Rais Magufuli Kakutana na Viongozi Mbalimbali Ikulu Leo Na Kukubali Kuteuliwa kuwa makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)

Rais John Magufuli, amepokea rasmi taarifa ya uteuzi wa kuwa makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC),  kwa mwaka mmoja kuanzia Agosti 2018 - Agosti 2019.

Taarifa hiyo imekabidhiwa kwa Rais Magufuli leo Oktoba 8, 2018 na Katibu mtendaji wa Jumuiya hiyo Dkt. Stergomena Tax, ambaye amesema amekutana na Rais Magufuli ili kumpa taarifa ya uteuzi uliofanyika kupitia mkutano mkuu wa 38 wa SADC ambao ulifanya Agosti 17-18, 2018 mjini Windhoek nchini Namibia.

Taarifa ya Ikulu imeeleza kuwa kufuatia uteuzi huo sasa Rais Magufuli atakuwa ndiye Mwenyekiti wa SADC ajaye katika kipindi cha mwaka 2019/2020 ambapo atahudumu kwa mwaka mmoja kama ilivyokawaida.

Kwa upande wake Rais Magufuli ameeleza kuwa ameupokea kwa heshima kubwa uteuzi huo na yupo tayari kufanya kazi hiyo kwa kushirikiana na wenzake kwa manufaa ya nchi zilizopo kwenye jumuiya hiyo.



from MPEKUZI

Comments