguo za michezo huku nikiendelea kuwa na hasira yangu. Nikachukua viatu vyangu vya kuchezea mpira na kueleka uwanjani. Nikawakuta wanafunzi wa darasa la kwanza wakipangwa nani aanze kucheza kwenye mechi ya darasa la pili. Bonge na wezake nao ni miongoni mwa wachezaji walio jitolea katika kucheza mechi hii.
 
“Ethan”
Mwalimu wa michezo wa darasa langu aliniita huku akinitazama.
“Naam”
“Mbona macho yako ni mekundu, vipi una umwa?”
“Hapana mwalimu”
Nilijibu huku nikitazama chni, mwalimu kwa ishara akaniita na kuniwekea kiganja cha mkono wake wa kulia shingoni mwangu ili kunipima joto la mwilini mwangu.
“Joto lako lipo vizuri”
Aliniambia huku akiendelea kunishika shika kwenye shingo yangu.
 
“Ben”
Mwalimu na Bonge akaitika, hapa ndipo nikafahamu jina halisi la bonge.
“Unacheza namba gani?”
“Mfungaji mwalimu”
Nikatamani kucheka kwa kweli, kwa maana huyo anaye sema anaweza kucheza nafasi ya ufungaji ni kibonge hata kutembea kwake ni shuhuli, kinacho mpa uhodari kidogo ni wezake anao tembea nao. Mwalimu wa darasa letu akapanga kikosi chake cha kwanza na mimi na wezangu wengine tukabaki nje. Wachezaji wakapewa jeshi na wakaingia kiwanjani. 
 
“Mbona wewe hujachaguliwa?”
Sauti ya kike ikanistua na kugeuka nyuma, nikamuona binti aliye nisaidia muda wa machana nilipo kuwa nina nyanyaswa na kina bonge akiwa amesimama nyuma yangu huku na yeye akiwa amevalia nguo za mazoezi na walinzi wake wakiwa pembeni yake.
“Nitacheza tu”
“Nawewe kukaa”
Aliniuliza huku akionyesha sehemu ya pembeni yangu ambayo haina mtu katika benchi hili.
“Sawa unaweza kukaa”
 
Taratibu akakaa huku akiwa na tabasamu pana sana.
“Kwa nini wewe hujaenda kucheza na wezako”
“Mimi sipendelei sana michezo ya kike, ninapenda sana mpira”
“Mmmm….sasa huku wanacheza wanafunzi tu wa kiume?”
“Yaa ila nikipata nafasi na mimi nitacheza”
“Hahaaa..unapenda kucheza nafasi gani?”
“Golikipa”
“Weeee huoni ni nafasi ambayo ni hatari”
Msicha huyu hakunijibu chochote zaidi ya macho yetu kuyapeleka golini kwetu na tukashuhudia goli likiingia kwneye nyavu ya goli letu. Mpira ukaanza tena, mwanafunzi mwenzetu akampatia pasi bonge, ila bonge badala ya kupiga pira akapiga hewa na kuanguka chini kama kifurushi cha chumvi. Nikamuona mwalimu akifumba macho yake kwani yeye ndio kama kocha.
 
“Hhahaa ujanja wa bure nje, kumbe uwanjani ni mpuuzi”
Nikatamani kusema kitu ila nikaishia kukaa kimya tu.
“Wamekuone tena baada ya pale holini?”
“Hapana”
“Una uhakika?”
“Ndio”
“Hili bonge linakivunia nafasi ya baba yake kuwa mkuu wa shule nzima, ndio maana linakuwa jeuri”
“Ahaaa kumbe baba yake ni mkuu wa shule”
“Ndio, ila mimi ndio niyamkomesha kwa maana baba yake hata kwangu hazungumzi chochote”
 
“Unaitwa nani?”
“Mim?”
“Ndio”
“Naitwa Camila”
“Aha una jina zuri”
“Asante na wewe ulisema unaitwa nani vile?”
“Ethan”
“Sawa sawa”
Tukashuhudia goli la pili likiingia, hazikupita hata dakika mbili tukafungwa goli la tatu, na mpira ukaenda dakika za mapumziko. Bonge akwa na kazi ya kuwafokea wezake huku akitoka uwanjani akiwa amenunua sana. Wachezaji wakaka chini huku tukiwa tumemzunguka mwalimu wetu wa darasa. Mwalimu akaanza kupanga kikosi wachezaji nilio kuwa nao nje, wakaambia watacheza kipindi cha pili huku mimi peke yangu nikiwa ndio nimeachwa.
“Mwalimu mbona Ethan haujamuingiza”
 
“Hatuta……”
Bonge akaanza kuzungumza, ila Camila akamuonyeshea ngumi na kumfanya bonge kukaa kimya.
“Atacheza ngoja tuwajaribu na hawa wezake”
“Sawa”
Camila akanitazama huku akitabasamu na kunifanya kidogo nijawe na amani kubwa sana moyoni mwangu, kumpata rafiki ambaye kusema kweli ameanza kuwa mtetezi wangu mkubwa kutoka kwa kina bonge na kundi lake. Bonge na wachezaji wengine wakaingia katika kipindi cha pili cha mchezo huku bonge akiwa amefungw akitambaa cha uongozi wa timu. Kusema kweli mwalimu ana mpendelea bonge ila hajumudu kwa lolote uwanjani, zaidi ya kupiga piga tu kelele. Kuingia na kuingia tukafungwa goli la nne lililo mfanya mwalimu kukasirika sana.
 
