RC Makonda Afunguka Tukio la kutekwa Mo Dewji

Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda amezungumza akiwa eneo la tukio ambalo leo October 11, 2018 Mfanyabiashara maarufu nchini MO Dewji ametekwa akiwa anaingia Gym alfajiri.

Amesema tayari upekuzi umeshaanza katika maeneo yote muhimu hasa kwenye hoteli, nyumba za wageni, mipakani na kwenye viwanja vya ndege kuhakikisha jeshi  linanasa mtandao wa watuhumiwa waliohusika na utekaji huo

RC Makonda amefafanua kuwa miongoni mwa watekaji nyara, wapo wazungu wawili, hali inayoonyesha  kuwa tukio hili limefanywa na wenyeji kwa kushirikisha na  raia hao  wa kigeni.

Amesema  baadhi ya walinzi na wahudumu wa Gym ya Colosseum wamekamatwa ili kulisaidia jeshi la polisi maana wao ndo wanajua ni gari gani ilifika pale, ilikuwa na watu gani na walikaa muda gani


from MPEKUZI

Comments