Radi Yaua Wanafunzi 6 na Kujeruhi Wengine 25

Wanafunzi sita wa shule ya msingi, Emaco Vision iliyopo mjini Geita wamefariki dunia baada ya kupigwa na radi wakiwa darasani huku wengine wakijeruhiwa wakiwamo walimu wawili.

Tukio hilo limetokea leo Jumatano Oktoba 17, 2018  saa 3:30 asubuhi. Wakati mvua ikinyesha na radi kubwa kupiga.

Ofisa elimu msingi, Yese Kanyuma amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kusema hadi sasa majeruhi ambao bado wako hospitali ni 25.


from MPEKUZI

Comments