“Mwalimu kwani Bonge ana msaada gani uwanjani?”
Camila alizungumza kwa hasira huku akimtazama mwalimu. Mwalimu akameza tu mate na kukaa kimya.
“Unamuogopa kwa sababu baba yake ni mkuu wa shule. Sasa mtoe na mimi babu yangu ni raisi”
Camila alizungumza kwa msisitozo nikamuona mwalimu akizidi kuwa mnyonge sana na akapata kigugumizi cha kufanya maamuzi. Mwalimu akamuita refa msaidizi na kumuambia kwamba anahitaji kufanya mabadiliko ya timu.
“Ila wewe unaweza au naingiza ugonjwa zaidi?”
Mwalimu aliniuliza kwa jazba kidogo jambo ambalo likaufanya moyo wangu kufedheheka kidogo.
“Nitaweza”
 
Nilibu kinyonge huku nikimtazama mwalimu usoni mwake. Mpira ulipo toka bonge akaambiwa kwamba anatakiwa kutoka jambo lililo mfanya bonge kukasirika sana. Nikakabidhiwa jezi yenye namba tisini na tisa mgongoni mwangu, yaani namba ya mwisho kwenye mpira.
“Jitahidi Ethan sawa”
Camila alizungumza kwa kuninong’oneza
“Sawa”
Bonge akanitazama kwa macho makali, akashindwa kunifanya chochote kwa maana amemuona Camila akiwa amesimama pembeni yangu. Alipo fika nje ya uwanja akavua kitambaa cha mkononi mwake na kukitupa chini, nikakiokota, nikataka kukivaa ila mwalimu akakataa na kuniambia nikamkabidhi kipa wetu. Nikakimbia huku nikielekea golini, nikamkabidhi golikipa kitambaa na akajifunga mkononi mwake.
 
‘Nicheze wapi Mungu wangu’
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikiuona uwanjani ni mkubwa sana. Nikawaona washambuliaji wa darasa la kwanza wakija kwa kasi, nikajaribu kumzuia mwenye mpira, ila nikastukia kuona mpira ukipita katikati ya miguu yangu kisha akakimbilia mbele kidogo na kufunga goli la tano. Nikamtazama Camila huku mapigo ya moyo yakinienda kasi sana, woga ukanijaa. Nikimtazama mwalimu, sura yake imejaa hasira, nikiyahamishia macho yangu kwa bonge, yeye ndio usisema, naona hata pale alipo ananitukana matusi mengi sema tu siyasikii kutokana nipo mbali naye.
“Usiogope”
Mchezaji mmoja wa darasa la pili aliye nipitishia mpira wangu katikati ya miguu alizungumza huku akinipiga begani mwangu. 

Wezangu wawili wakachukua mpira na kuuweka katikati ya kiwanja huku mimi nikiwa nje ya dura hili kubwa. Wakanza mpira, na cha kushangaza wakanipatia mpira na wakatawanyika kuniachia kizaa zaa hichi. Nikatazama goli la wapinzani wangu, nikashusha pumzi kidogo kisha nikapiga mpira huu kwa mguu wangu wa kushoto, mpira kwa kasi huku ukielea elea hewani, ukafika golini, na golikipa wa darasa la pili akashindwa kuudaka na ukaingia nyavuni.
 
Nikabaki nikiwa nimeshikwa na butwaa, wanafunzi wenzangu wakaanza kunirukia huku wakishangilia, ila nikashindwa hata nifanye nini kwani sijui imekuwaje hadi mpira huo kufika golini. Nikamtazama Camila nje ya uwanja, nikamuona akininyooshea dole gumba huku akitabasamu.
“Ethan unaweza, unaweza”
 
Wezangu walinipa moyo huku wakitawanyika. Wachezaji wa darasa la pili wakaanza mpira, mchezaji wetu mmoja akafanikiwa kuwapokonya mpira huu na kunipasia, nikautuliaza huku nikiwaangalia wachezaji wa darasa la pili wanavyo nifwata, nikaanza kuichezesha miguu yangu kwa kuizungusha juu ya mpira, wakajaribu kuuchukua, ila nikaugusa kidogo na wakaukosa, nikaanza kukimbia kuelekea golini mwao, kila mchezaji wa darasa la pili alipo jaribu kunifwata, nilijikuta nikimtoka na akaukosa mpira huu, nilipo fika golini nikamtisha kipa kama ninapiga mpira huu kulia, jambo lililo mfanya kipa kuruka kulia, ila kwa mguu wangu wa kushoto nikaupeleka mpira huo upande wa kushoto na kuzifanya nyavu za goli la darasa la pili kutingishika. Goli hili kusema kweli, likanifanya niruke kwa furaha. 
 
Nikakumbatiana na wachezaji wezangu kwani tuna matumaini ya kukomboa magoli matatu yaliyo salia.
‘Hii ndio nafasi ya wewe kuwa na nguvu hapa shule’
Nilimsikia rafiki yangu akiniongelesha katika ufahamu wangu wa akili.
‘Kweli’
‘Ndio, hakisha kwamba watu wanakujua wewe ni nani?’
‘Sawa’
Mpira ukaandelea, nikafanikiwa kuuchukua mpira huu na kama kawaida, nikawachenga wachezaji wa darasa la pili, nilipo fika golini, nikampatia mchezaji mwenzangu, akapiga shuti zito na tukafunga goli la tatu. Uwanja ukaanza kujaa, wanafunzi na waalimu walio kuwa wakiendelea na michezo mengine, wakaanza kuhamia kwenye huu uwanja. 
 
“Tumebakisha goli mbili, tunaweza kujitahidi sawa”
Niliwahimiza wezangu mara baada ya kumaliza kushangilia goli letu hili. Wachezaji wa darasa la pili wakazidi kuchanganyikiwa, kwani mashambulizi yalizidi kuwaelemea, hatukumaliza hata dakika mbili, mchezaji wetu mwengine akapiga kichwa mpiwa nilio piga nikiwa pembeni ya uwanja na kufunga goli la pili.Shangwe zikazidi kurindima uwanjani hapa, watu wakasahau kama tunao cheza hapa ni watoto, ila burudani tunayo itoa kwa kweli ni ya kukata na shoka.
 
“Ethan, Ethan”
Mwalimu aliniita, kwa haraka nikamkibilia hadi alipo na kumshikiliza.
“Tuna dakika tano, jitahidini mukomboe”
“Tano?”
Nilimuliza huku nikimwagikwa na jasho mwili mzima.
“Ndio”
“Sawa mwalimu”
“Ethan”
Camila aliniita, akanionyeshea vidole viwili, nikamnyooshea dole ngumba kwa mkono wangu wa kulia kisha nikarudi kiwanjani. Mpira ukaanza, kutokana nimesha ujua udhaifu wa wachezaji hawa wa darasa la pili, nilicho kifanya ni kuumiliki mpira, kasi na nguvu alizo nijalia Mungu kusema kweli, zinanisaidia kuweza kuminyana nao wanafunzi hawa. Wachezaji wote wa darasa la pili wakawa wananikaba mimi na kuwasahau wezangu, nilipo fika golini kwao kwa bahati mbaya wakanichezea rafu na refa akaweka ipigwe penati. 

Wezangu wakaniomba nipige penati hiyo ila nikakataa, akapiga golikipa wetu, na kwa bahati nzuri akafanikiwa kufunga, ubao wa magoli ukaonyesha goli ni tano kwa tano. Nikamuona mwalimu wetu akikenua meno yote thelathini na mbili yanaonekana, akanionyeshea kwamba zimebaki dakika mbili kabla ya mpira kuisha, mpira katika kuchezwa kwa bahati mbaya ukatoka katika upande wa darasa la pili na refa akaamuru ipigwe kona. 

Tukakusanyika golini mwa darasa la pili, mchezaji wetu mmoja akapiga kona moja maridhwa, bila ya kuhofia kwamba nitaumia au kuvunjika, nikaruka juu na kupiga tikitaka moja nzuri na mripa ukaingia golini, na kuufanya uwanja mzima kujawa na rufaha, wezangu wakanilalia hapa chini nilipo anguka huku machozi ya furaha yakinimwagika usoni mwangu. 
 
“ETHAN….ETHAN…..ETHA…..N”
Uwanja mzima uliimba jina langu, wezangu wakanisaidia kunyanyuka na tukarudi upande wetu. Kitendo cha darasa la pili kuanza mpira, refarii akapiga kipinga cha mwisho akishiaria kwamba mpira umekwisha. Nikamuona Camila akiingia kwa kasi uwanjani, breki ya kwanza akanirukia na kunikumbatia kwa nguvu huku akiliwa kwa furaha. Mechi tu ya kirafiki imeonekana kama mechi ya mashindano makubwa ya kugombania kombe. 
 
“Nakupenda Ethan, nakupenda sana Ethan”
Camila alizungumza huku akiendela kunikumbatia kwa nguvu na machozi yakizidi kumiminika usoni mwake, nikajikuta nikishindwa hata kuzungumza kwani hara rafiki zake bonge walio nipiga leo bafuni, wote wakanifwata na kunikumbatia, kasoro Bonge tu yeye mwenyewe ndio amebaki nje ya uwanja huku akiwa amenuna sana na dhairi anaonyesha kwamba bado ana kinyongo na mimi.

==>>ITAENDELEA KESHO


from MPEKUZI

Comments